Akitumia takwimu za walioshiriki Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika pekee anaweza kuwa anakosea. Nafikiri kuna wakati aliyekuwa anashiriki Klabu Bingwa ni aliyechukua Kombe la Muungano, kama sikosei kwa hiyo hapo tayari Bingwa wa Tanzania Bara alikuwa amepatikana, unless hakuwa anatambulika kama bingwa. Ila aangalie na hizo data na taratibu za kipindi kile za kupata mabingwa. Yanga wana tabia za kupotosha kwa hiyo sitashangaa kama na hili wamelilazimisha.
Ila ningependa Yanga wakumbushwe kuwa hadi mashindano ya CECAFA level ya vilabu yanasitishwa, Simba ndiyo anashikilia rekodi ya kulichukua mara nyingi.