Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Usikose kuangalia kipindi cha Tamasha la Michezo ITV kuanzia saa nane mchana ili umshuhudie Kocha Liston Katabazi akieleza kwa undani madudu ya TFF na ubadhilifu wa pesa unaofanywa na viongozi wachumia tumbo wa shirikisho hilo ambao ndio chanzo cha kudumaa kwa mchezo wa Soka hapa nchini.
 
Nyinyi hamumtaki? Au ndio sizitaki mbichi hizi hahahaha. Hamna timu nyie
Hahahaa.

20200316_151541.jpg
 
Usikose kuangalia kipindi cha Tamasha la Michezo ITV kuanzia saa nane mchana ili umshuhudie Kocha Liston Katabazi akieleza kwa undani madudu ya TFF na ubadhilifu wa pesa unaofanywa na viongozi wachumia tumbo wa shirikisho hilo ambao ndio chanzo cha kudumaa kwa mchezo wa Soka hapa nchini.
Mkuu huyo Katabazi ameshaharibu mambo huko.

20200510_191938.jpg
 
Shadeeya

Unaonekana wewe ni mwana Yanga kindakindaki

Hongereni kwa timu ya Wananchi kuzindua Jarida lao, App yao na Website yao

Ila website hiyo waambie haipo secured, Yanga ni taasisi kubwa Tanzania (Hata Manara anajua) warekebishe Jambo hilo
 
Shadeeya

Unaonekana wewe ni mwana Yanga kindakindaki

Hongereni kwa timu ya Wananchi kuzindua Jarida lao, App yao na Website yao

Ila website hiyo waambie haipo secured, Yanga ni taasisi kubwa Tanzania (Hata Manara anajua) warekebishe Jambo hilo
Shukran Mkuu.

Tulishawasilisha hili Mkuu na wanalifanyia kazi.

Manara anaachaje kujua sasa Mkuu. 😅😅
 
Shukran Mkuu.

Tulishawasilisha hili Mkuu na wanalifanyia kazi.

Manara anaachaje kujua sasa Mkuu. 😅😅

Halafu na App pia watu wengine wanalalamika kuwa wanashindwa kuipakuwa, hapa inawezekana wanashindwa kuelezwa njia sahihi ya kuipakuwa App hiyo (Wengi wao waliojaribu kuipakuwa Mara ya kwanza ikawagomea kabla ya App kufanyiwa marekebisho)

Kama kweli wewe ni Yanga Kindakindaki nitunuku jezi chapa GSM kwa maoni niliyotoa hapa * Ninatania* ... Sitanii
 
Halafu na App pia watu wengine wanalalamika kuwa wanashindwa kuipakuwa, hapa inawezekana wanashindwa kuelezwa njia sahihi ya kuipakuwa App hiyo (Wengi wao waliojaribu kuipakuwa Mara ya kwanza ikawagomea kabla ya App kufanyiwa marekebisho)
Oooh. Lilishaisha hilo.
Kama kweli wewe ni Yanga Kindakindaki nitunuku jezi chapa GSM kwa maoni niliyotoa hapa * Ninatania* ... Sitanii
Duuh!!
 
TUNATAKA KWENDA KISASA ZAIDI "LUC EYMAEL"

KOCHA wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael ameanza kuimarisha kikosi chake kimya kimya kwaajili ya msimu ujao kwa kuwafuatilia wachezaji anaowahitaji.

Eymael ambaye yupo kwao Ubelgiji ameiambia Mwanaspoti Online kuwa anaamini timu hiyo itakuwa imara zaidi msimu ujao kama mambo yatakwenda sawa na kupata wachezaji atakaowapendekeza.
Amesema yeye ni kocha ambaye anafanya kazi kitaalamu hivyo kila kitu kinachofanyika ni kwa kuangalia timu nzima.

