TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

Mbona mtandaoni hakuna hiyo stori? If it is true RIP Manji.

Huu mwaka ni mbaya mno kuwahi kutokea, hapa ni June tu kuna vifo vingi sana vya watu wa kawaida na maarufu duniani mf vifo vya viongozi kama Rais wa Iran, Makamu Rais Malawi, Mkuu wa Majeshi Kenya, yani kuna mabalaa kila mahali , kuuwawa watu kwenye ukumbi Russia, mafuriko makubwa yaliyoua watu wengi Dubai, India, Kenya, TZ, Burundi nk, vifo vya mahujaji zaidi ya 1000 kwa joto huko Saudi Arabia, kuuwawa protesters Kenya watoto wa Gen Z sijui wamefika 27 , lakini kitu kibaya zaidi ni vifo vya watoto wasio na hatia hapa TZ mtoto albino asie na nguvu za kupigania uhai wake kwa madhalimu akiwemo baba yake mzazi, mtoto Asimwe na huko Gaza watoto wadogo wanauwawa sana kwa kupigwa mabomu, kunyimwa chakula, kunyimwa matibabu na dunia nzima imebariki iko kimya , pia kuna vita kali ya Gaza, Myanmar, Sudan, Congo DR, Ukraine watu wanauwawa sana huko nk.

My take :
Allah is not happy with the world for genocide in Gaza ambako ni ardhi takatifu iliyomtoa Nabii Issa bin Mariam, Nabii Mussa, nk kule watu hawana chakula, hawana pa kulala na hawana maji , wanapigwa mabomu mda wote na dunia nzima ikitazama tu. Tumuombe sana Mungu maana bado kuna miezi 6 mbele balaa kila mahali, kila kukicha!
Kiongozi umeandika maneno mazito kweli kweli. Mungu atujarie neema yake, duniani kumejaa dhiki faraja ni chache
 
View attachment 3029953
Yusuf Manji enzi za uhai wake
Mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mdhamini wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki dunia jana Jumamosi Juni 29, 2024 saa 6 usiku katika Jimbo la Florida nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wake, Mehbub Manji akizungumza na Mwananchi Digital muda mfupi uliopita.

Yusuf Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), kampuni inayojihusisha na sekta mbalimbali kama vile magari, ujenzi, vifaa vya kilimo, utalii, huduma za afya, na mali isiyohamishika.

Manji pia alifahamika kwa kujihusisha na shughuli za kijamii na misaada mbalimbali nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga.

Pia Manji alijihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Manispaa ya Temeke. Septemba 6, 2017 alipoteza sifa ya Udiwani kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Atakumbukwa kwa mafanikio makubwa na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.

Pia soma
- Yusuf Manji apoteza sifa ya kuwa Diwani wa Mbagala Kuu kwa kushindwa kuhudhuria vikao
Rip Manji.....
 
Mimi namzungumzia manji hakuwaga MTU wa maneno mengi Wala longo longo Wala blabla..

Barabara zote kijichi Zina lami hio yote Ni Asante MANJI..

Ni boss ambae Hakuwa na maneno mengi Ni mzee wa action na wote ambao wamewai ku SHARE A MOMENT FOR LIFE na manji wanamuelezea Kama a real GENTLEMAN

Askofu GWAJIMA aliwai kumzungumzia manji kwa mazuri walipo kutana kituo Cha polisi walipo itwa na makonda kipindi Cha Ile saga ya madawa ya kulevya

Pia siku za mwisho za uhai wa magufuli walikutanaga na manji kwenye uzinduzi wa viwanda vya manji morogoro...

Apumzike kwa amani Tajiri MANJI
Unapuyanga sana kuchanganya mafile
 
View attachment 3029953
Yusuf Manji enzi za uhai wake
Mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mdhamini wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki dunia jana Jumamosi Juni 29, 2024 saa 6 usiku katika Jimbo la Florida nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wake, Mehbub Manji akizungumza na Mwananchi Digital muda mfupi uliopita.

Yusuf Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), kampuni inayojihusisha na sekta mbalimbali kama vile magari, ujenzi, vifaa vya kilimo, utalii, huduma za afya, na mali isiyohamishika.

Manji pia alifahamika kwa kujihusisha na shughuli za kijamii na misaada mbalimbali nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga.

Pia Manji alijihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Manispaa ya Temeke. Septemba 6, 2017 alipoteza sifa ya Udiwani kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Atakumbukwa kwa mafanikio makubwa na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.

Pia soma
- Yusuf Manji apoteza sifa ya kuwa Diwani wa Mbagala Kuu kwa kushindwa kuhudhuria vikao
Mungu aiweke roho ya mwenzetu mahali inapostahili .
Vipi mwenzetu hadi umauti alikuwa na umri gani?
 
Back
Top Bottom