Kuelekea CAF CHAMPION LEAGUE 2022/2023 ili tufanikiwe kufika mbali tunapaswa kusajili mbadala wa hizi namba na kufanga maboresho makubwa nafasi kadhaa.
1. BEKI WA KUSHOTO
Timu yetu haina beki wa uhakika wa kushoto hasa wa kushindana kwenye mashindano ya kimataifa. Hana apatikane mtu mrefu na mwenye mwili mkubwa kiasi atusaidie kimataifa.
2. WINGA WA KUSHOTO NA KULIA
MOLOKO, NTIBAZONKIZA, USHINDI, NKANE watuache kwanza, FARIDI hajiamini na ni mchezaji asiye na muendelezo sahihi. Akijirekebisha atatusaidia na hasa awe anatokea banchi.
NTIBA, anakaa sana na mipia bila sababu.
Tupata mbavu mbili kama MSUVA akae kulia, na KISINDA kushoto.
3. NAMBA 10.
Pamoja na kumsifia sana Feisal lakn lazima tuseme ukweli anahitaji stamina kubwa maana ni legelege mno, ni aamue aingie gym au awe anatokea sub. Tupate giant kama KAMUSOKO mtu ambaye akijichimbia chini huchukui mpira na mwenye uwezo na kupiga mabomba hasa.
4. NAMBA 5.
Yes MWAMNYETO atafutiwe changamoto hasa kutoka mataifa ya Magharibi au kusini mwa Afrika.