Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Sasa anajenga ni aliyesaini au anaetoa pesa? [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Mdanganye asitishe Mradi wa JPM aone atakavyokuwa humiliated kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.. miradi ya JPM ndo inambeba [emoji1787]
 
Mdanganye asitishe Mradi wa JPM aone atakavyokuwa humiliated kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.. miradi ya JPM ndo inambeba [emoji1787]
Ili iwaje?

Samia Sio mjinga kama Mwendazake aliyesitisha Bagamoyo Port Kwa sababu za wivu
 
Dah! Kigoma haijapewa hata hatua 1. Mpango hana msaada na kigoma.
Kigoma ndio Mkoa unajengwa Barabara nyingi Kwa Sasa hapa Tanzania tena za Kisasa..

Nyingine hii hapa πŸ‘‡
 
Taja Barabara, miradi ya kimkakati ndio Mdudu gani? [emoji23][emoji23]
Yaani wewe una tatizo katika kufikri. Unaishi Tanzania ipi hadi hujui miradi ya kimkakati kiasi cha kung'ang'ania nikutajie barabara, du! SGR haiunganishi tu Mikoa ila hadi nchi kwa nchi. Reli ya Dar Arusha ilifufuliwa. Meli kwenye maziwa zinajengwa mpya na za zamani zimekarabatiwa kuunganisha mikoa na nchi kwa nchi. Madaraja yamejengwa kuunganisha mikoa au kupunguza misongamano katika majiji. Viwanja vya ndege vimepanuliwa kuwezesha ndege zilizonunuliwa na Mwendazake ziweze kurahisisha usafiri mkoa kwa mkoa.

Awamu hii ni barabara gani mpya zimejengwa? Alizoacha mwendazake ngapi zimekamilishwa? Hizo unazopigia vuvuzela bado ziko kwenye makaratasi tu.

Kwa kuwa unang'ang'ania utajiwe barabara zinazounganisha mikoa alizokamilisha Mwendazake, kama hujui ngoja nikukumbushe maono yake yaliyoainishwa kwenye Ilani ya CCM (2020) akiwa hai, Sura ya Kwanza.

9. Kukuza uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani uliojengwa katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi:-
(i) Kujenga na kukuza uchumi shindani hususan kupitia sekta
za viwanda na huduma za kiuchumi utakaowezesha ustawi wa wananchi wote;
(ii) Kuimarisha miundombinu ya kimkakati ili kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi na tija;
(iii) Kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kukua na kustawi pamoja na kuvutia wawekezaji ili watoe mchango
stahiki katika maendeleo ya nchi yetu;
(iv) Kuboresha masilahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi katika sekta zote;
(v) Kuongeza faida ambazo nchi yetu inapata kutokana na maliasili zetu na utajiri wa nchi kwa kuimarisha usimamizi wa mikataba ya uzalishaji na kujenga uwezo wa ndani wa kuvuna na kuchakata/kusarifu rasilimali hizo;


Katika hayo kuna jipya lipi Awamu imefanya? Katika maono hayo ya Mwendazake, ni kwa kiwango gani Serikali ya sasa imekamilisha?

Hayo maswali ndiyo ya kujadili la, ni Akili ya urofa tu.
 
Umeishiwa 😁😁😁😁
Nimecheka 🀣🀣🀣🀣
Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.

Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.

Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.

Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.

Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.

Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.

Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.

Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.

Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?

Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?

Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.

Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.
 
Umemfunua uchi CHAWA na watetezi wengine kama yeye.

Isitoshe hatuna sheria ya kusimamia mkataba wa EPC+F na kwa kuwa haujewekwa wazi, hatujui madhara yake "Contractor" au "Sisi (Taifa)" tukishindwa kutimiza masharti ya mkataba
 
Barabara za kulipia Huwa ndio Zina element ya BOP na kiukweli ni chache sana Africa Kwa sababu inaleta ukakasi wa Kisiasa Kwa hapa Africa na Tanzania in particular
Salaam ndugu,
Kimsingi Hakuna barabara tunazotumia zizizolipiwa..tunalipa Siku zote kupitia tozo maalumu iwekwayo ktk Mafuta..

Iwe mkulima,Mfanyakazi,Mfanyabiashara..Whenever we purchase diesel or petroleum products we pay Road Toll..

Imewekwa in directly..Hakuna asielipa..Kama ambavyo tunavyolipa Ewura,REA kupitia manunuzi ya umeme kila leo..

Wananchi tunabeba mizigo ya kodi na tozo kila eneo..Ni vema viongozi wetu wakaongeza umakini ktk matumizi na ukopaji ambao tutalipa tu Kama sio Sisi vizazi vyetu..
 
Kwenye mikataba ya ujenzi, ambapo mwenye mradi anamlipa "Contractor" fedha ya kutekeleza, anapaswa kuweka dhamana. Lakini aina hii ya mkataba ambapo "Contractor" anatumia fedha yake aweke dhamana ya nini?
Performance as per contract.
What if aki underperform?
What if akilipua ujenzi?
 
Hatupaswi kuwafurahia sana wachina..
Tuweke taratibu Za wazi zaidi ili kuvutia wakandarasi bora toka ktk mataifa mengine makubwa Japan,Korea na Kwingineko..

Zipo tuhuma nyingi juu ya Sifa za makampuni ya kichina kwenye Utoaji Rushwa ili kupata miradi (They are very aggressive ktk hili) hili si la kubezwa..Na wanapotoa rushwa hufanya madudu ktk quality delivery..
 
Mbakaza manaake Nini?
 
Magufuli kuanzisha mengi mazuli tu pia kafanya uharibifu mkubwa sana leo bungeni kuna kundi 1 tu la ndio mzee yote hii sababu ya magu lakini tumsamehe sababu alisha kufa,mama nae yuko njema kila alianzisha mzee baba hana malizia bila hila
 
[emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…