Yoweri Museveni Rais wa Uganda amepiga marufuku Mitumba. Amesema ni Nguo zilizoachwa na Wafu wa Ulaya

Ni idea nzuri.
Lakini kabla hatajaiga walichofanya ni busara kama tutahakikisha tunazalisha nguo za kutosha na zinazo kidhi mahitaji ya makundi yote ya watanzania.

Huo uzalishaji kwa sasa haupo.

Inabidi tuwapatie wauza mitumba alternative endapo tutakataza mitumba.
 
Uanda na Rwanda wanyonge wanatembea uchi ?
Rwanda wanajitambua. Hapa hata hizo za China na Uturuki zisizo mitumba ni fake tupu na ni zile reject za Viwandani. Hii nchi ina mambo ya hovyo sanaa. Na siku wakithubutu kupiga marufuku mitumba, watanzania wengi watavaa midabwada.
 
Mmeanza kuona nadrip saivi tudemu na mimi napatamo
Mnataka m ban brand zangu
 
Ni idea nzuri.
Lakini kabla hatajaiga walichofanya ni busara kama tutahakikisha tunazalisha nguo za kutosha na zinazo kidhi mahitaji ya makundi yote ya watanzania.

Huo uzalishaji kwa sasa haupo.

Inabidi tuwapatie wauza mitumba alternative endapo tutakataza mitumba.
Haiwezekani kukuza uzalishaji wakati kuna cheap import za mitumba. Lazima upige kwanza marufuku mitumba ndiyo uzalishaji wa ndani utakua.
 
Ni kweli.
Lakini lazima angalau kuwe na sera au mpango kazi wa kufufua viwanda vya nguo ili kuweza kucover vaccancy itakayo kuwepo.

Hivi sasa hivyo vyote havipo. Tuanze na hivyo kwanza.
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaonya Wananchi Nchini humo juu ya kununua na kutumia nguo za mitumba akisema hizo ni nguo zilizokusanywa baada ya watumiaji wake (wazungu) kufariki na kubainisha kuwa lengo ni Watu wa Uganda wanunue nguo mpya kutoka kwenye viwanda vinavyozalisha mavazi vya Uganda.

“Ni za watu waliokufa. Mzungu akifa, nguo zake hutupwa. Sijui ni mtu gani anakusanya nguo zake na kuzipeleka Afrika. Tunapaswa kuacha kuvaa,” Museveni alisema.

"Tuna watu hapa ambao wanazalisha nguo mpya lakini hawawezi kupenyeza sokoni kwa sababu mitumba tayari imejaa."

Museveni alitoa kauli hiyo wakati akizindua viwanda 15 katika Hifadhi ya Viwanda ya Sino-Mbale wilayani Mbale jana. Pia alivunja ardhi kwa viwanda vingine 9 katika bustani hiyo hiyo.

Rais Museveni ameagiza pia kuanzia September 01,2023 cable na metres za umeme zisingizwe kutoka nje ya Nchi ili Watu wanunue kwenye viwanda vya Uganda ili kuijenga Uganda, (Buy Uganda, Build Uganda - BUBU).

#KitengeUpdates
 
Ni kweli.
Lakini lazima angalau kuwe na sera au mpango kazi wa kufufa viwanda vya nguo ili kuweza kucover vaccancy itakayo kuwepo.

Hivi sasa hivyo vyote havipo. Tuanze na hivyo kwanza.
Kweli. Sera ni muhimu. Kama kurahisisha uanzishwaji wa viwanda kwa kutoa nafuu ya kodi, meeneo nk.
 
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaonya Wananchi Nchini humo juu ya kununua na kutumia nguo za mitumba akisema hizo ni nguo zilizokusanywa baada ya watumiaji wake (wazungu) kufariki na kubainisha kuwa lengo ni Watu wa Uganda wanunue nguo mpya kutoka kwenye viwanda vinavyozalisha mavazi vya Uganda.

“Ni za watu waliokufa. Mzungu akifa, nguo zake hutupwa. Sijui ni mtu gani anakusanya nguo zake na kuzipeleka Afrika. Tunapaswa kuacha kuvaa,” Museveni alisema.

"Tuna watu hapa ambao wanazalisha nguo mpya lakini hawawezi kupenyeza sokoni kwa sababu mitumba tayari imejaa."

