Zakazakazi: Yanga sio Mabingwa mara 29 na Simba sio Mabingwa mara 22

Mi naona yanga ndio wamejipunguzia idadi inaweza kuwa 30+ ila kwa Sasa ili u trend we ongelea yanga tofauti na Zakaria anajaribu kuwa relevant baada ya kushindwa kufikia malengo ya boss wao ya kuhakikisha kama sio Simba basi Azam awe bingwa ndio anakuja na hizi blah blah
Yanga ni bingwa mara 29 mwakani tunaenda 30 hizo takwimu Wala hazikutoka kwenye maandishi ni zimetoka kwa watu wa Simba na Yanga waliokuwa uwanjani kuyashuhudia hayo kwa macho
 
kwaio kwenye 29 kuna 6 ya muungano na 5 ya bara waliyochukia kwa misimu hio 6 (yani makombe 11 ya ligi ndani ya misimu 6 sio?)

simba na yanga takwimu zao zina uongo mwingi
Umeelewa kweli nilichokisema? Yanga kachukua makombe yote mawili kwa pamoja mara tano. Sasa kwanini wewe umechagua kuhesabia upande wa muungano wakati waliochukua na ligi kuu bara pia?
1983
Muungano [emoji736]
Tanzanian bara [emoji736]

Mwaka 1987
Muungano [emoji736]
Tanzania bara [emoji736]

Mwaka 1991
Muungano [emoji736]
Tanzania bara [emoji736]

Mwaka 1996
Muungano[emoji736]
Tanzania bara [emoji736]

Mwaka 1997
Muungano [emoji736]
Tanzania bara,[emoji736]

Mwaka 2000
Muungano [emoji777]
Tanzania bara [emoji736]
 
Simba kachukua mara tano (1993, 1994, 1995, 2001 na 2002
Kwa hiyo kuna uwezekano katika hizo 29 za Yanga, zimehesabiwa za Bara na za Muungano wakati katika 22 za Simba, za Muungano hazijahesabiwa?

Je hii inamaanisha tukijumuisha makombe yote mawili, tofauti ya Ubingwa wa ndani kati ya Simba na Yanga ni 29-27?

Haya maswali nayauliza kwa nia ya kujua siyo kuleta mabishano.
 
Juu hapo umesema Yanga alichukua Muungano mara 6, hapa umelist miaka 5 na kuchukua mara 4.
 
Kwahiyo Zaka naye ni mtu mwenye akili timamu? Wapi Yanga wamesema ni Mabingwa wa Jamhuri ya Muungano? Huyu Zwaza hajui kuwa Kuna Bingwa wa Tanzania bara na Zanzibar? Halafu kukawa na Bingwa wa Muungano? Huyu Chizi muulizeni Yanga ni Bingwa wa Muungano mwaka huu? Zanzibar kuna Bingwa na Bara kuna Bingwa Sasa kipi hilli Zezeta limeshindwa kuelewa mpaka liwajaze ujinga Mbumbumbu wahed?
Zaka ndio msemaji takataka anayepambana na Yanga na kila anavyojitahidi anaambulia vipigo, akigeukia marefa anajikuta timu yake anatedeka uwanjani hadharani, Mpuuzeni huyu Zezeta nyinyi Mbumbumbu
 
Na hapo amewasahau tukuyu stars bhanyambala
 
Acha mbambamba, tupe mkeka wako. Hizo bingwa 29 ni mwaka gani na kombe lilikuwa linaitwaje kila mwaka Yanga ilipotwaa. Nipo hapa nasubiri...
 
Acha mbambamba, tupe mkeka wako. Hizo bingwa 29 ni mwaka gani na kombe lilikuwa linaitwaje kila mwaka Yanga ilipotwaa. Nipo hapa nasubiri...
TFF wanajua siye ni mabingwa wa kihisoria,kama hutaki wafuate
 
Acha mbambamba, tupe mkeka wako. Hizo bingwa 29 ni mwaka gani na kombe lilikuwa linaitwaje kila mwaka Yanga ilipotwaa. Nipo hapa nasubiri...
Takwimu hapewi kipofu au Chizi anapewa mtu mwenye akili timamu.
Ingekuwa unataka mkeka wangu ungemuuliza kwanza huyo Monitor lizard kuwa huo mwaka Malindi kawa Bingwa wa Muungano je Bingwa wa Bara alikuwa nani? Na kama Yanga ni Bingwa mwaka huu je Zanzibar hakuna Bingwa? Yanga ni Bingwa wa mara 29 wa Ligi kuu ya Tanzania Bara, Sasa wewe ni Zaka mnajipa shida gani hapo?
 
Soma post yangu ya kwanza katika uzi huu nilihoji pia tafiti aliyofanya nikakumbushia hilo suala la Kombe la Muungano. Utafiti wake una kasoro maana umetumia chanzo cha taarifa kisicho sahihi kwa alichokuwa anakitafuta maana si kila aliyeenda kucheza Klabu Bingwa CAF alikuwa bingwa wa bara.

Je miaka ambayo kulikuwa na ligi ya Muungano, mshindi wa ligi ya Bara alikuwa "bingwa wa bara" au "mwakilishi wa bara" katika Kombe la Muungano lililoenda kupata Bingwa?

Bado nahitaji huo mkeka kwa matumizi binafsi.
 
Hahaha, watu wanaumia sana lakini hakuna namna. Yanga imeanzishwa mwaka gani? Je ilikua haichezi ligi mpaka 1965? Jijibu hilo kwanza.

Ila Simba eleweni sisi Yanga ni wakubwa wenu, mabingwa wa kihistoria, tumechukua ubingwa wa ligi kuu mara nyingi na tumewafunga mara nyingi zaidi. Stop trying to divert from the reality, pambameni maana mnayo miaka ya kutosha kuifuta hiyo, na mnaweza mkashindwa kuifuta hiyo historia pia.
 
Tatizo la huu mjadala lipo kwenye chanzo.

Hakuna chanzo rasmi ambacho tunaweza kutumia kama references
 
Kabla ya 1965 kukikuwa na Ligi gani?

Historia inaonesha Yanga ilikuwa inacheza unofficial tournaments za mitaani tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…