Zakazakazi: Yanga sio Mabingwa mara 29 na Simba sio Mabingwa mara 22

Naye data zake zina walakini. Mbona hajaitaja MTIBWA SUGAR ambayo ilichukua ubingwa mara 2 mfululizo 1999 na 2000?
soma post zote za zakazakazi ameongelea hizo data,
jamaa kaanika ukweli wote, simba na yanga walikua wanatudanganya!
 
Anaandika Zakazakazi,

YANGA SIYO MABINGWA MARA 29 NA SIMBA SIYO MABINGWA MARA 22

Hii ni changamoto kwa wadau wote wa soka nchini Tanzania; wachambuzi, waandishi wa habari, mamlaka za soka na serikali kwa maana ya wizara ya michezo na baraza la michezo.

Fanyeni utafiti na mje na majibu sahihi maana siku zinavyozidi kwenda, uongo unakuwa ukweli kwa sababu watu wanaamini yasiyo sahihi.

Ligi ya Tanzania ilianza mwaka 1965 ikiitwa Klabu Bingwa ya Taifa. Hadi mwaka huu, 2023, ni miaka 58. Maana yake kuna mabingwa 58 wanatakiwa kuwepo.

Sasa kama Yanga ni mabingwa mara 29, Simba mara 22 maana yake hawa wawili peke yao wamechukua ubingwa mara 51.

Katika misimu 58, imebaki misimu 7 pekee ambayo wamechukua wengine.

Hao wengine ni wafuatao.

Cosmopolitan -1 (1967)
Mseto -1 (1975)
Pan African - 1 (1982)
KMKM - 1 (1984)
Majimaji - 3 (1985, 1986 na 1998)
African Sports - 1 (1988)
Malindi - 2 (1989 na 1992)
Pamba - 1 (1990)
TZ Prisons - 1 (1999)
Azam FC - 1 (2014)

Jumla 13

Ukijumlisha na zile 51 za Yanga na Simba, unapata 64...inawezekanaje?

Ligi iliyochezwa miaka 58 inakuwaje na mabingwa 64...hesabu za wapi hizo?

Timu zilizotajwa hapo ndiyo mabingwa wa Tanzania wanaotambuliwa na CAF na FIFA, na ndiyo walioshiriki Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka husika.

Ndiyo maana nilianza kwa kutoa changamoto kwa wadau.

Tembeleeni tovuti za CAF na FIFA muone ni timu zipi ziliiwakilisha Tanzania kwenye Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia 1965.

UKWELI
Yanga ni mabingwa mara 22 na Simba mara 21.

22+21= 43 - Yanga na Simba
43+13=56 - Jumla (kati ya 58)

NB: Kuna misimu miwili (1970 na 2003) Tanzania hakukuwa na bingwa.

Ndiyo maana unapata mabingwa 56 katika misimu 58.

Itaendelea...

Soma sehemu ya pili hapa

Soma sehemu ya tatu hapa

Soma sehemu ya nne hapa

Soma sehemu ya tano hapa

Soma sehemu ya sita hapa

Soma sehemu ya saba hapa

Soma sehemu ya nane hapa

Soma sehemu ya tisa hapa
Kama ligi ilianza 1965, na FAT ilianzishwa 1945, hii miaka 20 FAT (TFF) ilikuwa inasimamia UMISETA??

Acheni kujiumiza ili tu kutaka kudogosha takwimu za Yanga. Aliye juu yupo juu tu ndugu.
Screenshot_20230623-142446_Chrome.jpg
 
Kama ligi ilianza 1965, na FAT ilianzishwa 1945, hii miaka 20 FAT (TFF) ilikuwa inasimamia UMISETA??

Acheni kujiumiza ili tu kutaka kudogosha takwimu za Yanga. Aliye juu yupo juu tu ndugu.View attachment 2666381
Kwanza FAT ilianzishwa mwaka 1930 lakini haikuwa rasmi

Rasmi imekuja kutambulika na FIFA mwaka 1965

Ni sawa na Yanga ukisoma historia ilianzishwa mwaka 1920s huko, lakini ilianza kutambuliwa rasmi mwaka 1935.

Na hata hayo mashindano unayosema mengi hayakuwa rasmi yalikuwa ni local, mengine yalikuwa ni ligi za Dar Es Salaam tu hapa ambazo ushindi wake watu wa.ejihesabia kwenye ligi ya bara.

Pia kuna mashindano yaliyohusisha timu za Visiwani ambapo hayo mashindano hayaana vigezo vya kusema ni ligi ya bara.