Museveni alitoa kauli hiyo wakati akizindua viwanda 15 katika Hifadhi ya Viwanda ya Sino-Mbale wilayani Mbale jana. Pia alivunja ardhi kwa viwanda vingine 9 katika bustani hiyo hiyo.

Rais Museveni ameagiza pia kuanzia September 01,2023 cable na metres za umeme zisingizwe kutoka nje ya Nchi ili Watu wanunue kwenye viwanda vya Uganda ili kuijenga Uganda, (Buy Uganda, Build Uganda - BUBU).

#KitengeUpdates
Pesa za uchaguzi tu anapewa na wazungu😆😆😆
 
Duh! Mama asije kuiga hii. Vijana wengi hawana ajira wamejiajiri katika hiyo sector ya kuagiza mabalo ya mitumba na kuuza.

Wengine ndio nguzo za familia zao. Unless kuwe na alternative means za kuwafanya waishi vizuri tofauti na hiyo kazi.
 
Hii safi sana.

Nimelikemea hili na nimeliponda kwa miaka mingi sana.

Waafrika wote tupige marufuku mitumba yote. Ya nguo, ya magari, ya nafriji na kila kitu.

Ndipo tutakapoweza kufanya vyetu wenyewe.

Hapa namuunga mkono Museveni 100%.
Tuna viwanda vya nguo tofauti na makaniki, mashuka makanga na mavitenge?
 
Kama kawaida yetu tunaongelea vitu kwa upeo mfupi umeona nilochosema..., Unless Otherwise Viwanda vya ndani ambavyo havipo na quality yake leaves a lot to be desired itapelekea watu kuvaa midabwada (hii sio theory tu it happened hapo nyuma) kwahio sitetei mitumba ila mimi ni muumini wa bottom up approach anza kwanza vutia watu vitu vyako; quality na taste (kuna kipindi watu walipenda kuvaa mavitenge (though they were not cheap) watu wanavaa mitumba sio sababu tu imetoka nje bali quality na uniqueness..., Leo hii dada anauza nyanya kipato chake cha kuunga unga ila akienda mnadani anatoka na kupendeza hata Beyonce haoni ndani..., Kutokana na Economy of Scale ni ngumu kwa nguo ya ndani kushindana na price ya hio mitumba....(we are not there yet) Unaweza ukasema kwanini wanunue cheap na wasinunue za gharama (swali linakuja watu wako wana- sufficient income) ?

Issue sio kuzoea tu issue / fashion ni taste na uniqueness hata huku kuna kipindi watu walikuwa wanavaa nguo saresare; au kule China kuna kipindi cha kufunga mikanda walikuwa wanavaa manguo yao fulani ya kufanana na viatu vya kamba za katani - lakini leo giving them a choice kila mtu anafanya anachofanya (To each their own)

Kwani hata bila kuboreshwa ni baya na unaongelea vazi material au kufunga lubega (hio sio mmasai tu ni kabila nyingi tu) ila nakuuliza hilo vazi la mmasai wakiboresha unadhani litacost kiasi gani kwenye market value kwa viwanda vyetu hivi vinavyotegemea umeme wa Makamba ?

Kumbe hujui midabwada ni nini midabwada ni viraka watu wanakosa pesa za kununua nguo hence wanashona na kuweka viraka..., mafundi viatu watarudi kushona viatu sababu ukinunua kimoja unakibembeleza kisiishe au wote kuvaa Bata na Bora / Sare Sare usiongelee Nike na Adidas au Puma hao wakija huku hakuna pesa (pesa zako za madafu kwao ni hasara)

Unajua hata kabla ya Rambo na vifugashio tulikuwa tunaishi na mifuko ya karatasi (ila ukweli ndio huo hizo plastics ni cheaper) kwahio wakiacha rambo sio kwamba watu wanatumia mifuko mingine ambayo ni expensive ila inawafundisha Reuse (katika ile 3Rs)

Nimekujibu hapo juu mifuko / plastics ni cheaper ndio maana imesambaa sana ila inaharibu mazingira balaa...., ndio maana hata ulaya wanataka kufanya hivyo Ni manufaa kwa mazingira ila ni kipigo kwa mifuko ya watu / Pesa

Usingoje mitumba ipigwe marufuku kuza sekta ya nguo za ndani zikiwa nzuri watu watanunua ni utamaduni..., Uganda watu wanapenda kuvaa nguo za kushona huku nguo za kushona sio kivile (pia quality ni mbovu unavaa nguo mara moja inapauka ikipigwa upepo) hio sio huku tu hata original za China unadhani kwanini kuna watu wanachukua kiatu dukani wanasugua soli chini ionekane ni mtumba, ili wakuuzie kama mtumba ?

