Tetesi: Zaidi ya wafanyakazi 600 yawakuta TPA......

Tetesi: Zaidi ya wafanyakazi 600 yawakuta TPA......

Acha tu mkuu japo sijakata tamaa lakini kuna mambo yanatakiwa angaliwa kwa jicho la huruma sana

Mpaka nilifika iyo hatua ni sababu naona kabisa kama jamaa watakuwa wanafanya michezo kichafu

Alafu cha kufurahisha zaidi unakuta wametangaza post watu 10 wanahitajika ukisoma status ya iyo nafasi unaambiwa mtu mmoja ameshaitwa kazini, ikabidi nianze fatilia status ya post mbali mbali nikaona kama vinavyoandikwa ni vile vile nikaanza ona kuna ujanja ujanja tu apa
 
Dah hapa undugu umetumika sana. Watakaojazana kwenye hizi nafasi ni ndugu walioshtuliwa na ndugu zao waliopo bandari.
Ila taasisi kubwa kama bandar ifanye hili jambo kwa siri kweli...?
Au ndio yale wameshaajiri watu kisirisiri alaf baadae ndio wanatangaza nafasi za kazi kisanii...? Huu si uhuni uliotukuka
Hapo ndo unakuta accountant mjomba, HR kaka, manager dingi, secretary Dada yani mpaka raha wote ofisi moja. Mkimaliza kazi mnajadili dinner itakuwa chakula yani home.
 
Hapo ndo unakuta accountant mjomba, HR kaka, manager dingi, secretary Dada yani mpaka raha wote ofisi moja. Mkimaliza kazi mnajadili dinner itakuwa chakula yani home.
Mpaka utoboe hapo.. Mungu anajua. Binafsi nilishawahi kufanya kazi kwenye kampuni moja. Si ya kiserikali.. ni binafsi. Kaka ndio director, manager mke, hr dada, accountant dada.

Yaaan ukimuudhi hata dada, au akakuchukia tu. Kesho huna kazi.
Ni moja ya kampuni zenye uongozi mbaya sana, niliwah kuwaonya kuhusu hilo.

Ndio ninachoona hapa, si kwamba watu hawana qualification, wanazo na zaid, ila uliritimba, undugu, kubebana..
 
Haya mambo yanaumiza sana ndugu zangu ujue tunaomba kazi kila siku tunakesha kwenye mitandao lakini hauitwi hata interview tu wakati huo huo wenzako wanapata kazi

Hapa ndio Huwa napata kigugumizi inamana mimi Sina vigezo kiasi hiki au kuna mahali nakosea

Kuna siku niliamua wasiliana Na wahusika CV people maana ninaomba sana kazi kwenye website yao lakini hata interview tu sijawahi itwa jamaa wakasema niwasiliane Na ofisi zao ambazo zipo dar es salaam, dah niliumia sana nikaamua achana tu na hili Jambo

Lakini kwa kweli waajiri mnatupa stress sana tuiteni tu hata interview kama tutakosa tukose huko mbele lakini sio kuwekana kindugu nafasi zinatangazwa alafu zinaishia juu juu

......
pole sana ndugu, tuko kwenye boat moja
 
Habari wakuu,

Kuna tetesi kuwa tarehe 29.05.2018 zaidi ya wafanyakazi 600 walio na vyeti feki wamepewa barua za kuachishwa kazi pasipo malipo yeyote kwani walikuwa wakiibia serikali hivyo hawastahili fidia.

Ili kuziba pengo lao, kuna tangazo lilitolewa watu wapeleke vyeti vyao, na watu wameshapeleka sasa wanasubiria tu kuitwa kwenye usahili,hivyo watakaobahatika kuajiriwa angalau na wao watapunguza machungu ya maisha.
Wawatimue na darasa la saba.
 
Huwa nafurahi sana taarifa za Mtumishi wa Umma kufukuzwa kazi. Mtu akiwa serikalini anajionaga mungu sana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jitahidi nawe uingie.
Kazi za serikalini hazina mwenyewe labda URAIS ndo wa WENYEWE CCM
 
kuna jamaa nilikuwa nimemkopesha million 2 nae katimuliwa ndio ishakula kwangu.
 
Hii habari ni ya ukweli, nathibitisha cz kuna ndugu yangu kapeleka vyeti vyake na walitoa ajira kimya kimya, ili watu wasijue, na ni nyingi sana,

Sasa kama wamewafukuza Watu Kazi kwa dhambi ya Kufoji Vyeti vyao je na Wao wanapoajiri Watu Kisirisiri hawaoni kuwa hata Wao wanatenda dhambi ile ile hivyo na Wao wanatakiwa ' Kujifukuza ' tu wenyewe?
 
Kwani mpaka leo ndani ya serikali kulikuwa na wenye vyeti feki??? au darasa la saba hao???
Nijuavyo kuna watu waliajiriwa serikalini kwa elimu ya msingi (darasa la saba) kuanzia mwaka 2004 hao ndio wanaotolewa.
 
Mpaka utoboe hapo.. Mungu anajua. Binafsi nilishawahi kufanya kazi kwenye kampuni moja. Si ya kiserikali.. ni binafsi. Kaka ndio director, manager mke, hr dada, accountant dada.

Yaaan ukimuudhi hata dada, au akakuchukia tu. Kesho huna kazi.
Ni moja ya kampuni zenye uongozi mbaya sana, niliwah kuwaonya kuhusu hilo.

Ndio ninachoona hapa, si kwamba watu hawana qualification, wanazo na zaid, ila uliritimba, undugu, kubebana..
yono auction mart nini?
 
Back
Top Bottom