Zaka au sadaka ni hiari, kuwapigia simu waumini kuwakumbusha ni kuwalazimisha

Mkuu usiwe mbishi, siri ya utajiri ni kutoa sadaka kuanzia kina Mo na wengine, chunguza utajua ukweli.
 

Rejea comment hapo juu kutoa sio kupata MUNGU anazo sababu zingine nje ya kutoa Ili akubariki.
Baraka sio pesa pekee.
Shetani ni Mkuu wa ulimwengu huu kwasababu dunia ni makazi ya muda kwa shetani na mwanadamu.
Makazi ya umilele ni paradiso na jehanamu. Mungu ni mmiliki wa vyote yaani kuzimu, duniani, mbinguni, paradiso na jehanamu.
 
HUU NI UKWELI ASILIMIA 100.
 
Unaenda nje ya mada, hapa tunajadili utoaji wa zaka na sadaka kwa lazima huko makanisani. Unataka kuniambia hao wazungu wanaoleta misaada ya nguo na magari wanafanya hivyo kwa neema ya kutoa zaka na sadaka kwa nguvu!!?? Kwanza huko Ulaya na Marekani hayo mambo ya dini hayana nguvu kihivyo unavyodhani, wao wanaamini Mungu yupo ila aliwapa akili na ufahamu wa kuijenga leo na kesho yao bila kutegemea miujiza. Nyie mliofungwa ufahamu ndo mnaamini hamtafanikiwa bila kumkabidhi pesa zenu sheikh au mchungaji!
 
Kwani kuna miungu wangapi huko makanisani!? Nnavyojua mimi Mungu ni mmoja so tutayapima mafanikio ya kila mlokole kwa kuamini yanatoka kwa Mungu yuleyule anyewabariki wengine.
Kuna makanisa ya Mungu Jehovah na kuna makanisa ya shetani pia.
Kubarikiwa sio mali pekee ni zaidi ya hio
 
Mkuu usiwe mbishi, siri ya utajiri ni kutoa sadaka kuanzia kina Mo na wengine, chunguza utajua ukweli.
Sadaka unaitoa kwa nani? Sadaka kama ile ya Mengi ndo sadaka sahihi ila hapa tunapinga sadaka za kulazimishana, kupigiana simu kwa nguvu eti tupeleke kwa mchungaji! Sadaka zangu ninatoa na nitaendelea kutoa kwa wahitaji (yatima, wajane na wazee wasiojiweza) na ninaamini huko ndiko baraka zangu zilipo.
 

Ninekuambia watoaji wakubwa wote wako beyond hizo terminologies wanatoa kuliko hizo asilimia kumi za vitabuni walishavuka huko


Ibrahim utajiri wake haukuanzia kichwani kwake,Mungu ndie alianzisha,Yakobo utajiri wake haukuanzia kichwani kwake ulianzishwa na Mungu aliyempa siri ya kondoo kuzaliana bila kujamiiiana,Taifa la Israeli walikuwa maskini wa kutupwa watumwa kwa waarabu misri Mungu akawapa nchi na utajiri

Wewe wewe ni muamini sana akili zako
Biblia inatamka wazi

Mit 3:5-6​

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako


Pia inatamka Mungu ndie atoaye utajiri huamini basi baki hivyo


Kum 8:18​

Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Pia kuna utajiri wa aina mbili tofauti yake kubwa ni kudumu vizazi hadi vizazi Utajiri wa kupewa na shetani au wa kutegemea akili za kibinadamu tu huwa haudumu vizazi vingi Wa kupewa na Mungu hudumu vizazi vingi

Mit 8:18​

Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia.
 
Kunaa watu wana miaka na miaka wanamuomba Mungu wawe matajiri ila Mungu anasema NO.

Wakipata sana basi ni laki laki za kula tu ili wasife.

🥱😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Hakuna anayepinga zaka wala sadaka. Tunachopinga ni kupigiana sim kulazimishana kutoa. Wengine zaka na sadaka zetu huzipeleka kwa wahitaji moja kwa moja na si kanisani.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
Kanisa halina jeshi wala jela hakuna linalolazimisha Halina uwezo wa kukulazimisha kuwa muumini wala kukulazimisha kutoa
Kila jamii ina taratibu zake ukiona hukubaliani jiondokee tu nenda kaanzishe dini yako ambayo haikusanyi sadaka wala zaka

Tatizo kuna waleta fujo makanisani Kanisa lina utaratibu wake unasema sitaki mimi nitakuwa nafanya hivi si uende uanzishe kanisa lako liminal hayo unayoyaamini usiyokubaliana na hapo ulipo.? Au tafuta kanisa lenye misimamo kama yako badala ya kuleta vi imani vyako vya ajabu ajabu ambavyo hacienda na utaratibu uliopo hapo ulipo.

Ukiona una kiiimani chako kinatofautiana na jamii ulipo au kanisa ulipo.unaanza tukelele twa hiki sikubaliani ni wakati wako muafaka uhame au ukaanzishe kidini chako
 
Wewe siyo Mkristo ni Mnafiki ndiyo maana taratibu za kanisa lako Unaleta Jamiiforums.
Ukiwa mwanakanisa hai unajua kuwa kanisa linahitaji Nini kwa Sasa na inawezekana ulihaidi Mwenyewe Sasa Kama huna hela hiyo Mwambie huna.Acha kukashifu
 
Wewe siyo Mkristo ni Mnafiki ndiyo maana taratibu za kanisa lako Unaleta Jamiiforums.
Ukiwa mwanakanisa hai unajua kuwa kanisa linahitaji Nini kwa Sasa na inawezekana ulihaidi Mwenyewe Sasa Kama huna hela hiyo Mwambie huna.Acha kukashifu

Ni kweli unachoongea
Badala ya yeye kushinda humu anapinga kinachofanywa na kanisa lake ahame aende kwingine kwenye hiyo imani yake isiyoendana na kanisa alipo au kama haliko popote akaanzishe lake lisilokusanya sadaka au zaka au fungu la kumi full stop.

Viongozi wa dini ni wakati waanze kuwa wakali mtu anasema hiki sikubaliani aambiwe tu ondoka nenda huko.mnaoendana kiimani au kaanzishe dini yako
Watu wa aina hii wanaleta vurugu makanisani zisizo za lazima

Kanisa libaki tu na wale wakubaliana na kuendana taratibu za kanisa husika
 
 
Shida kubwa umekalili kuwa ucha Mungu ni kujitoa muhanga, kuuwa na kuwachukia watenda dhambi. Mungu alishatoka huko aliua sana na uovu haukuisha akaamua kujivika Rehema na Neema. Bwana Yesu alikuwa rafiki wa watenda dhambi na watoza ushuru.
 
Kondoo wa Bwana watalala njaa wewe ,😁
 
Luka 11:42
Lakini ole wenu Mafarisayo, kwa sababu mnatoa sehemu ya kumi ya mnanaa na mchicha na kila aina ya mboga, lakini mnapuuza haki na kumpenda Mungu! Mlipaswa kufanya mambo hayo, bila kupuuza yale mengine. 43 Ole wenu Mafarisayo,

Hilo hapo andiko la fungu la kumi katika agano jipya. Yesu anawaambia wasipuuze hayo mengine. Yaani sehemu za kumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…