Mashabiki tunajifanya tunajua kuliko kocha na kukalili wachezaji lakini ukiuliza madhaifa ya kikosi cha leo kilikuwa ni maeneo yapi zaidi ya matatizo ya kila siku? Nafasi zinatengenezwa lakini uwezo wa kutumia nafasi hakuna. Na ndio tatizo la Yanga hii tokea mechi ya kwanza ya ligi ni shida hilo hilo la umaliziaji wa mpira. Yanga hamna mfunia nyavu wa maana, utulivu hawana mafowadi. Laiti kama zile nafasi zilizopatikana zingetendewa kazi, hakuna mtu angetoa lawama kwa kocha. ila yote kwa yote pamoja ni kwamba wachezaji wengi walikuwa ni wa kikosi B lakini wamecheza vizuri sana. Kocha mzuri sio kujua mbinu, na ufundi tu bali na pamoja na kuwatengeneza mwachezaji. Makame, Adeyuni,Boxer,makapu,Nchimbi n.k tuliona kama hawastaili hata kuvaa jezi ya Yanga lakini sasa unaona wanaelekezwa wanabadilika. Credit kwa kocha