Wewe ndio unapenda ubishani kwa kuketa mifano ya kijinga.
Azam wametambulisha kocha kutoka Senegal hata miezi miwili hajamaliza, lakini hiyo haiwafanyi walizike na kuona eneo la coaching limerekebishwa.
Wanaweza kumsajili kocha ambaye ni bora kuliko huyu, then huyu msenegal abakie kuwa assistant coach.
Sasa kuja na hoja za kusema hakuna coach mwenye uwezo kama fulani hapo unakuwa hujui ulimwengu wa mpira.
Kwenye ulimwengu wa soka zipo mbinu nyingi ambazo zinatumika kufanya Club ifikie malengo yake.
Badala ya kuhonga timu kupanga matokeo nje ya uwanja, Club inaweza kusajili kwa lengo hata la kupunguza makali ya mpinzani, yani nikiona hapo Gongowazi msumbufu ni Nabi, namsajili Nabi nawaacha muendelee kutaabika.