TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

TANZIA Yusuf Manji, Mfanyabiashara maarufu aliyewahi kuwa mdhamini wa Yanga SC afariki dunia nchini Marekani

Tulikuwa kwenye kahawa mmoja wetu akasema huyu manji aliwahi kumwambia Magufuli kipindi akiwa waziri kuwa hawezi kuongea na mbwa Bali ataongea na mwenye mbwa(jakaya jigwete)Mwenye kujua issues ilikuwa Nini?
 
Tulikuwa kwenye kahawa mmoja wetu akasema huyu manji aliwahi kumwambia Magufuli kipindi akiwa waziri kuwa hawezi kuongea na mbwa Bali ataongea na mwenye mbwa(jakaya jigwete)Mwenye kujua issues ilikuwa Nini?
Kafukue Kaburi wakwambie Nini Chanzo Ila kikubwa ni mmoja alikua Boss mwingine kijakazi by the time sasa ulipofika muda Meza ikapinduka ndio hapo itoshe kusema ukitaka kwenda kulipa kisasi basi jiandalie makaburi mawili na majeneza mawili moja lako na jingine la yule unaeenda kumlipiza kisasi maana kufa kupo asikwambie mtu

RIP Manji
RIP Magu
 
View attachment 3029953
Yusuf Manji enzi za uhai wake
Mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mdhamini wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki dunia jana Jumamosi Juni 29, 2024 saa 6 usiku katika Jimbo la Florida nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wake, Mehbub Manji akizungumza na Mwananchi Digital muda mfupi uliopita.

Yusuf Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), kampuni inayojihusisha na sekta mbalimbali kama vile magari, ujenzi, vifaa vya kilimo, utalii, huduma za afya, na mali isiyohamishika.

Manji pia alifahamika kwa kujihusisha na shughuli za kijamii na misaada mbalimbali nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga.

Pia Manji alijihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Manispaa ya Temeke. Septemba 6, 2017 alipoteza sifa ya Udiwani kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Atakumbukwa kwa mafanikio makubwa na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.

Pia soma
- Yusuf Manji apoteza sifa ya kuwa Diwani wa Mbagala Kuu kwa kushindwa kuhudhuria vikao
Angefariki kipindi cha Mwamba Jiwe Magufuli, ingesemwa Mwamba anahusika. Sijui Sasa hivi watasemaje!!
 
Back
Top Bottom