Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Attachments

  • FD05D11F-FAFD-4A3F-853B-A8DBEE5CD5AF.jpeg
    FD05D11F-FAFD-4A3F-853B-A8DBEE5CD5AF.jpeg
    140.9 KB · Views: 2
  • 1AE9A00D-AF79-402D-BB5A-51FE8156B55E.jpeg
    1AE9A00D-AF79-402D-BB5A-51FE8156B55E.jpeg
    51.3 KB · Views: 2
Kwa mara ya Kwanza baada ya Uhuru Tanzania imepata Rais Samia apewe maua yake.

Serikali ya Rais Samia imeandika Historia nyingine ya ubunifu kwa kusaini kuanza ujenzi wa barabara za kuu za lami kwenye mikoa 13 kwa pamoja zenye jumla ya urefu wa KM 2035 kwa mtindo wa EPC+ F (Engineering, Procurement, Construction and Finance) kwa gharama ya Tsh.Tilioni 3.8 ambapo miradi inatarajiwa Kukamilika ndani ya miaka 4 (2023-2027).


Akizungumza wakati wa kushuhudia kutiwa saini kwa mikataba hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa amesema kwamba, barabara hizo hazitokuwa za kulipia tozo kama wapotoshaji wanavyosema. Ikumbukwe hii haijawahi tokea toka Uhuru, walinda legacy mnafundishwa kazi.

My Take
Samia anawaonesha kwamba Private Sector inalipa kuliko Ujamaa mbuzi ambao baadhi ya watu wasiojielewa wanakumbatia.

Ndio maana hata kwenye Bandari anataka awafundishe namna ya kutumia rasilimali kwa manufaa ya watu badala ya kuhubiri propaganda za Uzalendo mbuzi na umaskini over years.

Hongera sana Mh. Rais, na Waziri wa Mbarawa Kwa Ubunifu,Historia itaandika jina lako kwa wino Mwekundu.

=====

MIRADI YA BARABARA ILIYOSAINIWA KWA UTARATIBU WA EPC + F

i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;

ii) Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa;

iii) Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki;

iv) Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma;

v) Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale;

vi) Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) inapita katika Mikoa ya Manyara, Simiyu, Singida na Arusha na inapita katika Majimbo ya Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Karatu, Iramba Mashariki, Meatu, Maswa Mashariki na Kisesa; na

vii) Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81) inapita katika Mkoa wa Iringa na inapita katika Majimbo ya Mufindi Kusini na Mafinga.

Haya maTozo meeengi uchumi unakuwaje
 
Sio kitu kipya Ulaya au Tanzania? Kipya ni nini?

Malalamiko Yako peleka Kuna husika ila Hii ni game changer hakuna Kiongozi amewahi Jenga Kwa wingi huo Toka Nchi hii Imepata habari..

Ujue nyie midembwedo wa Dar Huwa mnaropoka tuu bila kujua adha ya watu Mikoani.
1. Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;
SWALI:-
Mbona Waathiriwa (wamiliki wa ardhi wanaopisha upanuzi wa barabara) hawajalipwa fidia yao ya kutwaliwa ardhi zao, Je, fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara hii zinaenda kulipa fidia waathiriwa au zinaenda kutumika katika ujenzi wa barabara??? Uthamini wa ardhi tayari ulishafanyika mwaka 2011 na 2012.
Tatizo la fidia pia lipo kwa Barabara ya kutoka Arusha Mjini hadi Kongwa Dodoma, huko uthamini haujafanyika kabisa. Sijui itakuwaje??
 
1. Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;
SWALI:-
Mbona Waathiriwa (wamiliki wa ardhi wanaopisha upanuzi wa barabara) hawajalipwa fidia yao ya kutwaliwa ardhi zao, Je, fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara hii zinaenda kulipa fidia waathiriwa au zinaenda kutumika katika ujenzi wa barabara??? Uthamini wa ardhi tayari ulishafanyika mwaka 2011 na 2012.
Tatizo la fidia pia lipo kwa Barabara ya kutoka Arusha Mjini hadi Kongwa Dodoma, huko uthamini haujafanyika kabisa. Sijui itakuwaje??
Watalipwa tuu
 
Watalipwa lini??
Kwa nini hawakulipwa kabla ya kusainiana mikataba hii ya ujenzi??
Siku zote walikuwa wapi tangu mwaka 2012 wakati uthamini wa ardhi ulipofanyika??
Kwani utekelezaji wa mradi umeanza? Samia sio dhulumati kama yule,pesa mtapewa shida Yako ni nini?
 
Leta hoja achana na ngonjera na michambo, kaimbe taarabu huko, huku hupawezi.
kwahiyo hiyo yako ndio hooooojaaaaa?
acha wenge buda this is Tanganyika hata dead man anaweza ongoza kingine hapa sibanduki
acha kujiona mjaaanja kwa jukwaa la politics nikiingia humu kusumbua ni unstoppable,
halafu sikua serious saaaana ndio maana sipendi ligi za kitoto kamanda wangu,
anyway

CCM ni sawa na shamba la migomba ukizalisha ndizi na mgomba huna kazi wanaku
fyekelea mbali!


#boraandazi
#chamachamambuzi
 
Back
Top Bottom