Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Mdanganye asitishe Mradi wa JPM aone atakavyokuwa humiliated kwenye uchaguzi wa mwaka 2025.. miradi ya JPM ndo inambeba [emoji1787]
Ili iwaje?

Samia Sio mjinga kama Mwendazake aliyesitisha Bagamoyo Port Kwa sababu za wivu
 
Dah! Kigoma haijapewa hata hatua 1. Mpango hana msaada na kigoma.
Kigoma ndio Mkoa unajengwa Barabara nyingi Kwa Sasa hapa Tanzania tena za Kisasa..

Nyingine hii hapa 👇
Screenshot_20230617-185132.jpg
 
Taja Barabara, miradi ya kimkakati ndio Mdudu gani? [emoji23][emoji23]
Yaani wewe una tatizo katika kufikri. Unaishi Tanzania ipi hadi hujui miradi ya kimkakati kiasi cha kung'ang'ania nikutajie barabara, du! SGR haiunganishi tu Mikoa ila hadi nchi kwa nchi. Reli ya Dar Arusha ilifufuliwa. Meli kwenye maziwa zinajengwa mpya na za zamani zimekarabatiwa kuunganisha mikoa na nchi kwa nchi. Madaraja yamejengwa kuunganisha mikoa au kupunguza misongamano katika majiji. Viwanja vya ndege vimepanuliwa kuwezesha ndege zilizonunuliwa na Mwendazake ziweze kurahisisha usafiri mkoa kwa mkoa.

Awamu hii ni barabara gani mpya zimejengwa? Alizoacha mwendazake ngapi zimekamilishwa? Hizo unazopigia vuvuzela bado ziko kwenye makaratasi tu.

Kwa kuwa unang'ang'ania utajiwe barabara zinazounganisha mikoa alizokamilisha Mwendazake, kama hujui ngoja nikukumbushe maono yake yaliyoainishwa kwenye Ilani ya CCM (2020) akiwa hai, Sura ya Kwanza.

9. Kukuza uchumi wa kisasa, fungamanishi, jumuishi na shindani uliojengwa katika msingi wa viwanda, huduma za kiuchumi na miundombinu wezeshi:-
(i) Kujenga na kukuza uchumi shindani hususan kupitia sekta
za viwanda na huduma za kiuchumi utakaowezesha ustawi wa wananchi wote;
(ii) Kuimarisha miundombinu ya kimkakati ili kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi na tija;
(iii) Kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kukua na kustawi pamoja na kuvutia wawekezaji ili watoe mchango
stahiki katika maendeleo ya nchi yetu;
(iv) Kuboresha masilahi na mazingira ya kazi kwa wafanyakazi katika sekta zote;
(v) Kuongeza faida ambazo nchi yetu inapata kutokana na maliasili zetu na utajiri wa nchi kwa kuimarisha usimamizi wa mikataba ya uzalishaji na kujenga uwezo wa ndani wa kuvuna na kuchakata/kusarifu rasilimali hizo;

Katika hayo kuna jipya lipi Awamu imefanya? Katika maono hayo ya Mwendazake, ni kwa kiwango gani Serikali ya sasa imekamilisha?

Hayo maswali ndiyo ya kujadili la, ni Akili ya urofa tu.
 
Umeishiwa 😁😁😁😁
Nimecheka 🤣🤣🤣🤣
Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.

Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.

Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.

Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.

Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.

Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.

Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.

Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.

Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?

Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?

Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.

Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.
 
Umemfunua uchi CHAWA na watetezi wengine kama yeye.

Isitoshe hatuna sheria ya kusimamia mkataba wa EPC+F na kwa kuwa haujewekwa wazi, hatujui madhara yake "Contractor" au "Sisi (Taifa)" tukishindwa kutimiza masharti ya mkataba
 
Barabara za kulipia Huwa ndio Zina element ya BOP na kiukweli ni chache sana Africa Kwa sababu inaleta ukakasi wa Kisiasa Kwa hapa Africa na Tanzania in particular
Salaam ndugu,
Kimsingi Hakuna barabara tunazotumia zizizolipiwa..tunalipa Siku zote kupitia tozo maalumu iwekwayo ktk Mafuta..

