Yupo wapi siku hizi?

Yupo wapi siku hizi?

Kuna yule demu aliimbaga ''kalamu na karatasi vinarahisisha mambo.... " ilikuwa kama rap fulani hivi, chorus aligonga Nuruel nadhani. Huyo demu aliwahi pia kushirikishwa kwenye wimbo fulani by James Dandu.

Huyo mdada jina lake Nani? Na yupo wapi ?

Nilikuwa chalii sana by that time. I liked that song sanaaa.

-Kaveli-
Yes demu flani hivi alikuwa ana nyama nyama hivi na mwanya flan hivi amaizing.
 
'Da Jo' from Kigamboni.... the female emcee who made me start internalising bongo hip hop. I loved muuuch ile flow yake ya kurap.

'Da Jo' yupo wapi nowadays? Anafanya nini?

One of my most favourite female emcees wa bongo hip hop by then.

-Kaveli-
Da Jo Da Jo tumekukubaliiiii ,Na badoooo ft BAD SPARK.
 
Ah we da jo tumekukubali...
Na bado nadhani kuna swaliii... [emoji23] [emoji23]

Kuna ile, "we si ndo uloleta nyodo, unataka soo"
"Inspectah mwenyewe anazimia na mimi akiniona ohoo Miss Kigamboni" - Da Joh
 
BDP wametawanyika tawanyika but habari njema ni kwamba hapa majuzi wamesharekodi wimbo bado kuutoa tuu... Issa yupo kigamboni, drez kimara na computer pose nadhani ndio kabaki kino.
Hivi kati ya hao nani anayeitwa MWASUBIRA??
 
Flo
Habari wakuu.

Nimeona kuna haja ya kuanzisha uzi maalumu wa kufahamu walipo baadhi ya watu wetu waliowahi kujulikana sana enzi hizo.

Leo naanza kwa kutaka kujua wapo wapi watu hawa?

1) Flora Nducha wa Radio One
2) Enika wa baridi kama hii
3) Peter Manyika- Kipa wa Yanga
4) Snare wa East Coast Team
5) KR jibaba wa Wanaume TMK
6)Sinta wa Juma Nature
7) Suma Lee na CPWAA
8) Angel Damas aliwahi kua Miss Tanzania
9) K.sal Mwana Mkiwa
10) Edger Maokola Majongo
11) Masood Sura Mbaya
12) Yule mtunzi wa Jumba la Dhahabu
13) Kibakuli na Swebe wa Kaole
14) Tina na Mjuba wa Tausi
15) Mabaga Fresh

List imeongezeka
Wapo wapi hawa?

1) Sekion David
2)Nyamayao
3)Bab lee wa Kizizi
4)Jimmy Plus wa Misukosuko
5)Tabia wa Kidedea
6) Paulin Zongo
7) Mama Terry wa Ushauri Nasaha
8) MB Dogg na Marlaw
9) Sajna na CSir Madini wa Tetemesha
10) Bery Black na Bery White wa Znz
11) LWP
12) Pingu na Deso
13) YP na YDash
14)Nina wa Mambo hayo
15)Besta

Wengine
1) Rose Chitala
2) Danny Msimamo
3) Da Jo
4) Farida RK
5) Dunga Mandugu Digital
6)
7)
8)
9)
10)
11)
12)
13)
14)
15)


Tujuzane tu

Na kama kuna mtu aliwahi kukufurahisha enzi hizo mtaje hapa jungu kuu halikosi ukoko tujue wapo wapi na wanafanya nini.

kulingana na maoni inasemakana wapo wachache wameshatungulia mbele za haki (R.I.P) wapumzike pema!

Ahsanten.
Flora nducha na Rose chitala. Umenikumbusha mbali sana. Kuna Abubaqar Sadick. Kuna kibwagizo kiliimbwa nahisi ni banza stone akiwataja watangazaji wa Radio one enzi hizo. Kina Misa ya Bingi (huyu sikuwahi kumfuatilia sana ila nahisi lilikuwa jibaba flani bongebonge) enzi hizo tv ni za kuhesabu, ukimuona mtangazaji wa radio kwenye tv, unasimulia wiki nzima
 
KR mara ya mwisho nmemuona Wasafi Festival dar na kwenye interview wasafi tv
 
Back
Top Bottom