Mgeni aje awekeze ili alipwe nini wakati watu wamepigika ? Hivi ushajiuliza kwanini wawekezaji wengi wa vitu ambavyo ni fashion hawaji kuwekeza huku ? Jibu watu hawana buying power.....

Huo ubunifu unasubiri nini . Si wabuni waende kuwauzia diaspora waliopo ulaya ?

Anza ila kuanza sio kwa kupiga siasa anza kwa kuzalisha quality kutoka viwanda vya ndani promote nguo zako ili kina mama Aisha na Mwajuma na Neema wapende kuvaa kitu kutoka Mwatex na sio Mombasa hio ndio njia sahihi sio kulazimisha watu

Unadhani hio pamba yako ukishamaliza kuitengeneza na kuwa-refined kwa umeme huu wa Makamba na ukatoa nguo itakuwa bei gani ? Ushajiuliza kwanini kuna vitu vinatoka ulaya vinakuwa na bei ndogo kuliko vitu vya ndani ? Jibu ni Economy of Scale - Pile it High.., Sell it Cheap.......; Na kama soko lako ni la kuokoteleza volume unazotoa hazitafanya bei iwe chini - Anza kidogo waambie watoto wa shule, wanajeshi n.k. wavae nguo made in Tanzania (ila utashangaa mzazi itabidi atoe mara tatu ya bei aliyokuwa anatoa jana)
Watetezi wa magharibi hamjawahi kosa hoja za kuuendeleza na umagharibi.
Fashion ni propaganda za kimagharibi hakuna la zaidi.
Kadeti ya mwaka 90 wala haina tofauti sana na ya mwaka 2023 ni uongouongo wa kibiashara tu.
Kitambaa cha mchelemchele kuna yofauti gani na hivi vitambaa vya mafuta vya siku hizi ?
Jambo ka pili kupiga marufuku mitumba haina maana kupiga marufiku nguo mpya kutoka nje. Wewe unaemependa fasheni utanunua fasheni mpya au kuagiza duka la mtandaoni.
Ndugu yangu kwenye mitumba kuna fasheni gani? Mitumba si ni fashion iliopitwa na wakati !
Nyerere aliopozuia mitumba ni zama tofauti na leo.
Leo kuna mashine za kiviwabda huitaji mabilioni ya fedha kuvijenga na ndio maana ASIA wameweza kujitosheleza nguo na kuuza nguo dunia nzima.
Kama Malaysia,Thailand , Vietnam nk wameweza sisi tunashindwa nini ?
Unafikiri China iliwainua watu wake ghafla na kwa mpigo kwenda kipato cha kati na juu ?
Tanzania tunatakiwa tuende kwenye vitendo badala ya maneno .
Nakuhakikishia Uganda wala hawata tembea uchi kisa kuzuia mitumba na tutaenda kujifunza kwao miaja si mingi.
China inazalisha nguo kwa bei rahisi sana. Kwa nini tuendelee kuvaa mitumba?
Hayo malonya waliotupa wazungu ni midabwada acha kuyapamba.
Tunavaa mitumba muda mwingine ni kwa sababu ya mazoea na hatutaki kufikiri wenyewe, wazungu wafikiri kwa niaba yetu, mpaka lini.
Wewe na mimi tuchukue hatua ya kubadirika kwanza kifikra, kufanya linaloshindikana liwezekane.
Ifike mwisho sasa kulaumu tu wabna siasa , mbona kina mengi waliweza sisi tunashindwa nini? Kaxi kulaumu laumu tu.
Tulaumu huku tukichukua hatua ktk kika jambo.
Tumekuwa watu wa kulaumu huku tunajua tunaowalaumu hawatabadiri chochote.
 
