Kwa Shutuma zake nyingi na zisizovumilika namuomba Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan aamuru Kukamatwa upesi kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kisha Yusuf Manji awe Shahidi #1 wa yanayomsibu.
Kila nikikumbuka Tukio alilofanyiwa Manji wa Watu pale Kwake Sea View huku Paul Makonda akiratibu Zoezi zima hadi Manji Chozi la Uchungu kuntoka baada ya Pesa zake zaidi ya Bilioni 3 Kunyakuliwa na Gari lake la Thamani Mhusika kulichukua na Kujimilikisha na aliyelala Kimoja sasa Geita akibariki Krav Maga huwa naumia sana.
Yusuf Mehboob Manji usiogope Kuusema huu ukweli ambao najua hata Rafiki yako mkubwa Rais Mstaafu Mzee Kikwete pamoja na Mwanae Ridhwani ( ambao nao walidharauliwa sana na Makonda aliyokuwa RC wa Dar ) wanalijua hili ila waliogopa kusema kwa Baba yake wa Hiari yasije yakawakuta nao.
Najua yakianza Kufumuka ya Paul Makonda nina uhakika wote tutakubaliana kuwa alichokifanya Ole Sabaya ni cha Mtoto kama ni Viumbe wa Majini ( Baharini ) kwa Ufisadi, Uonevu na Ukatili Sabaya ni Papa ila Makonda ni Nyangumi.
Na ninashangaa kwanini hajakamatwa.