Hata hivyo sidhani kama kuchukuwa uraia wa marekani ni sawa na kuukana wa Tanzania.
Pamoja na kwamba hakuna uraia pacha Tanzani, lakini watu hawaelewi hilo.
Easy Papa Manji.
Article don.
If you have two dollars, you will give away one.
Kupata uraia wa Marekani kuna kitu kinaitwa "Oath of Allegiance". Hiki ni kiapo cha utii ambacho kina maneno kwamba mla kiapo anaachana na allegiance ya nchi zote na kuweka allegiance Marekani.
Hiki kiapo ndicho kitu pekee kinachoweza kumfanya mtu aseme kuwa ukichukua uraia wa Marekani unaukana uraia wa nchi yako.
Lakini, State Department, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, imefafanua kuwa watu wanaochukua uraia wa Marekani hawaukani uraia wao wa awali, wanabaki nao, Marekani haijali kuhusu uraia huo, suala la kama wanaendelea au hawaendelei kuwa raia wa nchi hizo, ni suala kati ya hao watu na hizo nchi, Marekani haihusiki katika hilo.
Zaidi, kuukana uraia wa Tanzania kunatakiwa kufanywa kwa process maalum, process hiyo ina form na ada ya kulipia. Kama mtu hajajaza hiyo form na kutoa hiyo ada, bado hajaukana uraia wa Tanzania.
Sasa, Manji alijaza hiyo form na kuilipia ada ya kuukataa uraia wa Tanzania?