Tuna viwanda vya nguo tofauti na makaniki, mashuka makanga na mavitenge?
Mkuu tusidanganyane. Kiwanda cha vitambaa sio cha nguo. Wale kazi yao kuzalisha vitambaa wewe weka cha kuzishona.
Kiwanda cha nguo kinaweza agiza vitambaa dunia nzima kulingana ba ubora wa vitambaa hulazimishwi utumie vya ndani tu.
Vazi no 1 la mwafrika hasa kina mama ni vitenge na khanga. Uholanzi, ufaransa, uturuki, India na sasa China ndio wanaofaidika wa soko hapa Afrika.
Humu Bujibuji ameweka mada ya VITENGE ni vizuri tusome tuelewe hizi biashara zinaendeshwaje.
Miaka ya 90 na kurudi nyuma kilikuwepo kiwanda cha BORA walitoa viatu vya kila aina kuanzia Moka, raba, buti, kandambili, yebo za masai nk.
Kwa hio ni suala la maaamuzi tu.
Siku hizi teknolojia ipo sokoni ni wewe kununua mitambo uanze uzalishaji wa nguo za fasheni.
Labda useme sisi timezoea uchuuzi.
 
Watetezi wa magharibi hamjawahi kosa hoja za kuuendeleza na umagharibi.
Fashion ni propaganda za kimagharibi hakuna la zaidi.
Kadeti ya mwaka 90 wala haina tofauti sana na ya mwaka 2023 ni uongouongo wa kibiashara tu.
Kitambaa cha mchelemchele kuna yofauti gani na hivi vitambaa vya mafuta vya siku hizi ?
Again you miss the Point Big Time rudia kusoma niliyoyaeleza kwanza hapo juu, wakati wengine wanavaa mchelemchele watoto wa kitaa mafukara walikuwa wanavaa nini ? Jiulize kwanza hilo swali..., Unadhani isingekuwa mitumba watoto wangapi wangekuwa wanatembea vifua wazi na peku ?!!

Unaangalia jambo kwa perspective ambayo ni cultural mimi naongelea nyingine ambayo ni affordability..., hence naongelea uhalisia..., kama viwanda vyetu haviwezi ku-compete na viwanda vya nje mwisho wa siku ni kuvalishana second best..., unaongelea tuagize nguo za nje kwa top dollar ? zipi original za China ambazo hazina tofauti quality-wise na original za huku ? Ili iweje ?
Jambo ka pili kupiga marufuku mitumba haina maana kupiga marufiku nguo mpya kutoka nje. Wewe unaemependa fasheni utanunua fasheni mpya au kuagiza duka la mtandaoni.
Point yangu ya hapo juu rudia tena quality, durability na value for money..., Mitumba ni cheap kwa baadhi ya watu hadi vitoto ambavyo vingekuwa vinatembea kifua wazi vinavaa nguo..., pia ni quality kuliko so called original ambazo watu wataleta huku kulinga na buying power yetu..., tatu kuna kitu kinaitwa ex-catalogue mitumba sio yote imeshavaliwa mingine ni ex - catalogue haikuuzwa kipindi cha summer, kwahio summer imekwisha imeingia msimu mwingine basi hazina soko tena... Watu wenye buying power wana luxury ya kwenda na wakati kwahio wewe nguo za msimu zikiisha kuziweka store ni gharama wala huwezi kuuza nguo ya mwaka jana mwaka huu (hio ishatoka kwenye fashion)
Ndugu yangu kwenye mitumba kuna fasheni gani? Mitumba si ni fashion iliopitwa na wakati !
Fashion iliyopitwa na wakati wapi ? Nini maana ya Fashion ?
Generally, fashion is a popular style or practice, especially in clothing, footwear, accessories, makeup, body, or furniture. It comes from a Latin ward “Facere ...

