Zaidi ya Vijana 100 waondoka kwenye mradi wa BBT, sababu yadaiwa hakuna uelekeo

Hiyo pesa, nguvu,mipango wangeipeleka kwa huko vijijini maeneo yenye watu wanaofanya kilimo kazi yao,

Ova
 
Watanzania ni wachawi na maneno ya watanzania ni ya kichawi. Watu walishasema na kutabiri huu mradi wa BBT hautafanikiwa.
Watu waliona tu,kilimo hawa wanafikiri ni sawa na kukatika
Mauno unacheza singeli amapiano
Kilimo kina wenyewe .. ...
Huko vijijini mashambani kuna mabwana mashamba wapo wapo tu

Ova
 
Hao vijana wamekusanywa kwenye hiyo kambi ,wanalima kwa jembe , hamna hata tractors za kawaida , ni wenyewe ndio walisema ,na hata mifumo ya umwagiliaji hamna
Yaani hao ni peasants WA enzi za mkoloni
Upuuzi mtupu

Sent from my Nokia 6.2 using JamiiForums mobile app
 
Nia njema ya kupiga ilishakamilika kinachotokea sasa ndiyo kilichokuwa kimepangwa
 
Siyo uchawi tatizo mradi ni wazo la waziri siyo wizara wala,serikali hapo ndio shida ina maana waziri anaawafundisha watalaamu cha kufanya baada ya wataalamu wamuelekeze waziri nini chakufanya
Utapeli mtupu
 
Makapi yatenganishwe.

katika andiko la kibiblia, Mathayo 3:12 ambapo inashiria kutenganisha mema na mabaya, au yenye thamani kutoka kwenye yasiyofaa.

Katika muktadha wa BBT, utenganishi wa ngano na makapi yake inaweza kuzingatiwa.

Mafanikio ya vijana hawa BBT inategemea na kanuni hizo hizo, Wapo watakaofanikiwa na wapo watakaoshindwa. Wapo watakakuwa na thamani na wapo watakaokuwa bila ya thamani.

Hiyo haina maana BBT itashindwa.

Mafanikio ya BBT na Vijana waliomo humo yatategemea mambo mchanganyiko, ikiwa ni pamoja na juhudi za mtu binafsi(individuals), usimamizi wa project nzima na mbinu za utekelezaji kwa upande wa Serikali. Wapo watakaofaulu na wapo watakaofeli. Wanaofaulu ndio ngano na hao walifeli ndio makapi yenyewe.

Changamoto hazikosekani katika 'initiatives' za kiuchumi.

Bashe chapa kazi, piga jembe.
 
Watanzania ni wachawi na maneno ya watanzania ni ya kichawi. Watu walishasema na kutabiri huu mradi wa BBT hautafanikiwa.
Mradi ulionekana toka mwanzo hautafanikowa. Mradi umechukua makada tupu na vijana wa mjini wasiojua hata mahindi yanaonekanaje yakiwa shambani.

Mradi umekaa kisanii na mratibu huyo Vumilia ni kyande tu. Hiyo ilikuwa sehemu ya upigaji ya Bashe.
 
Wakulima halisi wenye kazi zao wamewatosa,mna watafuta vijana waliyozoea kushinda kidimbwi ndy muwapeleke shamba,wataweza wapi ???

Ova
Hapo sasa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mradi gani ulionzishwa na viwavi(mchwa) ukafanikiwa? Hapo waliandaa propozo kupiga pesa tu.
 
Watanzania ni wachawi na maneno ya watanzania ni ya kichawi. Watu walishasema na kutabiri huu mradi wa BBT hautafanikiwa.
Tatizo utaratibu uliotumika haukuwa mzuri, walipaswa washirikishwe watu wote kwenye mnyororo wa kilimo (financing, agriculture, market, etc), sasa wao waliishia financing bila kungalia issue za TMX etc. Bashe alikuwa na wazo zuri ila wahuni walimdanganya
 
Taarifa ya kipumbavu hii.
Maelezo hayaoneshi kuna kero gani hapo kambini.
Je, kama hao walioondoka walikuwa wako after something kama P ESA? This thread is Nonsensual and Rubbish
 
Kama barabara za mwendokasi zinajengwa ila magari hakuna na hawana mpango wa kununuatutegemee nini toka kwao?
 
Watanzania ni wachawi na maneno ya watanzania ni ya kichawi. Watu walishasema na kutabiri huu mradi wa BBT hautafanikiwa.
Tulikuwa tu kutokana na utaratibu Kwa umiotumika kuwapata hao vijana. Wengi wao walikuwa watoto ama ndugu wa watumishi wa Halimashauri mbalimbali away makada wa CCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…