changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Mapinduzi haitwi ligi ya muungano bali inaitwa kombe la mapinduzi, ile ilikuwa ni ligi ya Tanzania bara hivyo ni tofauti na bonanzaSasa hii si kama Mapinduzi tu ambayo saizi inaitwa Bonanza?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mapinduzi haitwi ligi ya muungano bali inaitwa kombe la mapinduzi, ile ilikuwa ni ligi ya Tanzania bara hivyo ni tofauti na bonanzaSasa hii si kama Mapinduzi tu ambayo saizi inaitwa Bonanza?
Sasa angalia hiyo First Division ilianzishwa mwaka 1888, Man U ilianzishwa mwaka 1878
Mpaka hapo hoja yako ni flawed
Huwezi kuleta mashindano ya ndondo ukayaita ubingwa wa Tanzania64 - 65 ni kwamba ligi ilirasimishwa na bingwa wa kwanza akawa Sunderland...
Kabla ya hapo ligi ilikuwa ikichezwa pasipo urasmi na mabingwa walikiwa wakipatikana...
Jaribu tu kujiuliza timu za Simba na Yanga zilizoanzishwa miaka ya 30, je zilikuwa zipo zipo tu hadi huo mwaka 64/65?
mtibwa hajawekwa, kwa kumbukumbu zangu amewahi kuwa bingwa miaka ya kati ya 2000-2010 hapa, sikumbuki vizuri mwakaAnaandika Zakazakazi,
YANGA SIYO MABINGWA MARA 29 NA SIMBA SIYO MABINGWA MARA 22
Hii ni changamoto kwa wadau wote wa soka nchini Tanzania; wachambuzi, waandishi wa habari, mamlaka za soka na serikali kwa maana ya wizara ya michezo na baraza la michezo.
Fanyeni utafiti na mje na majibu sahihi maana siku zinavyozidi kwenda, uongo unakuwa ukweli kwa sababu watu wanaamini yasiyo sahihi.
Ligi ya Tanzania ilianza mwaka 1965 ikiitwa Klabu Bingwa ya Taifa. Hadi mwaka huu, 2023, ni miaka 58. Maana yake kuna mabingwa 58 wanatakiwa kuwepo.
Sasa kama Yanga ni mabingwa mara 29, Simba mara 22 maana yake hawa wawili peke yao wamechukua ubingwa mara 51.
Katika misimu 58, imebaki misimu 7 pekee ambayo wamechukua wengine.
Hao wengine ni wafuatao.
Cosmopolitan -1 (1967)
Mseto -1 (1975)
Pan African - 1 (1982)
KMKM - 1 (1984)
Majimaji - 3 (1985, 1986 na 1998)
African Sports - 1 (1988)
Malindi - 2 (1989 na 1992)
Pamba - 1 (1990)
TZ Prisons - 1 (1999)
Azam FC - 1 (2014)
Jumla 13
Ukijumlisha na zile 51 za Yanga na Simba, unapata 64...inawezekanaje?
Ligi iliyochezwa miaka 58 inakuwaje na mabingwa 64...hesabu za wapi hizo?
Timu zilizotajwa hapo ndiyo mabingwa wa Tanzania wanaotambuliwa na CAF na FIFA, na ndiyo walioshiriki Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka husika.
Ndiyo maana nilianza kwa kutoa changamoto kwa wadau.
Tembeleeni tovuti za CAF na FIFA muone ni timu zipi ziliiwakilisha Tanzania kwenye Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia 1965.
UKWELI
Yanga ni mabingwa mara 22 na Simba mara 21.
22+21= 43 - Yanga na Simba
43+13=56 - Jumla (kati ya 58)
NB: Kuna misimu miwili (1970 na 2003) Tanzania hakukuwa na bingwa.
Ndiyo maana unapata mabingwa 56 katika misimu 58.
Itaendelea...
Soma Hapa sehemu ya pili >>>>>> Sehemu ya pili
Kulikuwa na ndondo cupKwanza hizo takwimu Tu zina makosa kama ulivotaja.. Tukuyu stars na mtibwa hazijaorodheshwa ina maana tayari hoja yake haijitoshelezi lakini pia Yanga na Simba zimeanza miaka ya 1930's je, hiyo miaka hakukua na ligi Hadi huo mwaka 1965?? Tuanzie hapo.. kama hakukua na ligi Sawa lakini kama zilikuepo basi zaka anataka kutupotezea muda
Arsenal Unbeaten yake unadhani hakufungwa mashindano mengine? Unajizima data au sio?Unajua kwenye masuala ya takwimu ukiwa mjanja unaweza kuzitumia unavyotaka wewe kwa manufaa yako na kwa kiasi fulani ukawa sahihi ingawa ndani yake umefanya udanganyifu kwa kuacha data fulani.