"Siwezi kusema wachezaji wangapi nitaachana nao lakini nitaongeza wachezaji. Nafanya 'research' kisha natuma majina kwa uongozi wa timu kuhusu wachezaji nitakaowahitaji, hivyo uongozi ndio utakaotoa maamuzi ya mwisho kwa yale mapendekezo ninayowapa," anasema Eymael.

Wachezaji wanaotajwa kuwaniwa kwenye usajili wa Yanga ni Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union, Sarpon wa Rayon Sport na Mpiana Moziz DC Motema Pembe.

Kuhusu program ambazo wanafanya wachezaji wake amesema aliwapa kabla hata hajaondoka nchini na kila baada ya wiki tatu anabadilisha program. Mazoezi ambayo wachezaji wa Yanga hufanya kwa muda huu ni pamoja na kuongeza pumzi, mazoezi ya viungo na mazoezi ya misuli ambayo pia hutolewa na kocha wa viungo, Riedoh Berdien.

"Hata hivyo napokea video za wachezaji wasiozidi tisa ambao wanaonyesha namna ya kile wanachokifanya kwa muda huu baada ya kupewa program."

Yanga yenye alama 51 katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, msimu uliopita ilimaliza nafasi ya pili kwa alama 86 na msimu wa mwaka juzi ilimaliza nafasi ya tatu kwa alama 52.


@Yangafulldozz.
 
KILA NITAKAPOKUTANA NA SIMBA NI KICHAPO TU .

Eymael kwa sasa yupo nchini kwao Ubelgiji ambako wananchi wote wanatakiwa kukaa ndani kipindi hiki ambacho kuna mapambano ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Kocha wa Yanga SC, Luc Eymael Dar es Salaam. Kocha wa Yanga SC, Luc Eymael ametoa ahadi tamu kwa mashabiki wa Yanga kuwa atahakikisha inaifunga Simba katika muda wote atakaoinoa timu hiyo. Eymael ametoa kauli hiyo miezi miwili tangu Yanga ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba, ambao ulikuwa wa kwanza kwake kuzikutanisha timu hizo tangu alipokuja nchini uliochezwa Machi 8, 2020.

"Niliumiza kichwa katika mbinu kuona vile ambavyo naweza kuwapa furaha mashabiki wa Yanga pamoja na kuwa tulikuwa na siku chache za maandalizi wachezaji wangu waliyashika tuliyoyafanyia kazi kwa muda mfupi. "Unajua huwa ni ngumu kupata matokeo ya ushindi katika kila mchezo wa watani wa jadi lakini ningependa kuacha rekodi ya kuwa kocha ambaye aliifundisha Yanga ambayo haikuwahi kupoteza dhidi ya Simba," alisema.

Mbali na ahadi hiyo, Eymael pia amedai kuwa na kiu ya kutaka kuifanya klabu hiyo ya wananchi kuwa tishio Afrika lakini kufika huko ni lazima waanze kwa kutawala soka la ndani kwa kutwaa mataji.

Yanga wenye pointi 51 wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku wakizidiwa kwa pointi tatu na Azam ambapo wapo nafasi pili, Simba ndio vinara wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 71.

Kocha huyo wa zamani wa Polokwane City na Black Leopards za Afrika Kusini, alisema kwa namna ambavyo anakitazama kikosi chake msimu ujao utakuwa tofauti zaidi na msimu huu kutokana na mipango iliyopo. "Lazima tuboreshe kikosi kwa sababu ni kawaida kila baada ya msimu kumalizika nikiwa kama kocha kutoa ripoti, kuna baadhi ya mambo yameanza kufanyiwa kazi. Siwezi kuyaweka tusubiri tuone," alisema kocha huyo mwenye miaka 60.

Lakini pia Eymael alizungumzia miongoni mwa matukio ambayo yapo katika kumbukumbu tangu ajiunge na Yanga ni pamoja na namna ambavyo aliongoza timu hiyo kupata matokeo ya ushindi dhidi ya Simba, Yanga ikiwa chini ya Mbelgiji huyo, aliifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa watani wa jadi ambao ulihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

@Yangafulldozz.
 
