Zaidi ya Vijana 100 waondoka kwenye mradi wa BBT, sababu yadaiwa hakuna uelekeo

Zaidi ya Vijana 100 waondoka kwenye mradi wa BBT, sababu yadaiwa hakuna uelekeo

Bado mimi naamini kuwa, nia ilikuwa njema
Changamoto kubwa ni hizi mvua za Elmino zilizonyesha hapo nyuma; wakulima ndio wanajua madhara yake...
waliopo nyuma ya key board hawawezi kuelewa, watabakia kulaumu tu
Hii nimeandika kutokana na uzoefu wangu kwenye masuaa ya Kilimo!
Kwa hiyo hizo mvua ndio zimezuia vijana kupewa mtaji na mashamba kama walivyoahidiwa au? Unamfahamu Chinangali Iko wapi?
 
Naunga mkono,ni ujinga Kwa Serikali eti kutafutiza graduate na kuwafundisha kulima wakati Kuna Vijana wenye passion wako tayari shambani badala ya kuwawezesha hao wao wanalazimisha jobless awe mkulima.

Serikali acheni huo ujinga wa kupoteza pesa Kwa upuuzi unless ni mradi wenu wa kipigaji.Mbaya zaidi waliochaguliwa ni wale wenye kadi za chama
Bashe ni mtu asiyejitambua mtu wa nadharia na si mtu wa vitendo! Anaacha kuchukua vijana wanaolima na wamezoea kilimo kama maisha yao anaenda kuchukua vijana wa Chuo kikuu! Pumbavu kabisa!
 
Zaidi ya vijana 100 wa Programu ya Kuwezesha Ushiriki wa Vijana Katika Kilimo Biashara (BBT- YIA) wanadaiwa kuondoka katika kambi ya Chinangali, Dodoma, ambako vijana hao wamekusanywa, wakidai hakuna mwelekeo kambini hapo, huku wakiishutumu Serikali kwa kushindwa kwake kutimiza ahadi ilizotangaza awali.

Kwa mujibu wa taarifa ilizozifikia The Chanzo, mpaka kufikia jioni ya Machi 19, 2024, vijana waliokuwepo kambini hapo ni kati ya 120 na 128 kutoka vijana 268 ambao Serikali imekuwa ikidai kuwepo Chinangali kushiriki kwenye programu hiyo inayokusudiwa kuongeza ajira za vijana milioni tatu na kuongeza ukuaji wa kilimo nchini hadi kufikia asilimia kumi ifikapo mwaka 2030.

“Watu tulioko pale [kambini] mpaka sasa hivi tunafika 134, kati ya watu 268 tuliotakiwa kuripoti, lakini walioripoti ni 261,” alisema mmoja wa viongozi wa vijana hao ambaye The Chanzo imeamua kutotaja jina lake kulinda usalama wake. “Watu wengine waliobaki hawako kwenye kituo, hawako kwenye kituo kwa sababu pale hakuna kinachoeleweka.”

“Wengine wanakuja, wanakaa siku mbili, wanachungulia, wanaondoka, wale wenye uwezo wa kifedha,” aliongeza kijana huyo. “Kwa siku mbili hizi, [Machi 18 na 19], watu wengi wameondoka, tumebaki watu kama 120 hivi. Lakini muda mwingi tunacheza hapo 120 hadi 130. Wengi wamekimbia hali iliyoko pale [kambini].”

Mmoja kati ya vijana walioondoka kambini hapo ameiambia The Chanzo: “Mimi binafsi nimeondoka, kuna mambo yangu nimekuja kufuatilia. Unajua kipindi kile watu wengi tuliondoka kwa sababu hapakuwa panaeleweka hapo ila nitarudi muda si mrefu. Pale kambini kusema ukweli panaboa. Sasa ukae pale ufanye shughuli gani, sasa ukalime shamba la ushirika ambalo hujui hata utavuna nini?”

The Chanzo ilimuuliza Vumilia Zinkankuba, Mratibu wa Programu ya BBT, endapo kama taarifa za vijana kuondoka kambini hapo zina ukweli wowote, ambapo aliomba apewe kwanza chanzo cha taarifa hiyo ndiyo ajibu kama ni za kweli au la.

The Chanzo, hata hivyo, iligoma kufichua watoa taarifa wake kwani kufanya hivyo siyo tu kungewaweka hatarini bali pia ni kwenda kinyume na maadili ya uandishi wa habari yanayosisitiza umuhimu wa kuwaficha watoa taarifa.

The Chanzo
Sema zaidi ya UVCCM 100 waondoka mradi wa BBT, huu si walichukuliwa UVCCM nchi nzima?
 
Bashe ni mtu asiyejitambua mtu wa nadharia na si mtu wa vitendo! Anaacha kuchukua vijana wanaolima na wamezoea kilimo kama maisha yao anaenda kuchukua vijana wa Chuo kikuu! Pumbavu kabisa!
Kwanini nae hajaenda kukaa kambini na wale vijana hadi mradi ukomae???.

Ni sawa na hili suala la elimu kwa vijana wetu kwa sasa. Serikali imeamua kuwatengeneza Wajasiriamali kwa wingi badala ya Wataalam.
Wajasiriamali hawa watatofautiana kwenye viwango vya elimu. Yaani
1. Wale watakaohitimu elimu ya Msingi.
2. Wale watakaohitimu elimu ya Sekondari.
3. Wale.watakaohitimu vyuo mbali mbali kwa fani zisizokuwa na tija.
 
Wengi wamerudu na STD's na HIV.
 
Kwahyo hawafanyi lolote muda wote huo? waliwaita kabla hawajamaliza maandalizi kwanini? So walikuwa wanasosholaiziana tuu hapo hapo...majanga haya
 
Kwahyo hawafanyi lolote muda wote huo? waliwaita kabla hawajamaliza maandalizi kwanini? So walikuwa wanasosholaiziana tuu hapo hapo...majanga haya
Wame "sosholaizi"na kuchokana, sasa wanatafuta escaping way!
Kazi za manunguniko hazifiki mahali.
 
Huyu mradi ulianza Kwa mbwembwe ila hapa JF watu walitoa tahadhari wakakebehiwa. Naona Leo mambo yamebadilika.
 
Wanapenda kubet....kilimo na ufugaji sio kazi kwenda na kurudi na furushi la hela.
 
Back
Top Bottom