Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Tujiandae vyema wana jangwani Township rollers wameapa lazima waje watoe kipigo cha mbwa koko.
Tujitahidi tufute aibu wale jamaa wa mwituni wasije kutucheka.
 
Nini lakini Mtani?
Hebu wacheni kututoa kwenye reli.
Najaribu kuwakumbusha wana jangwani wenzangu nikiwa kama mzalendo/mfia timu wa chama letu la Yanga, chonde chonde kama ni kutufunga basi watufunge angalau 3 tu zikizidi sana 4, tusiogope kuchekwa na wale wa mwituni ndio kujifunza huko pia ndio ukubwa huo.
Kila laheri chama kubwa Yanga sc
 
Najaribu kuwakumbusha wana jangwani wenzangu nikiwa kama mzalendo/mfia timu wa chama letu la Yanga, chonde chonde kama ni kutufunga basi watufunge angalau 3 tu zikizidi sana 4, tusiogope kuchekwa na wale wa mwituni ndio kujifunza huko pia ndio ukubwa huo.
Kila laheri chama kubwa Yanga sc
Dua la kuku hilo Mtani. πŸ’ƒπŸ’ƒ
 


20190806_141303.jpg

20190806_141550.jpg

20190806_141538.jpg
20190806_141527.jpg



20190806_141516.jpg

20190806_141500.jpg




 
20190807_063915.jpg

SALAMU ZA SHUKRANI*

Uongozi wa klabu ya Yanga unatoa shukrani za dhati kwa Wanayanga wote, Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wote kwa namna walivyoipokea wiki ya Mwananchi, na kujitokeza kwa wingi katika ushiriki shughuli mbalimbali za kijamii katika wiki ya Mwananchi zilizofanyika nchini kote Tanzania Bara na Visiwani.

Kama mnavyofahamu, shughuli nyingi zimefanyika kwenye wiki hii ambazo zimehusisha mambo yafuatayo;
1. Ukarabati wa Majengo ya Hospitali,Vituo vya afya,zahanati na majeno ya taasisi za umma.
2. Kutoa misaada kwa makundi maalum yenye uhitaji katika jamii.
3. Kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya wazi, ya umma kote nchini .
4. Kuchangia damu na kuhamasisha umma wa watanzania kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu katika Benki ya damu.

Tunaishukuru Serikali katika ngazi zote kwa kuruhusu Wanayanga kufanya mambo waliyokusudia katika wiki hii, vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa waliyoifanya wiki nzima hadi jana siku ya Kilele, Tunavishukuru Vyombo vya Habari nchi nzima kwa kazi nzuri waliyoifanya kuwahabarisha Wananchi juu ya matukio mbalimbali ya Wiki ya Mwananchi.

Tunaishukuru kamati ya Hamasa pamoja na kamati ya `utendaji ya Yanga kwa kazi kubwa ya uratibu wa shughuli hii, na zaidi tunawashukuru sana Wanayanga kwa kujitokeza kwa wingi jana kwenye hitimisho la wiki ya Mwananchi. Shukrani hizi pia ziende pamoja na pongezi za dhati za Uongozi wa Yanga kwa makundi hayo kwa kazi zao ambazo zimeipa heshima na faraja klabu yetu.
Tunafahamu sote kwamba Wiki ya Mwananchi imefikia tamati jana kwa mafanikio makubwa sana, lakini niwakumbushe tena kwamba mbele yetu kuna jukumu linguine la mchezo wa Kimataifa dhidi ya TownShip Rollers ya Botswana siku ya `jumamosi tarehe 10.08.2019 . Hivyo basi Tunawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga, kwa ari,upendo na mshikamano ule ule wa jana na hamasa ya Wiki nzima iendelee kwenye mchezo huo, tujitokeze kwa wingi sana kuipa nguvu timu yetu siku ya mchezo huo ili kuhakikisha tunapata ushindi.

Uongozi unaamini kwamba hamasa hii haitapoa kuelekea kwenye mchezo huo na hata Ligi itakayoanza baadaye mwezi huu. *Dr. Mshindo Msolla*
*Mwenyekiti-Young* *Africans Sports Club*
 
Back
Top Bottom