Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Kwenye hizi mambo ya imani kumejaa utapeli mtupu, mtu anachukua mkopo benki baba yake wa kiroho anamwambia toa fungu la kumi kwa ajili ya ulinzi wa huo mkopo[emoji1664]
Sasa mkopo ni pesa yako [emoji1787][emoji1787][emoji1787] zaka ilikuwa inatolewa kwa vile vilivyo vyako.kutoa mkopo zaka ni sawa sawa na umeajiliwa kuchunga ng'ombe mia wa tajiri yako wewe uchukue ng'ombe 10 wa tajiri na kuwatoa zaka kisha unasema hiyo ni zaka yako[emoji23][emoji23]
 
Kwenye hizi mambo ya imani kumejaa utapeli mtupu, mtu anachukua mkopo benki baba yake wa kiroho anamwambia toa fungu la kumi kwa ajili ya ulinzi wa huo mkopo🦍
Hiyo tayari imeshakuwa hasara. Kisa baba wa kiroho,tena hapo hapo nyumbani unga unabaki robo. Jama anakata tena kidogo anampa. Tena waliomuombea kupata huo mkopo,anaambiwa lazima washikwe mkono. Sasa kwenye kurudisha ameshindwa,nyumba yake(kama anayo),inapigwa mnada,baba wa kiroho anamuombea ajikaze tu kiume,kwamba yeye si wa kwanza wala wa mwisho.
 
Hahhaaha huo ni utapeli mkuu Kumnyang'anya mtu
 
Safi sana! Mkuu itoshe kusema Kuna baadhi ya maeneo nakubaliana na wewe kabisa
 
Kanisa limechukua nafasi ya hekalu.
Hahaha kanisani haliwezi kuchukua nafasi ya hekalu...
Labda kama ungeniambia Kanisa limechukua Nafasi ya Sinagogi...
Mkuu nenda kwanza kasome nini maana ya Hekalu na kazi zake na nini maana ya Synagogue na kazi zake..
Vinginevyo utakuwa unatumia hisia kujibu..
 
Peleka kwenye Kanisa linalohubiri sana habari za dhambi na kuishi maisha mema. Ukiona kanisa sijui inahubiri upate gari au nyumba, achana nalo
Vipi kule wanatangaza kiasi kinachokusanywa kila jumapili?
Vipi waumini huwa wanajulishwa matumizi ya Zaka hizo?
 
Malaki alikuwa nabii wa Mungu wa miungu yote duniani.
Mahali hapo ulipo, mchungaji wako anasema, Hatutoi zaka ili tubarikiwe bali tunalipa!
Vipi unalinganishaje hiyo Malaki na anachosema Mchungaji wako?
 
Mkuu uko sawa!
Mtume Paulo alifanyakazi za mikono ili ajikimu! Alikuwa Fundi wa kushona Mahema.
Lakini Wachungaji wa Nyakati zetu ni kubanana waumini.
Achilia mbali muumini anatoa zaka, lakini ataambiwa atoe sadaka ya kumtegemeza Mchungaji!
 
Hata Hekalu ni Mwili wa Kristo ambao ni sisi Wakristo,(1Wakorintho6:18-19)
Kwa hiyo Hekalu na Kanisa tafsiri yake ni moja.
Kuna Jengo la Hekalu au Jengo la Kanisa, lakini kuna Hekalu au Kanisa ambalo ni sisi Wakristo, Matendo2:47
Hekalu ni Jengo na Kanisa ni mwili wa Kristo
 
Yesu Kristo alishajitoa Sadaka hivyo mambo ya Zaka, Fungu la 10 nk alishazitamatisha

Fungu la 10 wanatoa Majamatini kwa wahindi
 
Tofautisha msaada na fungu la 10%.

Pia elewa msaada hauchagui wa kunugaika lakini fungu la 10%,zaka,sadaka,harambee,nk ni wizi na wanaonufaika ni maaskofu na wachungaji kwa kula vzr,magari,ndege,pombe,majumba,nk

Hili haliondoi muongozo wa fungu la 10,hutolewa madhabahuni tu na si kwengineko,tafuta kanisa imara upeleke zaka.
 
Mkuu uko sawa!
Mtume Paulo alifanyakazi za mikono ili ajikimu! Alikuwa Fundi wa kushona Mahema.
Lakini Wachungaji wa Nyakati zetu ni kubanana waumini.
Achilia mbali muumini anatoa zaka, lakini ataambiwa atoe sadaka ya kumtegemeza Mchungaji!
Yesu mwenyewe hakuwa na hayo mambo ya kubana watu. Yeye ndo alilisha watu 5000 lakini siku hizi watu 5000 wanamlisha mtu mmoja. Kwa wasiojua ni kuwa wachungaji wa sasa wanapiga dili nyingi sana chafu na safi.
 
Tatizo lako unatumia tafsiri za kale za Kiyahudi ndio maana hatuelewani.

Isitoshe 'kiroho' hata mwili wa mtu pia ni hekalu.

Agano la kale hekalu lilikuwa ni jengo ila kwa sasa hekalu linaweza kuwa jengo (Kanisa) au mwili.

1 Wakorintho 3:16
Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
 
Unataka kusema mtaji Mungu hakuwezeshi au?
Maandiko yote uliyoyatoa ukiyaangalia kwa kina yanagusia vyote mfano angalia maneno haya " fungu la kumi la vitu vyote" Je? mtaji haupo kwenye vitu vyote?...

Kama fungu la kumi ni ulinzi wa mapato yetu je? tunapaswa kulinda faida tu na siyo mtaji?.. Haya masuala yanahitaji uelewa mpana sana kiroho siyo kiuchumi tu. Je? faida tu ndiyo inayohitaji baraka za Mungu na ulinzi na siyo mtaji?.
Kuna mahali hatujaelewa



 
Tuambie sasa alichomaanisha Yesu na tuonyeshe kwa andiko Yesu alipokiri anaijua siku ya kiama.
 
Tuambie sasa alichomaanisha Yesu na tuonyeshe kwa andiko Yesu alipokiri anaijua siku ya kiama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…