View attachment 2662353KWAKO MCHAMBUZI MKUBWA MWAISABULA - 4
Bosi wangu @mwaisabula_mzazi, ligi yetu imepitia mabadiliko mengi sana ya kimuundo, mfumo na majina, hadi kufika hapa ilipo leo.
Mabadiliko makubwa yalifanyika katika awamu tatu, lakini hata hivyo hadhi ilibaki kuwa ile ile kwamba bingwa wa ligi hii ndiyo bingwa wa nchi na anawakilisha Tanzania kimataifa.
AWAMU YA KWANZA
Ule wakati ambao ligi ilikuwa ikiitwa mashindano ya kutafuta klabu bingwa ya taifa, yaani kuanzia 1965 hadi 1981.
Mengi kuhusu awamu hii nimeshayaelezea sana huko nyuma.
AWAMU YA PILI
Hii ilikuwa kuanzia 1982 hadi 2003. Nimeweka kipande cha andiko linaloelezea kwa kina msimu huo.
FAT ilibadilisha mfumo na muundo wa ligi ya zamani na kuja na mfumo na muundo mpya.
Mabadiliko hayo pia yalihusu jina, kutoka Klabu Bingwa ya Taifa hadi Union Super League, yaani Ligi Kuu ya Muungano.
Bingwa wa Ligi hii alikuwa sawa na bingwa wa ile ligi ya zamani, na alienda kushiriki mashindano ya Afrika.
Mabingwa
Pan African (1)
Yanga (6)
KMKM (1)
Simba (5)
Majimaji (3)
African Sports (1)
Malindi (2)
Pamba (1)
NB:Mwaka 2003 hakukuwa na bingwa kwa sababu ligi ilivunjika.
Katika awamu hii pia zilianzishwa ligi zingine mbili; Ligi ya Bara na Ligi ya Zanzibar.
Kwa hiyo kaka yangu Mzazi, ile ligi ya bara uliyosema mimi siijui, ndiyo nakuelezea kwamba ilianzia hapa.
Ligi ya bara ilishirikisha timu za bara pekee, na ilikuwa ya madaraja, kuanzia la kwanza hadi la nne.
Lengo la ligi hii ilikuwa kupata timu zitakazoenda kushiriki Ligi Kuu ya Tanzania, ambayo iliitwa Union Super League.
Kwa hiyo ligi ya bara ilikuwa sehemu ya ligi kuu ya Tanzania...Ligi ya Muungano!
Mwaka 1997 ligi ya bara ikafanyiwa mabadiliko kufuatia udhamini mnono wa Safari Lager.
Zile timu zilizokuwa daraja la kwanza zikapandishwa hadhi na kuwa Ligi Kuu...ndipo ikaanza Safari Lager Premier League!
Mabingwa wa Bara
Yanga (11)
Simba (6)
Mtibwa Sugar (2)
Coastal Union (1)
Tukuyu Stars (1)
Hii haikuwa ligi rasmi na ndiyo maana mabingwa hawa hawakupata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka hiyo!
Itaendelea....