Iwe mkulima,Mfanyakazi,Mfanyabiashara..Whenever we purchase diesel or petroleum products we pay Road Toll..

Imewekwa in directly..Hakuna asielipa..Kama ambavyo tunavyolipa Ewura,REA kupitia manunuzi ya umeme kila leo..

Wananchi tunabeba mizigo ya kodi na tozo kila eneo..Ni vema viongozi wetu wakaongeza umakini ktk matumizi na ukopaji ambao tutalipa tu Kama sio Sisi vizazi vyetu..
 
Kwenye mikataba ya ujenzi, ambapo mwenye mradi anamlipa "Contractor" fedha ya kutekeleza, anapaswa kuweka dhamana. Lakini aina hii ya mkataba ambapo "Contractor" anatumia fedha yake aweke dhamana ya nini?
Performance as per contract.
What if aki underperform?
What if akilipua ujenzi?
 
Nchi haiweki dhamana badala yake Contractor ndio anatakiwa kuweka dhamana ya pesa ndefu in form of bank guarantee Ili sisi tumbane Financier wake..

Kumbuka hii model mkandarasi ndio anabear takribani risks zote ambazo yeye ameziweka kwenye bei(offer price).

Mwisho uzuri contractors wengi ni Wachina na Taifa lao Lina uwezo Sasa Til.4 ni pesa ndogo sana kwao ndio maana umeona contractor wa 4 tuu kwenye miradi 7.
Hatupaswi kuwafurahia sana wachina..
Tuweke taratibu Za wazi zaidi ili kuvutia wakandarasi bora toka ktk mataifa mengine makubwa Japan,Korea na Kwingineko..

Zipo tuhuma nyingi juu ya Sifa za makampuni ya kichina kwenye Utoaji Rushwa ili kupata miradi (They are very aggressive ktk hili) hili si la kubezwa..Na wanapotoa rushwa hufanya madudu ktk quality delivery..
 
Ahadi hewa watu wamesaini mikataba 😆😆 we Jamaa Bure kabisa..

Kwanza tangu lini Samia amewahi kukupa ahadi hewa? Kwanza sio Barabara tuu Bali Hadi kwenye Afya amefanya mapinduzi, kwenye Elimu ndio kabisa Watoto wooote wanapata mkopo na Sasa kawaongeza wa diploma,Ajira ndio usiseme..

Samia ni kichwa kingine,anataka awasaidie huko kwenye bandari Wajamaa mbakaza Kwa kung'ang'ania umaskini na ujinga 😁😁😁
Mbakaza manaake Nini?
 
Duh! wewe mweu aliyeanzisha elimu Bila malipo unamjua wewe, baada ya Nyerere, JPM ndiye aliyesema elimu mpaka kidato cha NNE bure serikali itagharamia, mama yako anaendeleza TU.

Bajeti ya kilimo kufika hapo mama anaendeleza TU, Kwa kuwa JPM alishaanza Kwa kuifanya wizara iwe inajitegemea na alisema kwamba miaka ijayo bajeti ya kilimo itapanda Kwa Sababu 70% ya watanzania wanategemea kilimo, na ndiye aliyemteua bashe kwamba akatekeleze kile anachokizungumza bungeni Ni Kwa vile KIFO kilimkuta hakufanikiwa kukamilisha ndogo yake.

Barabara pia Ni kama unajitekenya yeye Yuko kwenye wizara miaka 20 barabara zote na madaraja yote makubwa yamejengwa na kusimamiwa na JPM Leo hii mnapita juu pale ubungo na sehemu nyingine mnazoendeleza kujenga Ni mitazamo yake kwamba tuko nyuma tubadilike Mzee Wa maamuzi magumu.

