Pre GE2025 Za ndani kabisa 2025, Fomu ya urais ndani ya CCM ni zaidi ya moja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tatizo hata challenges kutoka nje ya ccm zinabinywa kwa njia nyingi. Kuanzia uraia, kodi n.k!
Kifupi mabadiliko ili yatokee inabidi wananchi wawe na hamasa zaidi ya ile iliyojengwa na Lowassa vs JPM 2015!
 
Kifupi mabadiliko ili yatokee inabidi wananchi wawe na hamasa zaidi
Jibu ni hili hapa.
Kinacho takiwa sasa hivi ni kuiunganisha vizuri "hamasa" hiyo ya wananchi. Hamasa tayari ipo ya kutosha sana kumkataa huyu mama.
Kwa sasa hivi, ni CHADEMA ndiyo wenye nafasi ya kui 'co-ordinate' vizuri hamasa hiyo. Kuna mambo mengi sana wasiyo yataka wananchi kutokana na uongozi wa huyu mama.
 
kundi la wazee type ya kina kinana wasiozid 20 kwenye meza ya round jina likipita kazi inayobakia ni kulilinda kwa njia zote
Hii ni kwa mjibu wa akili yako inavyo kuelekeza wewe. Usifanye ndio uwe ukweli usio hojiwa!
Na kwa maoni yako, hao wazee uwajuao wewe tayari wanalo jina la Samia mezani, au siyo?
 
CHADEMA wana shida sana wale. Wanajiwazaga wao kabla ya wananchi!
Ilipaswa waje na sera kuwafungulie milango wote wasiomkubali bi Chura.
Lakini kwa ninavyo wafahamu wataanza masuala ya kuwaogopa wahamiaji!
Kushinda uchaguzi is all about numbers!
 
Ni kweli ana nguvu sana. Lkn jiulize kwanini mabango ya kumtangaza yametapakaa nchi nzima? Kwanini Misaada Makanisani na Misikitini yameshamiri kipindi hiki kuliko awamu zingine?? Kwanini bajaji, pikipiki na baisikeli zinamwagwa nchi nzima??

Nafikiri utakumbuka 2015 wakati wa kumpata Mgombea wao,.M/Kiti wao wakati ule chaguo lake hakuwa Jiwe. Na aliyempambania Jiwe unamkumbuka. Hivyo wakati mwingine M/Kiti wao huzidiwa. Kwamaana nyingine kuna Kundi lenye nguvu zaidi ndani ya Chama chao. Je ikitokea Kundi lile kulikubali Upande wa Pili wa Chama kile bado M/Kiti wao atakuwa na nguvu??

Nionavyo mimi ni kwamba anatumia nguvu nyingi kupambana na Wapinzani wa Vyama vilivyo nje ya CCM. Badala ya kupambana na Wapinzani wake ndani ya Chama chake. Naliona anguko lake kubwa toka kwa Wana CCM wenzie.
 
Nipo tayari ku-'bet' milioni tano (Tsh 5 milioni), kuwa hii ndiyo komedi tunayo isubiri itokee; na ndivyo itakavyo kuwa hivyo.
Endelea kuota.Ikiwa ni ndoto basi haina madhara.Ukiamka kutoka kwenye ndoto angalia usijinyee ukasingizia ndoto.
 
Ni kweli ana nguvu sana. Lkn jiulize kwanini mabango ya kumtangaza yametapakaa nchi nzima? Kwanini Misaada Makanisani na Misikitini yameshamiri kipindi hiki kuliko awamu zingine?? Kwanini bajaji, pikipiki na baisikeli zinamwagwa nchi nzima??
Hii ndiyo sababu hasa ya Mwenyekiti kutozongwa na yeyote ndani ya CCM. Huu ni ushahidi tosha na sababu za kumzuia mwingine yeyote kuthubutu kum'challenge' mwenyekiti.
Nafikiri utakumbuka 2015 wakati wa kumpata Mgombea wao,.M/Kiti wao wakati ule chaguo lake hakuwa Jiwe
Sasa, elewa kuwa Mwenyekiti wakati huo, Kikwete, hakuwa na maslahi ya kupigania tena; kwa sababu alikuwa hana nia, wala nafasi ya kugombea tena nafasi ya Rais.
Hali ni tofauti/ni kinyume kabisa na ilivyo sasa. Samia anautaka u-Rais kwa udi na ubani; na ndiye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.
 
Huwa kikanuni anapaswa kujivua uenyekiti wa chama wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya chama.

Hapo ndipo mzanzibari huyu hatoamini macho yake.
"
EEEeeeeHEEEeeeee!
Umenifanya nicheke sana mkuu G4N!

"Atajivua uenyekiti", amwachie nani?
Hivi hizo "kanuni" huko CCM unadhani zina maana yoyote?
Yeye ni Mwenyekiti; atakuwa mwenyekiti wa ajabu sana kwa yeye "kujivua" na kumwachia mtu ambaye hana uhakika naye kuwa yupo kwenye mstari sahihi.
Tazama vizuri ndani ya hiyo CCM sasa hivi. Tazama wajumbe wa Kamati Kuu ni akina nani; na sijui Halmashauri kuu, n.k.. Mwenyekiti ataachia tu bila kuwapanga watu wake kuhakikisha hakuna litakalo haribika wakati anaachia?
 
Bahati Yako mm mtumishi, hiyo pesa Yako ningeila kirahisi sn!
Tusifanye masihala mkuu 'Rabbon'. Sijawahi hata siku moja kutaniana na wewe, kwa kuheshimu misimamo yako katika mambo muhimu ndani ya taifa letu hili.
Kamwe sitanii; kwamba aliyo eleza mkuu 'FUSO' hapo juu, ndiyo 'comedy' yenyewe itakayo onyeshwa wakati utakapo wadia. Nami nipo tayari kabisa kusimamia uhakika wa hayo. Ndiyo maana sina shaka yoyote juu yake. Ikitokea vinginevyo, wewe nifahamishe tu; hata kupitia humu humu JF, nitimize ahadi yangu.
 
Hiyo ramli Haina tofauti na wale waliosema Samia atashindwa na hatomaliza miaka 2.

Leo wako wapi? πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Hiyo Ngoma ni Hadi 2035 Mzee πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://x.com/Jambotv_/status/1859271082378752226?t=sM9iyUbPJuFQW7b3kjFPZw&s=19
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…