Kipindi kile Yanga wanajigamba kwa rekodi za unbeaten, walipokumbushwa mbona mmefungwa mashindnao ya CAF, piw na Vipers, wakasema ooh tunahesabu mashindano ya ndani tu.
Kuna msemo mmoja kuhusu takwimu nikiukumbuka nitauleta.
Akiambiwa ana panicArsenal Unbeaten yake unadhani hakufungwa mashindano mengine? Unajizima data au sio?
We unazungumzia 1990-91 wakati kuna existence ya Club miaka ya 1860s?MFANO KUTOKA ULAYA
Una maanisha msimu wa 1990-91 wa First League Division wa nchini Uingereza ni sawa na Ndondo za mtaani?
Hii hapa ni team squad ya Liverpool ya msimu 1990-91 kabla ya Ligi kuitwa EPL.
View attachment 2658275
ilkua inaitwa 8 bora, timu 4 za bara na 4 za zenji....... ligi ya muungano!Coastal Union pia hayupo.
Hivyo Zakazakazi hana data kamili.
Ushindi unaotajwa hauhusishi timu za Zenji.
Wakati ule mabingwa wa bara walikuwa wakicheza na mabingwa wa Zenj Sidhani kama ilikuwa ligi.
Nikumbusheni.
Na Simba kachukua Muungano mara ngapi?Yanga imechukua kombe la muungano mara 6 na katika hizo mara sita ni mara moja pekee ndio kawa bingwa wa kombe la muungano pasipo kuchukua kombe la Tanzania bara (mwaka 2000) ila mara tano zote kabeba makombe mawili kwa pamoja. Hivyo kwenye takwimu zao zina makombe mawili kwa pamoja pia
Jamani wkt mwingine tutumie akili kidogo. Siyo kila jambo unaletewa hapa na unskubali tu. Hivi toka lini Kmkm na Malindi walishiriki liigi ya tz bara? Ni lini African sport alikuwa bingwa? Ina maana Coastal union na Mtibwa sugar hawajawahi kuwa mabingwa wa ligi yetu?. Upuuzi mwingine msiwe mnaupost hapa maana mnajiaibisha. Kiufupi hii taarifa ni full upotoshaji.Nakumbuka hii kitu Yanga sio Mabingwa wa kihistoria aliwahi kuelezea Venus Star lakini watu walibisha kwa mapenzi ya timu.
Ngoja tuone kama kuna watu wataojitokeza kum challenge Zakazakazi kisha tuone hoja zao ni zipi.
MISIMU MIWILI HAKUKUWA NA BINGWA
Kuna misimu miwili Tanzania haikuwa na bingwa rasmi kutokana na sababu tofauti...mwaka 1970 na mwaka 2003.
1970
Mwaka 1970 ligi haikufanyika kabisa kwa sababu timu nyingi ziligomea kushiriki, zikiongozwa na Yanga na Sunderland (Simba).
Mwaka huo FAT iliruhusu timu nyingi za mashirika kushiriki ligi. Wachezaji wa Yanga na Sunderland walikuwa wanafanya kazi kwenye hayo mashirika(ikiwemo Bandari na Cargo).
Kwa hiyo hayo mashirika yakazuia wafanyakazi wao kuchezea timu za mtaani ili wachezee timu zao za kazini.
Yanga na Sunderland zikakosa wachezaji, zikajitoa kwenye ligi...na ligi haikufanyika.
FAT ikaichagua Yanga ishiriki klabu bingwa Afrika mwaka 1971, kwa sababu walikuwa mabingwa wa msimu uliopita. Yanga wakajihesabia kupewa na ubingwa...lakini walipewa tiketi tu!
2003
Mwaka huu Ligi ya Muungano ambayo ndiyo ilikuwa ligi kuu ya Tanzania, haikumalizika baada ya Yanga kufungua kesi mahakama ya Ilala kupinga ligi kuchezwa kwa mtoano.
Yanga walipangwa kucheza na Jamhuri ya Pemba, na wakatoka Dar Es Salaam kuelekea Pemba. Kufika Unguja wakagoma kwenda Pemba wakisema wamegundua ligi huwa haichezwi kwa mtoano.
FAT na ZFA kama waandaaji wa ligi ya Muungano wakaitoa Yanga na kuipa ushindi Jamhuri. Yanga wakaenda mahakamani kupinga kutolewa.
Mahakama ikasimamisha ligi na kupanga kusikiliza kesi Februari 2004.
Ligi ikasimama na FAT na ZFA wakaipa Simba tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mwaka 2004.
Simba wakajitangazia kupewa na ubingwa...lakini haikuwa hivyo, walipewa tiketi tu.
