Yuko wapi Rais Magufuli? Msiache tetesi zienee. Kama anaumwa mnasema "ANAUMWA"

Status
Not open for further replies.
Hao uliowataja wameugua kwa BAHATI MBAYA ila huyu wa kwetu alikuwa anavitafuta viluilui mwenyewe akifikiri ni sifa
 
Unatumia lugha ngumu na ya chuki.

Miimi kusema raisi aandaliwe tukio kuna ubaya gani?

Mbona walimuandalia tukio la kwenda bandarini kuokota vichwa vya treni?

Again, kama anaumwa wakae kimya. Kama haumwi wamuandalie tukio.
Wampeleke hata Soga akazindue reli ya mwendokasi.
 
Kuna jamaa yangu yuko Nairobi ananiambia Nairobi Hospital hakuingiliki kabisa. Haijulikani kuna nini ila ulinzi wa pale haijawahi tokea, wagonjwa wanashauriwa kwenda Hospitali zingine.
Kwahiyo hospitali imejaa na hivyo haiwezi kupokea wagonjwa wengine.
 
Sasa kama Mungu pekee anatosha kwann Wampeleke Nairobi? Ina maana nyungu, covidol na Yale madude ya nimr hayafanyi kazi? Kwanamna hii watz tumedharaulika kupita kiasi maana inaonyesha hospitali zetu si kitu kabisa ni muda muafaka akitoka huko ( japo sina uhakika) akae na wadau wa sekta ya afya watatue changamoto zinazoikabila sekta ya afya ili kuimarisha huduma zetu na sisi tuwe kama wakenya
 
Unakosea Sana na watoka Sana nje ya mtoa mada, mtakua lini , au mtazeeka lini japo kuwa sensitive na maoni Kama ya mtoa mda punguza ushabiki kwenye nada zenye mantiki ya kitaifa

Kwani hizi mada zimekujaga huku ngap?
 
Nukuu:
Mnataka niwalete chukula na niwaengee nyumba kwani Mimi ndiye niliyeleta tetemeko.
Mwisho wa kununukuu.

Famili za Lissu, Ben, Kanguye, mawazo,Akwilina.
Waliopoteza ndugu zao kwaajili ya tumumbu tumbua

Waliofanyakazi kwa ufanisi ktk sekta za serikali
Wakakumbwa na vyeti feki ikiwa bado siku chache kustahafu na kunyimwa hata hela
thank japo ziwasaidie kuendesha maisha.

Waliovunjiwa nyumba zao barabara ya morogoro Kule kimara wakateseka kwa mvua na jua.

SWALI
Kama ni kweli hii tetesi, makundi haya yatakosa kufurahia na kuomba mabaya yamfike zaidi?
 
Hao uliowataja wameugua kwa BAHATI MBAYA ila huyu wa kwetu alikuwa anavitafuta viluilui mwenyewe akifikiri ni sifa
Yeyote akiugua ni bahati mbaya! Ukweli ni kwamba kwa mazingira yetu, hakuna mwenye uwezo wa kuchukua tahadhari kama inavyotakiwa! Hali na mazingira haviruhusu, ndio maana tunamtanguliza Mungu!
 
Sio lazima. Mwanzo alizushiwa kifo na hakuwahi kutokeza mtu yeyote kukanusha. Kwahiyo wacha wajinga waendelee kutiana ujinga.
Hapana. Yeye ni mmoja wa watu wanaoamini katika Mungu na sala. Kama anaumwa, tunapaswa kumwombea apone maradhi yake. Sidhani ni sahihi kumwombea apone kama haumwi - hapo ndio umuhimu wa kusema anaumwa ama la unakuja.

Kuumwa ni sehemu ya maisha ya binadamu. Kuumwa si kuwa dhaifu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…