Soma sehemu ya tatu utawekewa vizuri
 
Hio ya FAT kuanzishwa 1930 umeitoa wapi? mbona kwenye history inasema 1945
 
Hii topic ina complications nyingi kila source ina data zake hapa inaonekana Yanga ana makombe 28
IMG_20230623_171744.jpg
 
Nilishakosa Imani na baadhi ya mashabiki wa Jf acha tu nikae kimya.
 
Zakazakazi awapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa 23 wa ligi kuu

Full interview
 
Anaandika Zakazakazi,

YANGA SIYO MABINGWA MARA 29 NA SIMBA SIYO MABINGWA MARA 22

Hii ni changamoto kwa wadau wote wa soka nchini Tanzania; wachambuzi, waandishi wa habari, mamlaka za soka na serikali kwa maana ya wizara ya michezo na baraza la michezo.

Fanyeni utafiti na mje na majibu sahihi maana siku zinavyozidi kwenda, uongo unakuwa ukweli kwa sababu watu wanaamini yasiyo sahihi.

Ligi ya Tanzania ilianza mwaka 1965 ikiitwa Klabu Bingwa ya Taifa. Hadi mwaka huu, 2023, ni miaka 58. Maana yake kuna mabingwa 58 wanatakiwa kuwepo.

Sasa kama Yanga ni mabingwa mara 29, Simba mara 22 maana yake hawa wawili peke yao wamechukua ubingwa mara 51.

Katika misimu 58, imebaki misimu 7 pekee ambayo wamechukua wengine.

Hao wengine ni wafuatao.

Cosmopolitan -1 (1967)
Mseto -1 (1975)
Pan African - 1 (1982)
KMKM - 1 (1984)
Majimaji - 3 (1985, 1986 na 1998)
African Sports - 1 (1988)
Malindi - 2 (1989 na 1992)
Pamba - 1 (1990)
TZ Prisons - 1 (1999)
Azam FC - 1 (2014)

Jumla 13

Ukijumlisha na zile 51 za Yanga na Simba, unapata 64...inawezekanaje?

Ligi iliyochezwa miaka 58 inakuwaje na mabingwa 64...hesabu za wapi hizo?

Timu zilizotajwa hapo ndiyo mabingwa wa Tanzania wanaotambuliwa na CAF na FIFA, na ndiyo walioshiriki Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka husika.

Ndiyo maana nilianza kwa kutoa changamoto kwa wadau.

Tembeleeni tovuti za CAF na FIFA muone ni timu zipi ziliiwakilisha Tanzania kwenye Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia 1965.

UKWELI
Yanga ni mabingwa mara 22 na Simba mara 21.

22+21= 43 - Yanga na Simba
43+13=56 - Jumla (kati ya 58)

NB: Kuna misimu miwili (1970 na 2003) Tanzania hakukuwa na bingwa.

Ndiyo maana unapata mabingwa 56 katika misimu 58.

Itaendelea...

Soma sehemu ya pili hapa

Soma sehemu ya tatu hapa

Soma sehemu ya nne hapa

Soma sehemu ya tano hapa

Soma sehemu ya sita hapa

Soma sehemu ya saba hapa

Soma sehemu ya nane hapa

Soma sehemu ya tisa hapa
Huu ni msongo wa mawazo
 
Muulizeni Zaka Za Kazi.

Kama Ligi Kuu ilianzishwa mwaka 1965,

Je Yanga SC (iliyo anzishwa mwaka 1935) na
Simba SC (iliyo anzishwa mwaka 1936)..zilikuwa zina fanyanini wakati wote huo wa miaka 30?

Jibu langu:-

Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania lilikuwa affiliated na CAF kuanzia mwaka 1965.

Ndipo hapo Shirikisho la soka Tanzania likaanza kujitambua kama siku yake ya kuzali.

Lakini lilikuwa likifanya kazi tangu hapo awali basi nankutotambulika kihalali kama mashirika ya soka mengine ya ulimwengu.
Kabla ya 1965 zilikuwa ni ndondo tu
 
Poleni wote wenye kupitia maumivu makali . Wazee wa kutafuta history iwapunguzie maumivu. Wazee wa kupingana na ukweli. Endeleeni kujichelewesha.
.
Muhimu kwa sasa mpambanieni fei kiatu. Hiyo nyingine imeisha. Itaanza ligi mtanung'unika tena baada ya YANGA kuchukua tena
Haujagusa hoja

Ni kwasababu hauwezi kui refute kwakua ni kweli.
 
Back
Top Bottom