TFF YASUBIRI TAMKO LA SERIKALI KUENDELEA KWA LIGI :

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limesema linasubiri tamko la Serikali kuhusu hali ya mgonjwa wa Virusi vya Corona hapa nchini ili kurejesha ligi kuu ya Vodacom na shughuli zote za Michezo.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Wilfred Kidao alipokuwa akizungumza na vyombo vya Habari kwa njia ya mtandao. Kidao amesema wao kama Shirikisho wanaendelea na vikao vyao vya ndani ili kujua ni jinsi gani ligi hiyo itarejea lakini itategemea na tamko la Serikali kuhusu ugonjwa wa Corona.

“Tunasubiri tamko la Serikali ili kurejesha ligi ingawa sisi kama TFF tunafanya vikao vyetu kujadili suala hili.

Tunamshukuru Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kufikiria kuirudisha ligi kwahiyo tunawataka wadau wetu wasubiri mpaka muda utakapo fika,” alisema Kidao.

@Yangafulldozzz
 
MORRISON AHAIDI RAHA YANGA SC:-

Bernard Morrison ni moja ya wachezaji ambao walisajiliwa katika dirisha dogo kwenye kikosi cha Yanga akiwa mchezaji huru tangu alipoachana na DC Motema Pembe ya DR Congo.

Mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amewataka mashabiki wa timu hiyo kukaa mkao wa kula kwani anajipanga kuwa na kiwango bora zaidi ya kile alichokionyesha katika mechi chache alizoichezea ambacho hajaridhika nacho. Akizungumza na Mwanaspoti Morrison alisema kuwa mechi aliyofunga bao pekee la ushindi dhidi ya Simba ndio alikuwa anaanza kuwa katika makali yake.

"unajua hata wakati nacheza mechi na Simba nilikuwa na maumivu ya mguu ndio maana baada ya kuifanya kazi ambayo niliagizwa na kocha wangu nilitolewa.

Kwa muda mchache niliokuwa hapa Tanzania nadhani bado sijacheza kwa kiwango ambacho natamani kukiona kwanza nilikuwa sijazoea mambo mengi lakini kwa sasa naona vitu vingi vipo sawa," alisema.

"Nikirudi katika ligi nitakuwa nimeimarika zaidi kwa maana hiyo nadhani kuna vitu vingi ambavyo nitavifanya uwanjani katika kila mechi ili kuona timu yangu inaweza kupata ushindi.

Nadhani nikifanya mambo mengi mazuri kwa timu yangu nitaweza kuisaidia kupata matokeo ambayo inahitaji lakini kufikia malengo yake wakati huo huo nitakuwa najitangaza mwenyewe," alisema Morrison.
 
LUC EYMAEL KUAMUA HATMA YA KASEKE:-

Kiungo mshambuliaji wa Young Africans Deus Kaseke ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inafika tamati msimu huu utakapomalizika Nyota huyo ambaye alisajiliwa na Young Africans kwa mara ya kwanza mwaka 2015, anawasikilizia mabosi wake ofa ya mkataba mpya.

Hata hivyo amesema pamoja na kuwasikilizia viongozi wa klabu hiyo, Kaseke yuko tayari kusikiliza ofa kutoka timu nyingine ambazo zinahitaji huduma yake.

“Bado nina mkataba na Yanga mpaka mwishoni mwa msimu, nasubiri ofa ya mkataba mpya. Kipaumbele nimeipa Yanga lakini hata ikitokea timu nyingine tukafikia makubaliano, sina pingamizi,” amesema

Mpaka wakati ligi inasimama, Kaseke hakuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Luc Eymael. Inafahamika Young Africans ipo kwenye mkakati kabambe wa kukisuka upya kikosi chake ambapo nafasi ya washambuliaji wa pembeni ikipewa kipaumbele Eymael ndiye atakayeamua kama nyota huyo apewe mkataba au la.

@Yangafulldozz.
 
Back
Top Bottom