Mambo ya nyumba za NHC yeye alisisitiza Kwanza kwamba makusanyo ya nyumba hizo zinaliwa,mtu anakodisha nyumba Kwa mkodishwaji unakuta NHC wanalipwa laki moja alafu Yule mtu kati anachukia millioni,yeye alitaka akomeshe Kwanza ufisadi WA Kodi na miladi hewa na Ile ya isiyo na tija, kama mama yako anaendeleza ujue Kuna mtu kasafisha ndio maana mapato ya NHC yalipanda Kwa Sababu hapakuwa na madalali.

Demokrasia hipi haikuwepo mbona mkutano ilikuwa inaruhusiwa kwenye majimbo na ujue kwamba democracy Ni Jambo la ufahamu TU katiba inajieleza Ni uoga WA upinzani ,Kuna kijana alitaka kuandamana jumatatu amepewa onyo je? Nayo Ni democracy iyo unayoisema.

Ajila zinatolewa Kwa Sababu Ni wajibu WA serikali kuajili,lakini pia uelewe kuwa tofauti Ni viwango vya uajili TU lakini hata JPM aliajili na Sababu KUBWA alisema aondoe Kwanza vyeti feki na wafanyakazi hewa yeye ndiye aliyeweka mfumo Bora WA kutambua watumishi ili kuondoa udanganyifu na kupoteza pesa, hivyo Ni mwendelezo.

Kipindi cha JPM ndipo bank ya dunia ilisema Tanzania tumeingia uchumi WA kati, uchumi Ni suala pana unaweza ukawa unaona pesa IPO mfukoni lakini ikakosa thamani kama sasa elfu Kumi inapata kilo 3 za Mchele,NK;lakini kipindi kile Ni kilo Saba unaweza kulinganisha,kwenye bidhaa nyingine Leo kila kitu kipo juu Hadi JoJo.

Kifupi Ni kwamba anataka aonyeshe kuwa anaweza Ila Ni vizuri Ila afanye na afuatilie hasiache maagizo mlangoni watu wanatumbua pesa sana, pesa alizokopa angekuwa JPM ingekuwa Ni hatari alafu JPM mitazamo yake alitaka tujitosheleze Kwa kila Kwa kuwa ndio MSINGI imara WA nchi huru.
Magufuli kuanzisha mengi mazuli tu pia kafanya uharibifu mkubwa sana leo bungeni kuna kundi 1 tu la ndio mzee yote hii sababu ya magu lakini tumsamehe sababu alisha kufa,mama nae yuko njema kila alianzisha mzee baba hana malizia bila hila
 
Ona fala hili,Mkapa ndio alianza kufuta ada ya primary,JK alifuta ada ya day na kupunguza ya Sekondari, Mwendazake akafuta ya Sekondari,Samia amefuta Hadi form six,na vyuo vya Ufundi vya Serikali na mikopo Hadi Diploma na boom la elfu 10 Juu.

Fala wewe , Mwendazake alipunguza Bajeti ya Kilimo akahamishia hela Nishati na Ujenzi mama mwaka wa kwenda tuu katoa Bajeti kutoka bil.290 Sasa ni bil.970 2023/24..

Ona unavyoleta excuses kama yule yule failure wako,NHC ilikufa nyumba zote zilisimama kuanzia Kigamboni,Morocco square Hadi Kakakuona Tower poster,sekta ya real estates ilikufa kama zilivhokufa sekta zingine mama kafufua Mjini kunachangamka.

Kama Ajira ni wajibu wa Serikali Kwa nini Mwendazake alishindwa kuajiri akasomamisha Ajira,akaua mashirika ya pensio,akatuongezea makato ya Bodi,wizi wa retention fee na upuuzi mwingine kama huo? Hana akili ndio jibu rahisi.

Hakuna mikutano yeyote ikifanyika,Mungu mtu akikosolewa unakula risasi na ushenzi mwingine kama huo Kama watu wasiojulikana kuteka Wapinzani wa Serikali

Mazao yoote yaliporomoka bei Hadi kuficha aibu Kwa eti jeshi kununua korosho [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mwisho;Wajamaa na ujamaa ni upumbavu na umaskini wa akili Hadi Mali, propaganda na Vitisho ndio mnachoweza.
[emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581][emoji3581]
 
Back
Top Bottom