Mbona mtandaoni hakuna hiyo stori? If it is true RIP Manji.
Huu mwaka ni mbaya mno kuwahi kutokea, hapa ni June tu kuna vifo vingi sana vya watu wa kawaida na maarufu duniani mf vifo vya viongozi kama Rais wa Iran, Makamu Rais Malawi, Mkuu wa Majeshi Kenya, yani kuna mabalaa kila mahali , kuuwawa watu kwenye ukumbi Russia, mafuriko makubwa yaliyoua watu wengi Dubai, India, Kenya, TZ, Burundi nk, vifo vya mahujaji zaidi ya 1000 kwa joto huko Saudi Arabia, kuuwawa protesters Kenya watoto wa Gen Z sijui wamefika 27 , lakini kitu kibaya zaidi ni vifo vya watoto wasio na hatia hapa TZ mtoto albino asie na nguvu za kupigania uhai wake kwa madhalimu akiwemo baba yake mzazi, mtoto Asimwe na huko Gaza watoto wadogo wanauwawa sana kwa kupigwa mabomu, kunyimwa chakula, kunyimwa matibabu na dunia nzima imebariki iko kimya , pia kuna vita kali ya Gaza, Myanmar, Sudan, Congo DR, Ukraine watu wanauwawa sana huko nk.
My take :
Allah is not happy with the world for genocide in Gaza ambako ni ardhi takatifu iliyomtoa Nabii Issa bin Mariam, Nabii Mussa, nk kule watu hawana chakula, hawana pa kulala na hawana maji , wanapigwa mabomu mda wote na dunia nzima ikitazama tu. Tumuombe sana Mungu maana bado kuna miezi 6 mbele balaa kila mahali, kila kukicha!