Umeishiwa 😁😁😁😁
Nimecheka 🤣🤣🤣🤣
Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.
Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.
Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.
Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.
Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.
Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.
Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.
Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.
Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?
Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?
Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.
Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.