Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 819
- 1,093
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TAKRIBANI watu milioni 1.5 kutoka Mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma na Lindi wanatarajia kunufaika na mradi wa unaolenga kuboresha matumizi ya endelevu ya ardhi na kukuza uchumi wa ndani (FORLAND) wenye thamani ya Euro milioni 20.
Mradi huo ambao wa miaka minne (2025-2029) unafadhiliwa na Serikali ya Finland, unalenga kuwawezesha wapandaji wa miti wadogo wadogo na jamii kwa ujumla kuendesha na kusimamia mashamba ya miti na hifadhi ya misitu na kilimo cha Miombo kupitia mbinu za usimamizi wa misitu kupitia ushirikishi wa jamii.
Akizungumza katika maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini Dodoma, Mratibu wa Mradi wa Taifa wa FORLAND, Emma Nzunda, alisema mradi huo unatokana na mafanikio ya Mpango Shirikishi wa Upandaji Misitu (PFP2) na Mpango wa Kukuza Misitu na Mnyororo wa Thamani (FORVAC).
Mipango hii imelenga kuunganisha mafanikio yaliyopatikana chini ya mipango ya awali kwa lengo la kuhakikisha uwekezaji katika sekta ya misitu ulio endelevu.
"Mradi huu haulengi tu usimamizi bora wa misitu lakini pia unaimarisha minyororo ya thamani-kusaidia jamii, wawekezaji kwenye mashamba ya miti, na wafanyabiashara wadogo na wa kati katika kuongeza thamani ya mazao ya misitu wanayozalisha”, alibainisha Nzunda.
Kwa mujibu wake, FORLAND inafungamana kwa karibu na vipaumbele vya maendeleo vya serikali ya Finland na Tanzania na inachangia katika kupunguza umaskini, kuzalisha ajira, na kuimarisha ustahimilivu wa hali ya hewa.
Miongoni mwa matokeo muhimu yanayotarajiwa kutokana na mradi huo ni pamoja na uboreshaji wa usimamizi wa mashamba ya miti ya wakulima wadogo wadogo, uimarishaji wa kitaasisi katika elimu ya misitu, na kuongezeka kwa mazungumzo kati ya wadau wa umma na binafsi ili kuboresha mazingira ya sera ya misitu.
"Mradi pia unalenga kuongeza uwezo wa wakulima wa miti na mashirika yao kusimamia mashamba kwa ufanisi zaidi na kupata mavuno bora," Nzunda alisisitiza.
Aliongeza kusema kuwa FORLAND pia inasaidia kuboresha utafiti wa misitu na kukuza utawala bora wa misitu kwa kuunganisha juhudi za jamii pamoja na malengo ya kitaifa na kimataifa ya sekta ya mazingira.
Alindelea kusema kuwa, kwa sasa, mradi unafanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Kituo cha Mafunzo ya Viwanda vya Misitu na Miti (FWITC) kilichopo Mafinga ili kuwajengea wanufaika wa mradi huo ujuzi na uelewa kuhusiana na dhana nzima ya mradi huo.
Kwa upande wake, mwakilishi wa FWITC George Charamila, alielezea umuhimu wa umma kupata elimu kuhusiana na mradi huo ili uwe endelevu.
"Tunahitaji kuongeza uelewa kuhusu mbegu bora za miti, usimamizi endelevu wa misitu, mipango ya matumizi mazuri ya ardhi na jinsi upandaji miti unavyoweza kuwa biashara yenye faida," alisema.
Akizungumzia baadhi ya changamoto kuhusiana na mradi huo Charamila alisema ni pamoja na dhama potofu iliyoenea ya kwamba kuna miti maalum kwa ajili ya kuzalisha Samani (fanicha) nzuri.
Akitolea mfano alisema, “Wengi wanaamini ya kuwa ni miti ya asili pekee ndiyo inaweza kutoa mbao za kutengenezea samani zenye ubora; dhana hii haina ukweli wowote kwa vile hata miti ya kisasa ambayo inakua haraka pia hutoa malighafi bora kwa ajili ya kutengenezea fanicha na bidhaa zingine za mbao”.
Mjumbe wa Chama cha Wakulima wa Miti Tanzania (TTGAU), Mary Uswege, alieleza kufurahishwa kwake mradi huo ambapo alisema umewaongezea wakulima wengi wa kiti maarifa kuhusiana na kilimo cha miti.
Aidha alisema mbali na faida zilizozoeleka za miti pia kumeibuka faida ingine mpya ambayo ni mapato yatokanayo na biashara ya hewa ukaa (Kaboni).
"Mashirika yanayojihusisha na maswala ya mazingira kutoka mataifa ya Magharibi sasa yananunua hewa ukaa; hii ina maana sasa mtu anaweza kungeza kipato kwa kupana miti mingi kuuza hewa ukaa hata kabla ya kuvuna mazao mengine kama vile mbao kwa ajili ya matumizi mbalimbali”, alisema.
Aliendelea kusema kuwa kadiri changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ikiendelea kuongezeka miradi kama FORLAND inakuwa na umuhimu wake katika kusaidia Tanzania kuweka uwiano kati ya uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya kiuchumi kwa kuhakikisha ya kuwa miradi ya misitu inaboresha maisha ya watu na kwa muda mrefu.