Sasa kama watu wana-desturi ya kupenda hayo madela au manguo ambayo yanapatikana kwenye mitumba at that moment in time kama sio fashion ni nini ?
Nyerere aliopozuia mitumba ni zama tofauti na leo.
Leo kuna mashine za kiviwabda huitaji mabilioni ya fedha kuvijenga na ndio maana ASIA wameweza kujitosheleza nguo na kuuza nguo dunia nzima.
Again unaangalia vitu kwa mafungu..., hicho kiwanda unakachoweka ili kitengeneze nguo price yake per unit itakuwa ngapi ? Mtu ataacha kununua chumvi ili aende anunue shati ambalo akifua rangi inavuja ? Na usilete habari kwamba wakitengeneza zitakuwa cheaper.., hatuna economy of scale na tunaowatengenezea hawana buying power
Kama Malaysia,Thailand , Vietnam nk wameweza sisi tunashindwa nini ?
Unafikiri China iliwainua watu wake ghafla na kwa mpigo kwenda kipato cha kati na juu ?
Tanzania tunatakiwa tuende kwenye vitendo badala ya maneno .
Kwahio tumeshindwa kuendelea sababu ya mitumba ?
Nakuhakikishia Uganda wala hawata tembea uchi kisa kuzuia mitumba na tutaenda kujifunza kwao miaja si mingi.
China inazalisha nguo kwa bei rahisi sana. Kwa nini tuendelee kuvaa mitumba?
Again naona najirudia kama rekodi mbovu Jeans ya mchina ni bei gani quality gani kinauzwa vipi mtaani na kinakaa muda gani..., Na fukara anaweza aka-afford hio, Sasa hivi kuna viatu vya plastics sijui zinatokea China bei ni ndogo kila mtu anavaa mtaani; Umeshajiuliza Safari boot ile leather inayotengenezwa Tanzania Bei yake ni kiasi gani ?
Hayo malonya waliotupa wazungu ni midabwada acha kuyapamba.
Kwahio Jeans sijui inayotengenezwa wapi hapa Tanzania ni bora kuliko Levis au Lee ambayo huko ilipotoka ni ex-catallogue au unadhani ukitaka ununue ikiwa mpya mtu wa pale Tanga barabara ya nane ataweza kununua ? Au umeamua tu kuunganisha sentensi ili mradi zitoe paragraphs ?
Tunavaa mitumba muda mwingine ni kwa sababu ya mazoea na hatutaki kufikiri wenyewe, wazungu wafikiri kwa niaba yetu, mpaka lini.
Wewe na mimi tuchukue hatua ya kubadirika kwanza kifikra, kufanya linaloshindikana liwezekane.
Ifike mwisho sasa kulaumu tu wabna siasa , mbona kina mengi waliweza sisi tunashindwa nini? Kaxi kulaumu laumu tu.
Tulaumu huku tukichukua hatua ktk kika jambo.
Tumekuwa watu wa kulaumu huku tunajua tunaowalaumu hawatabadiri chochote.
Kwahio Mwatex, SunguraTex n.k. wanatoa mizigo ambayo ni cheaper, high quality na inayodumu basi ti watu wanaamua kuvaa hizo nguo nyingine ?

Ulishawahi kwenda kushona Koti la Suti au Kununua Dukani Jipya ? Bei zake ni vipi in comparison ? Na kama wewe uliweza kununua unadhani kila mtu anaweza kutokana na vipato vyao ?
 
Tutavaa nini? Hivyo viwanda vya kukuzwa viko wapi?

Si mliua Urafiki, Kilitex, Mwatex n.k mkawaachia Wahindi waje na Sunflag na A-Z na watumwa huko viwandani wa kuchanganya rangi na kuchochea moto ni watoto wenu walipwe elfu 60 kwa mwezi

Watu weusi wana Upumbavu sana
Inasikitisha sana...
 
Again you miss the Point Big Time rudia kusoma niliyoyaeleza kwanza hapo juu, wakati wengine wanavaa mchelemchele watoto wa kitaa mafukara walikuwa wanavaa nini ? Jiulize kwanza hilo swali..., Unadhani isingekuwa mitumba watoto wangapi wangekuwa wanatembea vifua wazi na peku ?!!

Unaangalia jambo kwa perspective ambayo ni cultural mimi naongelea nyingine ambayo ni affordability..., hence naongelea uhalisia..., kama viwanda vyetu haviwezi ku-compete na viwanda vya nje mwisho wa siku ni kuvalishana second best..., unaongelea tuagize nguo za nje kwa top dollar ? zipi original za China ambazo hazina tofauti quality-wise na original za huku ? Ili iweje ?

