Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

CAFCĹ Preliminary Draw.

YANGA vs KISUNUNU UNITED

Yanga itaanzia ugenini November 27- 29 huko Libya ,Na mchezo wa marudiano December 4 - 6 jioni Da r.

Kila la kheri Wananchi.
 
Nimetoka na masikitiko sana,hii game ilikuwa yetu kabisa,mbinu za kuanza kujilinda mapema ilikuwa mistake kubwa sana,ila ndiyo matokeo cos sare ni advantage kwetu
Tumalizie kwa kusema ilikuwa bahati yao.

Na hapa ndo tunarudia kale kamsemo ka Nugaz kwamba "Bila jannja jannjja Yanga hafungwi na Simba"
 
Mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari amesema kuzingatia mbinu walizopewa na kocha wao Cedric Kaze ni chanzo cha kuwanyima nafasi ya kung'ara nyota wa Simba Clatous Chama na Luis Miquissone kwenye mchezo wa watani ulioisha kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam jumamosi.

Katika mchezo huo Yanga walicheza soka bora kipindi cha kwanza kwa kuwazuia nyota wa Simba waliozoeleka kuamua matokeo kwenye mechi nyingi zilizopita za ligi hiyo kushindwa kufurukuta.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa mechi hiyo, Shomari alisema pamoja na kuzingatia mbinu hizo, lakini pia safu yao ya ulinzi ilikuwa makini kuziba nafasi ambazo wapinzani wao wangetumia kuwadhuru

"Mechi ilikuwa ngumu lakini upande wetu tumecheza kwa nidhamu kwa kuzingatia mbinu tulizopewa na kocha na tulifanikiwa kumzuia Chama na Luis kufungua ngome yetu"

Shomari hiyo ni mechi yake ya kwanza ya watani tangu amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mtibwa Sugar lakini ameshukuru Mungu licha ya ugeni huo alionesha kiwango bora
 
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema baada ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kwa takribani siku 22, ameanza kuuona mwanga wa timu anayoitaka.

Mtaalam huyo wa soka raia wa Burundi amesema wana nafasi ya kuendelea kujiimarisha kama timu na hata mchezaji mmoja mmoja.

Kaze amesema matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba hayakuwa mabaya kwa upande wao jambo walihitaji zaidi kuondoka na alama zote tatu.

Aidha Kaze ameeleza 'kukoshwa' na sapoti ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa kuiunga mkono timu yao.

"Tumepambana mpaka mwisho lakini matokeo sio tuliyoyatarajia. Baada ya kukaa na timu kwa siku 22 naanza kuona tunaimarika lakini tungali na nafasi ya kujiimarisha zaidi kwa mchezaji mmoja mmoja na timu pia"

"Asante sana Wananchi sapoti yenu jana ilikuwa muhimu sana. Tunarejea kazini kujiandaa na mchezo unaofuata Nov 22 dhidi ya Namungo tuhakikishe tunafanya vizuri," alisema Kaze

Yanga haijapoteza mchezo wowote tangu kuanza kwa msimu huu, imeshinda michezo saba na kutoka sare michezo mitatu.

Inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 24.
 
Hahahahaa. Mtani umesahau kabiisaa kwamba nyie last season game kibao zilikuwa za kulazimisha matokea na hatukulalamika namna hii.

Nionavyo tu saa hii mjipange namna mtatufikia na sio kulalamika.
Mbona mlikua mnalalamika sana mpaka mkatutungia na jina kabisa eti "Miamala FC"? Tuseme na nyie mnatembeza miamala msimu huu?
 
Tumalizie kwa kusema ilikuwa bahati yao.

Na hapa ndo tunarudia kale kamsemo ka Nugaz kwamba "Bila jannja jannjja Yanga hafungwi na Simba"
Umemsikia Injinia Hersi jana? Kasema wao kama wadhamini wanataka timu ishinde. Kwa hiyo watafanya "juu chini" wahakikishe wanaondoka na ushindi katika kila mechi.

Sasa pigia mstari hiyo "juu chini". Maana yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha miamala inatembea ili washinde
 
Umemsikia Injinia Hersi jana? Kasema wao kama wadhamini wanataka timu ishinde. Kwa hiyo watafanya "juu chini" wahakikishe wanaondoka na ushindi katika kila mechi.

Sasa pigia mstari hiyo "juu chini". Maana yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha miamala inatembea ili washinde
Aaahhh!! Hizi kauli hata na sisi tulikuwepo nazo mwaka jana hivyo semeni sisi waleee tuko points nne mbele yenu.
 
Jifarijini tu.

Mkitahamaki hamuwezi kutufikia tena.
Wakati ndio utaamua Shadeeya. Muda si mrefu wanaocheka watanuna. Ninavyowajua Wananchi yale mahaba kwa Kaze yatapotea na yatafuatia matusi na kashfa🤣🤣🤣🤣

#Churafcsiowavumilivukwamakocha
 
Back
Top Bottom