Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

MABOSI:- MKWASA KUKABIDHIWA TIMU

Mabosi wa Klabu ya Yanga wamechungulia mbali na kuona ligi inaweza kurejea hivi karibuni lakini bila ya kuwa na makocha wao wawili, Kocha Mkuu Luc Eymael na yule wa viungo, Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini. Sasa kwa ajili ya kuweka mipango sawa bila ya kutetereka, mabosi hao wa Yanga wameamua kumuachia mikoba kocha msaidizi, Charles Mkwasa kuwa ndiye awe msimamizi mkuu wa timu hiyo wakati ambao Eymael atachelewa kurejea nchini endapo tangazo la ligi kuendelea litakapotangazwa. ๏ฟผ

Mabosi hao wamefikia muafaka huo baada ya kuona Eymael ni ngumu kurejea Bongo kwa sasa kutokana na kwao, Ubelgiji kufunga uwanja wa ndege kutokana na janga la Corona ambapo pia akirejea atatakiwa kubakia karantini kwa siku 14.

Habari ambazo Championi limezipata ni kwamba timu hiyo itakuwa chini ya Mkwasa ambaye wamejiridhisha kuwa kutokana na uzoefu wake, ataweza kuibeba timu hiyo kwenye mechi zilizobaki.

Kabla ya kuja Eymael, Mkwasa aliachiwa timu hiyo baada ya kocha mkuu Mwinyi Zahera kuvunjiwa mkataba wake. โ€œInaonekana labda kocha Eymael anaweza kuchelewa kurejea Bongo kama ligi itaanza hivi karibuni, lakini hilo tayari limeshafanyiwa utaratibu wa kuweza kulikamilisha na kuwa vizuri.

โ€œKitakachofanyika ni kuwa Mkwasa ndiye atapewa timu aiendeshe kwa wakati huo kwa sababu wengi wamemuamini kutokana na kile alichokifanya wakati alipopewa timu baada ya Zahera kuvunjiwa mkataba,โ€ kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wake, Ofisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, amesema mipango hiyo wanaendelea nayo kuhakikisha hawapati tatizo lolote hata kama kocha huyo atachelewa kurudi na ligi ikianza.
Hapo program sijui zitatumia za mwalimu Mkuu au mkwasa nae atakuja na zake halafu kocha Mkuu akija ataendelea na zake!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ni Barakoa Fc tu kwa sasa. Haiwezekani ugonjwa unaisha halafu ndio wanasambaza vitambaa. ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

Mana baada ya kuuza sanitizer weee mwishowe ndio kaona agawie watu vitambaa ambapo wengi anaowapa hata sidhani kama hizo pasi wanazo sa si hatari hiyo Mkuu. ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 
Back
Top Bottom