Point yangu ya hapo juu rudia tena quality, durability na value for money..., Mitumba ni cheap kwa baadhi ya watu hadi vitoto ambavyo vingekuwa vinatembea kifua wazi vinavaa nguo..., pia ni quality kuliko so called original ambazo watu wataleta huku kulinga na buying power yetu..., tatu kuna kitu kinaitwa ex-catalogue mitumba sio yote imeshavaliwa mingine ni ex - catalogue haikuuzwa kipindi cha summer, kwahio summer imekwisha imeingia msimu mwingine basi hazina soko tena... Watu wenye buying power wana luxury ya kwenda na wakati kwahio wewe nguo za msimu zikiisha kuziweka store ni gharama wala huwezi kuuza nguo ya mwaka jana mwaka huu (hio ishatoka kwenye fashion)

Fashion iliyopitwa na wakati wapi ? Nini maana ya Fashion ?
Generally, fashion is a popular style or practice, especially in clothing, footwear, accessories, makeup, body, or furniture. It comes from a Latin ward “Facere ...

Sasa kama watu wana-desturi ya kupenda hayo madela au manguo ambayo yanapatikana kwenye mitumba at that moment in time kama sio fashion ni nini ?

Again unaangalia vitu kwa mafungu..., hicho kiwanda unakachoweka ili kitengeneze nguo price yake per unit itakuwa ngapi ? Mtu ataacha kununua chumvi ili aende anunue shati ambalo akifua rangi inavuja ? Na usilete habari kwamba wakitengeneza zitakuwa cheaper.., hatuna economy of scale na tunaowatengenezea hawana buying power

Kwahio tumeshindwa kuendelea sababu ya mitumba ?

Again naona najirudia kama rekodi mbovu Jeans ya mchina ni bei gani quality gani kinauzwa vipi mtaani na kinakaa muda gani..., Na fukara anaweza aka-afford hio, Sasa hivi kuna viatu vya plastics sijui zinatokea China bei ni ndogo kila mtu anavaa mtaani; Umeshajiuliza Safari boot ile leather inayotengenezwa Tanzania Bei yake ni kiasi gani ?

Kwahio Jeans sijui inayotengenezwa wapi hapa Tanzania ni bora kuliko Levis au Lee ambayo huko ilipotoka ni ex-catallogue au unadhani ukitaka ununue ikiwa mpya mtu wa pale Tanga barabara ya nane ataweza kununua ? Au umeamua tu kuunganisha sentensi ili mradi zitoe paragraphs ?

Kwahio Mwatex, SunguraTex n.k. wanatoa mizigo ambayo ni cheaper, high quality na inayodumu basi ti watu wanaamua kuvaa hizo nguo nyingine ?

Ulishawahi kwenda kushona Koti la Suti au Kununua Dukani Jipya ? Bei zake ni vipi in comparison ? Na kama wewe uliweza kununua unadhani kila mtu anaweza kutokana na vipato vyao ?
Hivi hio nguvu ya kununua wananchi wetu wataipata vipi hali bidhaa zenyewe wanazouza ni cheap.
Mtu anauza malonya kwa 200 unafikiri ataipata hio nguvu ya kiuchumi unayoisema?
Mitumba ni bidhaa mojawapo inayodunaza uchumi. Ina maana wewe mchumi hulioni hilo ?
Kwenye mitumba kuna value chain? Kama haipo huyo mtu wa kipata kidogo atapata vipi nguvu ya pesa.
Kiwanda pekee ndio kitakuza nguvu ya mlala hoi ya kununua.
Yaani wewe kama ni mchumi basi hii nchi haitaendelea, kwa sababu una promote ulala hoi badala ya kuukataa kwa vitendo!

Unaangalia uwezo wa kununua mitumba bila kuangalia mahara ya hio mitumba kwa muuza mitumba na mvaaji.
Mseven ameangalia mbali zaidi kuliko wewe unavyoangalia.
Waafrika wenzetu wanapoamua kiondokana na ukoloni mambo leo tuwasapoti na wataposhindwa tuwape ushauri.
Sikubaliani kamwe kuebdelea na wazo la mitumba kwa sababu ni jambo dhdlili na lisilofaa hata kidogo.
We jamaa unaweza mpelekea mama yako zawadi ya nguo ya mtumba ?
Mitumba ni sawa na makombo ya chakula.
Hivi mtu akikupa makombo utakula ?
Je ukila siku moja hayo makombo ndoo utafanya utegemezi wa maisha yako ktk makombo ?
Hio mitumba tuta vaa mpaka yesu anavyorudi? Je sisi ni vilema wa akili tusio weza kukuza vipato vyetu na kupata uwezo wa kununua vilivyobora?
Je tumejiweka na kujikatia hatimiliki ya mtu daraja la tatu. Unafikiri hoja zako zinamashiko na ubaweza fanya utetezi kwa watu werevu kuwa tuendelee tu kutegemea mitumba?
Bro warabu, wachina na wakolea nao siku wamejiunga na wazungu kutul4tea mitumba. Kweli tunavaa majasho ya kabila zote ?
Ifike mwisho bro.
 
