Tetesi: Zaidi ya wafanyakazi 600 yawakuta TPA......

Tetesi: Zaidi ya wafanyakazi 600 yawakuta TPA......

Haya mambo yanaumiza sana ndugu zangu ujue tunaomba kazi kila siku tunakesha kwenye mitandao lakini hauitwi hata interview tu wakati huo huo wenzako wanapata kazi

Hapa ndio Huwa napata kigugumizi inamana mimi Sina vigezo kiasi hiki au kuna mahali nakosea

Kuna siku niliamua wasiliana Na wahusika CV people maana ninaomba sana kazi kwenye website yao lakini hata interview tu sijawahi itwa jamaa wakasema niwasiliane Na ofisi zao ambazo zipo dar es salaam, dah niliumia sana nikaamua achana tu na hili Jambo

Lakini kwa kweli waajiri mnatupa stress sana tuiteni tu hata interview kama tutakosa tukose huko mbele lakini sio kuwekana kindugu nafasi zinatangazwa alafu zinaishia juu juu

......

broo hii dunia wanaposemaga ni ya Mungu huwa sielewagi kabisa

Mungu atafanya njia
 
Hizo idara zilikuwa za ajabu kweli... jamaa akishika ubosi anaenda kukusanya ndugu zake kijijini na kuwachongeshea vyeti vya magumashi stationary.....sasa baba zao walishastaafu/kutumbuliwa....makaratasi hayo yanapelekwa necta hayasomi basi....ndio muda wa walalahoi walioumiza muda wao vyuoni sasa waonje matunda ya elimu yao
 
Mm nilipata tangazo muda ushaenda
IMG-20180528-WA0000.jpg
 
wabaki na makazi yao Sie wengine na BAF zetu ..kumbe tuliitwa kuwa wachungaji tumegundua
 
Hamna mkuu asemayo huyo jamaa ni kweli wqnaofanya kazi za maana serkalin wanajiona miungu watu
Mimi nayashangaa mabank eti hayatukopeshi sisi sekta binafsi eti hatuna security ya kazi, serikalini wana security ya kazi sasa kwa serikali hii mabank yameangukia PUA
 
hivi huko kweli kuna watu wenye weredi? walilenga watu wa Dar peke yao ,mtu wa ngara ,katavi ,songea anawezaje kuleta vyeti halisi ndan ya mda huo?
Zilikua na watu hizo hapo wanapiga mihuri tu;hii ndio bongo hauoni hapo kama walilenga ndani ya TPA na sio nje?
 
Ni hivi kama huna connection kupata kazi ni ngumu sana,hata huko nje kazi zinapatikana kwa ma agent.ukitaka kazi tafuta wa kukushika mkono
 
Katika hali hii unategemea kupata wafanyakazi wenye ufanisi..
 
*TANGAZO LA AJIRA**
Kama una Ndugu, Jamaa au Rafiki aliyesoma Chuo cha Bandari
Afike kesho 28/05/2018 asubuhi saa12 Ofisi za TPA (bandarini)
Kuna hitajika vijana/watu 500 kujaza nafasi za kazi ya Ukarani.
Pliz share this information

Tangazo lilikuwa simple yaani hivyo tu unalamba kazi.....
IMG-20180528-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom