Hivi wote waliowahi kuugua corona duniani kote walikuwa hawachukui tahadhari? Kwa hiyo waziri mkuu wa uingereza alikuwa hachukui tahadhari? Trump alipokuwa Rais wa Marekani alikuwa hachukui tahadhari? Makamu wake alikuwa alikuwa hachukui tahadhari? Mwacheni Mungu aitwe Mungu!!!au unadhani wale wote ambao hawajaugua corona wao ndio wataalamu Sana wa kuchukua tahadhari kuliko waziri mkuu wa Uingereza na Trump? Mwacheni Mungu aitwe Mungu! Chanjo cha maarifa ni kumjua Mungu.
Ukweli ni kwamba ulinzi namba moja ni Mungu!! Bila yeye tahadhari zote hazifui dafu!! Sisemi kwamba tahadhari watu wasichukue, lakini nasema Mungu kwanza tahadhari baadaye kama alivyotuasa Rais wetu kuwa watanzania tumtangulize Mungu.