Mara hizo mbili, ndizo zinafanya hesabu iwe 58 lakini mabingwa halisi ni 56.
Itaendelea...
2003 Bingwa Tanzania bara alikuwa Simba, ilikuwa 8 Bora nakumbuka kabisa. Aache ujinga wake huyo ZakazakaziMISIMU MIWILI HAKUKUWA NA BINGWA

Onyesha ligi ambayo ilikuwa rasmi miaka ya 1860 huko ambapo Notts County ilianzishwa.View attachment 2658311View attachment 2658312
Kwa Mujibu wa ZAKAZAKAZI basi Manchester Utd amebeba ndoo mara 13 tu kwasababu ligi imeanza mwaka 1992. Na misimu ya nyuma huko hakukuwa na ligi bali ni Ndondo cup, Gombania goli na Mechi za kirafiki.
Jamani tutumie akili zetu vizuri.
kwaio kwenye 29 kuna 6 ya muungano na 5 ya bara waliyochukia kwa misimu hio 6 (yani makombe 11 ya ligi ndani ya misimu 6 sio?)Yanga imechukua kombe la muungano mara 6 na katika hizo mara sita ni mara moja pekee ndio kawa bingwa wa kombe la muungano pasipo kuchukua kombe la Tanzania bara (mwaka 2000) ila mara tano zote kabeba makombe mawili kwa pamoja. Hivyo kwenye takwimu zao zina makombe mawili kwa pamoja pia
Zaka za Kazi anajidhalilisha bure, takwimu ziko sahihi, ila alivyo pimbi anakokotoa mabingwa kama calculus. Anachanganya mabingwa wa Bara na Muungano, atuambie ni mwaka gani Malindi ilishiriki ligi ya Bara umbwa huyu. TFF na ujinga wao hawawezi kuwa wajinga kwa kiwango cha Zakazi, wangeshachalenjiwa kitambo sana hii issue. Rekodi zipo na wakongwe waliokuwepo wapo pia, mbwiga wa mbwiga huyu.Anaandika Zakazakazi,
YANGA SIYO MABINGWA MARA 29 NA SIMBA SIYO MABINGWA MARA 22
Hii ni changamoto kwa wadau wote wa soka nchini Tanzania; wachambuzi, waandishi wa habari, mamlaka za soka na serikali kwa maana ya wizara ya michezo na baraza la michezo.
Fanyeni utafiti na mje na majibu sahihi maana siku zinavyozidi kwenda, uongo unakuwa ukweli kwa sababu watu wanaamini yasiyo sahihi.
Ligi ya Tanzania ilianza mwaka 1965 ikiitwa Klabu Bingwa ya Taifa. Hadi mwaka huu, 2023, ni miaka 58. Maana yake kuna mabingwa 58 wanatakiwa kuwepo.
Sasa kama Yanga ni mabingwa mara 29, Simba mara 22 maana yake hawa wawili peke yao wamechukua ubingwa mara 51.
Katika misimu 58, imebaki misimu 7 pekee ambayo wamechukua wengine.
Hao wengine ni wafuatao.
Cosmopolitan -1 (1967)
Mseto -1 (1975)
Pan African - 1 (1982)
KMKM - 1 (1984)
Majimaji - 3 (1985, 1986 na 1998)
African Sports - 1 (1988)
Malindi - 2 (1989 na 1992)
Pamba - 1 (1990)
TZ Prisons - 1 (1999)
Azam FC - 1 (2014)
Jumla 13
Ukijumlisha na zile 51 za Yanga na Simba, unapata 64...inawezekanaje?
Ligi iliyochezwa miaka 58 inakuwaje na mabingwa 64...hesabu za wapi hizo?
Timu zilizotajwa hapo ndiyo mabingwa wa Tanzania wanaotambuliwa na CAF na FIFA, na ndiyo walioshiriki Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika katika miaka husika.
Ndiyo maana nilianza kwa kutoa changamoto kwa wadau.
Tembeleeni tovuti za CAF na FIFA muone ni timu zipi ziliiwakilisha Tanzania kwenye Klabu Bingwa/Ligi ya Mabingwa Afrika kuanzia 1965.
UKWELI
Yanga ni mabingwa mara 22 na Simba mara 21.
22+21= 43 - Yanga na Simba
43+13=56 - Jumla (kati ya 58)
NB: Kuna misimu miwili (1970 na 2003) Tanzania hakukuwa na bingwa.
Ndiyo maana unapata mabingwa 56 katika misimu 58.
Itaendelea...
Soma Hapa sehemu ya pili >>>>>> Sehemu ya pili
mkuu kuwa mtulivu na uitazame hoja ya Zakazi kwa umakini, anayo hoja ila inawezekana kaiwasilisha kimakosa!View attachment 2658311View attachment 2658312