Tutavaa nini? Hivyo viwanda vya kukuzwa viko wapi?

Si mliua Urafiki, Kilitex, Mwatex n.k mkawaachia Wahindi waje na Sunflag na A-Z na watumwa huko viwandani wa kuchanganya rangi na kuchochea moto ni watoto wenu walipwe elfu 60 kwa mwezi

Watu weusi wana Upumbavu sana
Ngozi nyeusi ina laana ya milele.

Uafrika ni Laana.
 
Hivi hio nguvu ya kununua wananchi wetu wataipata vipi hali bidhaa zenyewe wanazouza ni cheap.
Mtu anauza malonya kwa 200 unafikiri ataipata hio nguvu ya kiuchumi unayoisema?
Kwahio unadhani huyo ambaye asingenunua kwa 200 ingekuwepo ya elfu hamsini angenunua au angekaa uchi au kushona ile aliyoachiwa na babu yake ? Tukianza kuongelea kukuza uchumi hio ni whole different ball game..., nchi hii imejaa uchuuzi na wala sio uzalishaji kwa hilo dawa yake ni kubwa zaidi wala mimi siogelei mitumba kama source of employment kwa wauzaji naangalia mitumba kama kimbilio la wengi ambao bila mitumba wangekuwa wanavaa nguo za kupauka kwa ukosefu wa quality supply....
Mitumba ni bidhaa mojawapo inayodunaza uchumi. Ina maana wewe mchumi hulioni hilo ?
Kwenye mitumba kuna value chain? Kama haipo huyo mtu wa kipata kidogo atapata vipi nguvu ya pesa.
Wewe tengeneza quality ambayo ni affordable watu watanunua.., watu wanapenda kupendeza watu wanapenda kuwa unique sio kupanda basi nyote mmevaa Sare (kuna mataifa kwao hilo wanaona sawa ila sio huku) kwahio kama kawaida ya watunga sera kutafuta tiba kwa mafungu..., Kuna kitu kinaitwa Broken windows fallacy unadhani kuvunja kwako kioo unakuza uchumi sababu mtengeneza vioo atapata kazi kumbe yule mnunuzi badala ya kununua viatu na nguo atanunua kioo kwahio anatoa pesa huku anapeleka kule..., Kwahio bila hizo nguo kuwa na quality ya kutosha na affordable prices itakuwa ni kazi bure mvaaji huyo huyo utampunguzia pesa ambazo zilikuwa zinabaki ili anunue vitabumbua baada ya kununua ngoa kwa bei rahisi...
Kiwanda pekee ndio kitakuza nguvu ya mlala hoi ya kununua.
Yaani wewe kama ni mchumi basi hii nchi haitaendelea, kwa sababu una promote ulala hoi badala ya kuukataa kwa vitendo!
Hivi unadhani kiwanda cha sasa kinahitaji watu wangapi ili kuweza kutoa materials ? (automation imefanya kazi imepungua sana) na inefficiency ya viwanda vyako itapelekea bei kuwa juu. Labda utasema watu waanze kununua vitambaa na kushonewa na mafundi cherehani majumbani (ila per unit gharama itakuwa juu sababu huwezi kushidana kwa bei na viwanda ambayo ni vinafanya mass production)...,

Kwahio unachosema wewe ni kama kuweka a cart infront of a donkey...., Cha maana ni kuboresha kwanza viwanda na kuhakikisha supply inatosha na quality inakuwa bora kuliko hata hizo ex catalogue za ulaya watu watanunua, mbona kuna kipindi khanga na mashuka ya mwatex n.k. watu walikuwa wanunua ? Kwanini waliacha unadhani ?
Unaangalia uwezo wa kununua mitumba bila kuangalia mahara ya hio mitumba kwa muuza mitumba na mvaaji.
Alternative ya mtu ambaye mtumba ndio uwezo wake wa kuvaa kutokuwepo kwa mtumba mtu huyo ni kuvaa nguo zilizopauka au viatu vilivyochanika
Mseven ameangalia mbali zaidi kuliko wewe unavyoangalia.
Moja sijajua amejiandaa vipi, pili culture ya waganda ni kupenda kushona na kuvaa original ndio maana hata kuna watu huwa wanakwenda Uganda kununua nguo na viatu na kuleta huku..., mimi huku nakupa uhalisia tatizo la hili taifa ni la wachuuzi bila uzalishaji wowote kwahio cha maana ni kuhakikisha uzalishaji unakuwa top notch baada ya hapo unaweza ukaongeza kodi kwenye baadhi ya bidhaa automatically kama quality ya ndani ni nzuri watu watanunua
Waafrika wenzetu wanapoamua kiondokana na ukoloni mambo leo tuwasapoti na wataposhindwa tuwape ushauri.
Sikubaliani kamwe kuebdelea na wazo la mitumba kwa sababu ni jambo dhdlili na lisilofaa hata kidogo.
We jamaa unaweza mpelekea mama yako zawadi ya nguo ya mtumba ?
Mitumba ni sawa na makombo ya chakula.
Hivi mtu akikupa makombo utakula ?Je ukila siku moja hayo makombo ndoo utafanya utegemezi wa maisha yako ktk makombo ?
Unajua mitumba inavyopatikana ? wewe unaongelea mtu mwenye alternative anayeweza kununua nguo mpya kwahio wewe unaona la maana zaidi ni kuondoa alternative ya mtu ambaye bila hayo so called malonya unayoyaitwa wewe angekaa uchi au kuvaa kauka nikuvae ni bora zaidi ? Unaongelea Ukoloni mamboleo hizo nguo unazovaa leo ni utamaduni wako ? Unasema mtu akinipa makombo ? alternative ni nini kukaa njaa ? Kwahio issue sio kuondoa makombo ni kuhakikisha kuna chakula fresh ili niweze kula....
Hio mitumba tuta vaa mpaka yesu anavyorudi? Je sisi ni vilema wa akili tusio weza kukuza vipato vyetu na kupata uwezo wa kununua vilivyobora?
Aliyekwambia uvae mtumba ni nani kama wewe you can afford kashone au kanunue zile nguo ambazo zikipigwa upepo zinapauka..., ila usiwapangie watu ambao bila hii alternative wangetembea vidole nje.....
Je tumejiweka na kujikatia hatimiliki ya mtu daraja la tatu. Unafikiri hoja zako zinamashiko na ubaweza fanya utetezi kwa watu werevu kuwa tuendelee tu kutegemea mitumba?
Aliyekwambia utegemee mitumba ni nani ? Mimi nakupa scenario kwamba isingekuwa mitumba kwa sasa watu wasivyo na disposable income ni kutembea peku na kuvaa viraka....
Bro warabu, wachina na wakolea nao siku wamejiunga na wazungu kutul4tea mitumba. Kweli tunavaa majasho ya kabila zote ?
Ifike mwisho bro.
Ndio pale nakuuliza tena unadhani mitumba yote ni used zimevaliwa au kuna ex catalogue....

Mimi nakupa reality ya mambo..., ila kama tunaongelea Ideology na the Best case Scenario nisome kwenye Tamthiliya yangu hapo chini..... Best case scenario ninayoiona mimi ni kujitegemea kwa vyote vinavyoweza kufanyika ndani..., ila reality is a whole different game (sababu to achieve such a fate the whole systems needs to be revamped)

Rwanda wanajitambua. Hapa hata hizo za China na Uturuki zisizo mitumba ni fake tupu na ni zile reject za Viwandani. Hii nchi ina mambo ya hovyo sanaa. Na siku wakithubutu kupiga marufuku mitumba, watanzania wengi watavaa midabwada.
bado sijakuelewa

kwa hiyo Uganda na Rwanda ambako hakuna mitumba wanatembea uchi ??????
 
Duh! Mama asije kuiga hii. Vijana wengi hawana ajira wamejiajiri katika hiyo sector ya kuagiza mabalo ya mitumba na kuuza.

Wengine ndio nguzo za familia zao. Unless kuwe na alternative means za kuwafanya waishi vizuri tofauti na hiyo kazi.
Mafundi kushona wengi watapata kazi.
 
Back
Top Bottom