Mfikirishi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 8,939
- 10,403
Tatizo hata challenges kutoka nje ya ccm zinabinywa kwa njia nyingi. Kuanzia uraia, kodi n.k!Unajuwa mkuu 'Halaiser', hata sisi wengine (wewe na mimi) tulio nje ya haya maswala, wakati mwingine tunajikuta tukichnganya akili kama wao hao hao waliomo ndani.
Ni nani asiye juwa kwamba hizi taratibu (katiba, n.k.,) ni kama mapambo tu inapo fikia wakati wa kupigania maslahi ya makundi.
Chukulia kama hilo la kutambua hii ni "Awamu " ya ngapi? Hili lina nguvu gani ndani ya CCM?
Sote tuna fahamu, mwenye nguvu na uamzi ni Mwenyekiti na timu yake; wakati huo huo akiwa Rais mwenye mamlaka na Dola, aliyo na mamalaka yote ya kuitumia atakavyo yeye kufikia malengo yake.
Sasa niambie, ni nani huko ndani ya CCM anaye weza kujenga kundi la kumtisha mtu mwenye nyenzo zote hizo!
Hawa wote ndani ya CCM ni watu wanao tegemea fadhila toka kwa mtu huyo huyo. Wataanzia wapi kum'challenge' huyu!
Nionavyo mimi. Hayo unayo yaeleza kuwa unayasikia sasa hivi; hayo ni maneno tu yanayo pita huko mitaani. Wakati wenyewe utakapo wadia, kila mtu atalala ndani ya msitari asikose fursa zinazo tegemewa kwa anaye zigawa.
Huko ndani ya CCM sioni hata mmoja wao mwenye uwezo wa kumtikisa mwenyekiti wao.
Kama ni 'challenge' ni kutoka huku nje ya chama.
Kifupi mabadiliko ili yatokee inabidi wananchi wawe na hamasa zaidi ya ile iliyojengwa na Lowassa vs JPM 2015!