Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Hahaha dah Mtani!!una data kamili mie nishajisahau hivyo!!


Ila mtani unajua kuna kuvunja mkataba eti!!!Njaa haivumiliki

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaa. Pole Mtani mambo za Koona hizo zinafanya tunasahau mambo mengine kwani macho na masikio ndio tumeelekeza huko.

Sidhani Mtani kama anaeza fanya hivyo. Hatuna njaa mbona.
 
YANGA YATAKIWA KUTUMIA MAWAKALA WAZOEFU KUFANYA USAJILI

Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga Hans van Pluijm amesema utaratibu mbovu wa usajili ndio sababu inayopelekea mabingwa hao wa kihistoria wasajili wachezaji wenye viwango vya kawaida.

Pluijm ambaye aliisaidia Yanga kutwaa mataji mawili mfululizo ya ligi kuu misimu ya 2014-15 na 2015-16, amesema ili kupata wachezaji wazuri sokoni, Yanga inapaswa kurudi kwenye utaratibu wa kutumia Mawakala wazoefu.

Pluijm aliyewahi kupita vilabu vya Singida United na Azam Fc, amewataka mabosi wake hao wa zamani kuacha kusajili wachezaji kwa kutumia taarifa za mitandaoni kwani mara nyingi taarifa hizo hasa video zinazowekwa Youtube kuwahusu wachezaji hao ni zile ambazo wameonekana kufanya vizuri "Nimeifuatilia Yanga na nimegundua wanakosea kwenye usajili, kwani wanasajili wachezaji kutoka nje wa kiwango cha chini na kushindwa kuonesha ushindani, lakini hawajachelewa, kama wanahitaji wachezaji wazuri wanatakiwa kutumia mawakala wazoefu," amesema.

Pluijm alisema kama Yanga wanahitaji kuchukua ubingwa unaoshikiliwa na watani wao Simba, wanatakiwa kuacha kusajili wachezaji kimazoea kama miaka iliyopita, kwani mambo yamebadilika na ikiwa wanahitaji mchezaji mzuri lazima wakubali kupita njia sahihi kwa kutumia Mawakala "Unajua siku za hivi karibuni kumeibuka mazoea watu kusajili wachezaji kupitia mitandao, lakini wengi wao wamekuwa wakidanganya na mwisho unapata mchezaji anayekuja kukalia benchi badala ya kuwa msaada kwenye timu".

Pluijm ni mmoja wa makocha ambao wameacha historia nzuri kunako klabu ya Yanga katika muda ambao aliinoa timu hiyo.

@Yangafulldozz.
 
Hahah Gsm tangia hapo hali si hali

Nyie mlimfanya manji kafilisika mana kila mtu alikuwa analisha hadi familia za wachezaji(huu utani mwingine huu[emoji87][emoji87]

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya ni yako Mtani ila sisi tunajua GSM yuko vizuri.

Cha ajabu mnatujua kuliko tunavyojijua Mtani. Sema Manji alifilisiwa na yule naniliu yule 😷 kwa kumpa k e s i za kila aina mpaka akafilisika na si Timu yaWananchi.
 
Ni ukweli huo Mtani inabidi tubadilike sababu Timu kubwa kama Yanga kujaza magarasa haifai aisee.

Niliona sehemu anasema kwa sasa anajifua kwa nguvu zote na mpaka Corona ikiisha tutamsahau kwani atakuja kivingine kabisa. [emoji23][emoji23]
Hahah Jamaa anajiamini sana ila Ndio hivyo akili inataka ila mwili unakataa..

Ila kwa huyu wanaYanga siwacheki mlimkataa mapema mno sema ndio hivyo viongozi wanajiletea magarasa wanayoyataka!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ni yako Mtani ila sisi tunajua GSM yuko vizuri.

Cha ajabu mnatujua kuliko tunavyojijua Mtani. Sema Manji alifilisiwa na yule naniliu yule [emoji40] kwa kumpa k e s i za kila aina mpaka akafilisika na si Timu yaWananchi.
Hahah huko mie sichangii [emoji2089][emoji2089][emoji2089]

Ngoja nirudi nyumbani nikajifukize[emoji4][emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kidunula1 na Chikwuemeka naona kama Pluijm yuko sahihi.

Kwani na sisi tulizidi kusajili wachezaji ilimradi tu mwishowe wakawa watazamaji tu huku wanakula mshahara wetu pasi kuisaidia timu.
Yeah yupo sahihi,hasa wa kimataifa maana bora kusajili watano wa uhakika kuliko kusajili 10,wawili au wanne ndiyo wanapambana wengine ukiwa angalia hamna kitu........
 
Movement nzuri hii!
YANGA KUZINDUA WEBSITE NA APPLICATION

Uongozi wa Yanga umepanga kufanya uzinduzi mkubwa wa Website na Application ya Yanga Sc.

Afisa habari wa Yanga Sc Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kipo tayari kwa sasa hivyo mashabiki wajiandae ku support timu yao kwa kuweza (kupakua) download app rasimi ya Yanga Sc.

Uzinduzi huo unatarajia kufanyika siku ya Alhamisi Makao Makuu ya Klabu na matukio yote yatakuwa Live kupitia platform mbali mbali za mitandao ya kijamii ya Yanga Sc.

@Yangafulldozz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom