Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Msimu ujao mimi kama mshabiki wa Yanga, sitegemei kumuona Mwinyi Zahera na Noel Mwandila kwenye benchi la ufundi! Kiufupi tu, hawana jipya. Tunahitaji walimu wapya! Ikibidi mwalimu msaidizi awe mzawa na mwenye mapenzi ya dhati na timu yetu.

Nategemea uongozi ulioko madarakani, utaanzisha mara moja mchakato wa kuibadili timu na kuwa kampuni kama ilivyo kwa watani wetu wa jadi, Simba! Hii ni moja ya ahadi ya Mwenyekiti Dr. Mshindo Msolla wakati anagombea nafasi yake ya uenyekiti! Asidhani tumesahau.

Nategemea kuiona Kamati makini ya usajili kama ile ya akina Abdallah Bin Kleb na mwenzake Seif Magari! Iliyosajili wachezaji makini kiasi cha kuifanya Yanga kuwa mabingwa kwa miaka mitatu mfululizo. Wachezaji wote wa kawaida, wapewe mkono wa kwaheri ili timu irudi kwenye hadhi yake.

Kumuachia mtu mmoja tu kama mlivyompa uhuru Mwinyi Zahera kufanya mapendekezo na mwisho wa siku kusajili wachezaji wa kawaida, huku akiwaacha wachezaji wazuri, ni upuuzi usiovumilika.
 
Kutoka kwa mchambuzi ALI KAMWE [emoji116]

Mambo 10 nilioyaona Yanga Vs Pyramids

1: Pyramids [emoji119]. Ni ngeni Afrika lakini ina wachezaji bora na wazoefu kwenye michuano ya Afrika. Comfortable win wakiwa away[emoji119] .
.
2: Zahera dah[emoji114] Naheshimu sana kazi ya makocha lakini ni vyema sasa na yeye akaanza kujitathimini. He is so poor kimbinu/kiufundi. Wachezaji wote bora wa Yanga wanafia kwenye mpango kazi wake. Makame mwenye sifa ya kupiga pasi ya mita 25, leo anastrago kupiga pasi ya mita 5? Kweli.

3: Takwimu zinazungumza kwa makini ubovu wa mbinu za benchi la ufundi la Yanga. No way timu iko nyumbani inamuachia mgeni possession, inakosa mpango wa kaunta, inacheza rafu nyingi, inaongoza kadi za njano na nyekundu. Ilikua ngumu sana kujua Yanga wanatafuta bao kwa mpango gani.

4: Tshishimbi! Tunamlaumu bure kwa uzururaji wake uwanjani. Plan ya mwalimu mwanzoni ilielekeza hivyo. Baadae, kuja kwa Sibomana na Balinya kukawapunguza kasi Pyramids na ndio Papy alipokuja 'kuenjoy' mpira dakika 10 za mwisho. Kwa kuongezea, kocha wa Pyramids amesema amevutiwa na wachezaji wawili wa Yanga, FeiToto na Tshishimbi. This means, individual, Papy bado ni mchezaji mzuri aliyeangushwa na mpango wa Zahera.

5: Bado Yanga hawakujiandaa kucheza ma Pyramids uwanjani. Maandalizi yao mengi waliwaweka kwenye promotion na sio ufundi. Pyramids wamefunga mabao ambayo wamezoea kuyafunga kwenye mechi zao za ugenini
.
.
6: Mrisho Ngassa! Alicheza mechi ya kimataifa akiwa na akili za Mwadui. Lile ni kosa la kitoto sana kufanya na mchezaji mwenye uzoefu kama yeye
.
.
7: Kelvin Yondani[emoji119] Nenda kapumzike Soja. Kwa dakika zote alikua na kazi ya kuokoa, kumpanga Shikalo, kumpanga Ali Ali, kumpanga Makame. No way angeweza peke yake kuibeba Yanga pale nyuma.

8: Juma Balinya[emoji119] 'Top Striker' anayemalizwa na mahaba ya Zahera kwa Molinga. Hadi katika mechi muhimu Yanga wanayohitaji matokeo, miguu ya Balinya inakosa thamani
.
.
9: Ali Sonso anaendelea kuteseka na kudharaulika katika upande ule. Huenda aliwahi kucheza lakini ukweli ni kuwa, anakua bora sana akiwa beki wa Kati.

10: FeiToto[emoji119] Mchezaji bora wa mechi kwa Yanga, aliyefanyiwa sub na Zahera. No comment
(Ali kamwe)
 
20191028_070322.jpg
 
Back
Top Bottom