Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Wananchi tusivunjike moyo, mpira ndo ulivyo leo bahati haikuwa kwetu tusimlaumu sana kocha wachezaji wamepambana penalty hazina mwenyewe

Yanga daima mbele nyuma mwiko
 
Tangu nabi aondoke timu inasuasua tu na hizi sare zilimcost kaze mwaka jana jamaa anapenda kujilinda sana.
 
Kaze aache ujinga mechi zote anataka saido aanze na amalize dk 90 akumbuke waliopo benchi nao niwachezaji wa yanga sasa nimeelewa kwanini pablo hataki wasaidizi
 
Wananchi tusivunjike moyo, mpira ndo ulivyo leo bahati haikuwa kwetu tusimlaumu sana kocha wachezaji wamepambana penalty hazina mwenyewe

Yanga daima mbele nyuma mwiko
Hakuna kupambana. Coach abebeshwe msalaba
 
Ishu sio hadhi ya mashindano

Ishu ni kocha msaidizi hakubaliana na falsafa ya kocha mkuu na hii inatengeneza mkanganyiko.

Fei anachezeshwa second striker, yeye kamrudisha namba 8.

Naweza kutoa mifano zaidi

Mwanauto mwenzangu.

Tufukuze msaidizi kocha kisa Ndondo?

Haikubaliki.
 
Ishu sio hadhi ya mashindano

Ishu ni kocha msaidizi hakubaliana na falsafa ya kocha mkuu na hii inatengeneza mkanganyiko.

Fei anachezeshwa second striker, yeye kamrudisha namba 8.

Naweza kutoa mifano zaidi
Kaze analeta matabaka kwa wachezaji, yeye saido ndio chaguo lake kwenye kila first eleven yake
 
Kocha gani?

Nabi au kaze?
Ukiacha pre season, mechi kama hizi ndio za kujaribu mifumo na wachezaji.

Lakini tupotaka tukaze tuu mpaka wachezaji wasiopata namba waendelee kusugua benchi naona sio sawa.

Ukizingatia mechi yenyewe tumetolewa kwa matuta.

Tungefungwa ndani dakika 90 si bakora zingetembea?

Kufungwa kunaumiza na hasa mtani wako akiwa anafanya vizuri lakini sijaona sababu ya kureact namna hiyo.
 
Kwa hiyo na leo tulikuwa tunawajaribu wachezaji?

Kulingana na majaribio tuliyofanya kupitia haya matokeo tuliyoyapata, hawa wachezaji wanatufaa au hawatufai?

Au tuwape muda wa kutosha zaidi kuendelea kuwajaribu?
 
Wananchi tusivunjike moyo, mpira ndo ulivyo leo bahati haikuwa kwetu tusimlaumu sana kocha wachezaji wamepambana penalty hazina mwenyewe

Yanga daima mbele nyuma mwiko
Nakubali sana mwamba kiu yetu kubwa ni kombe la ligi kuu... Hapo tisifanye masikhara kabisa aisee

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kaze ni kocha wa daraja la chini sana...

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…