Zakazakazi: Yanga sio Mabingwa mara 29 na Simba sio Mabingwa mara 22

Kama kombe la Abiora?
 
TFF waoga sana wanajua hii kitu itavyokuja kuleta ugomvi
Unajua kwenye masuala ya takwimu ukiwa mjanja unaweza kuzitumia unavyotaka wewe kwa manufaa yako na kwa kiasi fulani ukawa sahihi ingawa ndani yake umefanya udanganyifu kwa kuacha data fulani.

Kipindi kile Yanga wanajigamba kwa rekodi za unbeaten, walipokumbushwa mbona mmefungwa mashindnao ya CAF, piw na Vipers, wakasema ooh tunahesabu mashindano ya ndani tu.

Kuna msemo mmoja kuhusu takwimu nikiukumbuka nitauleta.
 
Tupe mfano.

Mwaka upi kulikuwa kunachezwa ligi mbili kwa wakati mmoja?

Yaani Ligi ya Bara na Muungano.
 
Hapo kwenye list ya mabingwa ya Zakazakazi kuna Tukuyu stars na Mtibwa ambao wamesahaulika
Coastal Union pia hayupo.
Hivyo Zakazakazi hana data kamili.
Ushindi unaotajwa hauhusishi timu za Zenji.
Wakati ule mabingwa wa bara walikuwa wakicheza na mabingwa wa Zenj Sidhani kama ilikuwa ligi.
Nikumbusheni.
 
Ndio ujue anaokoteza tu ili kuwafanya mikia angalau mupate cha kuegemea na kushangilia mwaka huu
The more we get, the more you lose.

Kadri tunavyozidi kuwakumbuka mabingwa wengine ambao tuliwasahau kwenye list ndivyo inavyozidi kupungua nafasi ya Yanga kumiliki makombe mengi
 
Tatizo lako hua haujui na hauja gungua haujui ile unbeaten ilikua domestically ndio maana hata Arsenal , Benifica, AC Milan records zao zipo sababu unakuaga pimbi tunaku zoom tu
 
Huyu jamaa anawaita wenzake Changamoto wakati yeye mwenyewe ni changamoto.
Nimepita kwa sekunde 4 tu kaba sijaanza kuisoma tayari nimeona data ambazo sizo, naamini nikipata muda wa kusoma huenda nikaona zaidi taarifa ambazo zisizo.
Mwaka 1986 bingwa hakuwa Majimaji bali Tukuyu Stars.
 
MISIMU MIWILI HAKUKUWA NA BINGWA

Kuna misimu miwili Tanzania haikuwa na bingwa rasmi kutokana na sababu tofauti...mwaka 1970 na mwaka 2003.

1970

Mwaka 1970 ligi haikufanyika kabisa kwa sababu timu nyingi ziligomea kushiriki, zikiongozwa na Yanga na Sunderland (Simba).

Mwaka huo FAT iliruhusu timu nyingi za mashirika kushiriki ligi. Wachezaji wa Yanga na Sunderland walikuwa wanafanya kazi kwenye hayo mashirika(ikiwemo Bandari na Cargo).

Kwa hiyo hayo mashirika yakazuia wafanyakazi wao kuchezea timu za mtaani ili wachezee timu zao za kazini.

Yanga na Sunderland zikakosa wachezaji, zikajitoa kwenye ligi...na ligi haikufanyika.

FAT ikaichagua Yanga ishiriki klabu bingwa Afrika mwaka 1971, kwa sababu walikuwa mabingwa wa msimu uliopita. Yanga wakajihesabia kupewa na ubingwa...lakini walipewa tiketi tu!

2003

Mwaka huu Ligi ya Muungano ambayo ndiyo ilikuwa ligi kuu ya Tanzania, haikumalizika baada ya Yanga kufungua kesi mahakama ya Ilala kupinga ligi kuchezwa kwa mtoano.

Yanga walipangwa kucheza na Jamhuri ya Pemba, na wakatoka Dar Es Salaam kuelekea Pemba. Kufika Unguja wakagoma kwenda Pemba wakisema wamegundua ligi huwa haichezwi kwa mtoano.

FAT na ZFA kama waandaaji wa ligi ya Muungano wakaitoa Yanga na kuipa ushindi Jamhuri. Yanga wakaenda mahakamani kupinga kutolewa.

Mahakama ikasimamisha ligi na kupanga kusikiliza kesi Februari 2004.

Ligi ikasimama na FAT na ZFA wakaipa Simba tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa mwaka 2004.

Simba wakajitangazia kupewa na ubingwa...lakini haikuwa hivyo, walipewa tiketi tu.

Mara hizo mbili, ndizo zinafanya hesabu iwe 58 lakini mabingwa halisi ni 56.

Itaendelea...
 
Nenda CAS Mwanasheria
 
Tatizo lako hua haujui na hauja gungua haujui ile unbeaten ilikua domestically ndio maana hata Arsenal , Benifica, AC Milan records zao zipo sababu unakuaga pimbi tunaku zoom tu
Mara nyingi na ignore replies zako ili nijilindie heshima ila leo nakublock rasmi, usihangaike kujibu post zangu maku wee.

Kama mnafuata standard za Ulaya, na hiyo treble ya juzi mliyofanyia gwaride na tamasha nayo inafuata standard za Ulaya?
 
MFANO KUTOKA ULAYA

Una maanisha msimu wa 1990-91 wa First League Division wa nchini Uingereza ni sawa na Ndondo za mtaani?


Hii hapa ni team squad ya Liverpool ya msimu 1990-91 kabla ya Ligi kuitwa EPL.
 
Mara nyingi na ignore replies zako ili nijilindie heshima ila leo nakublock rasmi, usihangaike kujibu post zangu maku wee.

Kama mnafuata standard za Ulaya, na hiyo treble ya juzi mliyofanyia gwaride na tamasha nayo inafuata standard za Ulaya?
Maku mwenyewe
 
Ni kweli ila swali lingine, je ni sahihi kuweka pembeni takwimu za waliochukua Muungano au na zenyewe inabidi tuzijumuishe pale timu inapojigamba kuwa imechukua ubingwa mara kadhaa?

Kwa nini Yanga hawajumuishi takwimu za Kombe la Muungano?
Yanga imechukua kombe la muungano mara 6 na katika hizo mara sita ni mara moja pekee ndio kawa bingwa wa kombe la muungano pasipo kuchukua kombe la Tanzania bara (mwaka 2000) ila mara tano zote kabeba makombe mawili kwa pamoja. Hivyo kwenye takwimu zao zina makombe mawili kwa pamoja pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…