Zaidi ya kunitia ndani, kunipiga na kunitesa, je mwanasiasa aliye madarakani ana kipi kingine cha kunifanya?

Anaweza pia kukusababishia ulemavu wa kudumu katika mwili wako, anaweza kukusababisha ukimbilie uhamishoni nje ya nchi, anaweza pia kukuua!

Hawa wanasiasa kaa nao mbali kabisa! Maana ni banadamu kwa nje tu. Ila ukiingia ndani ya mioyo yao, aisee ni mbwa mwitu wakali sana.
 
Mkuu wanakutoa roho pia hilo usisahau.
 
Kweli hawa
walioko madarakani walishasaini mkataba wa makubaliano na shetani.
 
Nchi hii watu wanachokipa thamani ni Yanga vs Simba, Conection shoo shoo, umbea, kufatiliana, n.k.
Ndio maana tumeamua wacha Tozo ziwanyoshe kwanza. Wanalia lia tu na mabando na sisi vibomu hatuvumilii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…