Zakazakazi: Yanga sio Mabingwa mara 29 na Simba sio Mabingwa mara 22

Zakazakazi: Yanga sio Mabingwa mara 29 na Simba sio Mabingwa mara 22

Sehemu ya tatu

MWANZO WA LIGI

Nakupitisha kuanzia mwanzo kabisa ili tuelewane vizuri

Pichani kushoto ni Milan Celebic, kocha wa kwanza wa kigeni wa timu ya taifa, kuanzia Tanganyika hadi Tanzania.
Screenshot_20230615-171430.png


Kulia ni mchezaji wa timu ya taifa, Ally Samatta, baba yake nahodha wa sasa timu ya taifa, Mbwana Samatta.

Kocha huyo raia wa Yugoslavia, alikuja nchini mwaka 1964 akiletwa na serikali.

Wakati huo hakukuwa na ligi ya taifa bali ya Dar Es Salaam pekee iliyosimamiwa na chama cha soka cha Dar Es Salaam (Dar Es Salaam Football League Association-DFLA)

Chama cha soka cha taifa kilichoitwa TFA (Tanganyika Football Association) kilisimamia mashindano ya Taifa Cup ambayo yalishirikisha timu za mikoa.

Kupitia Taifa Cup ya 1964, kocha Celebic alimuona Ally Samatta na kumchagua kama mchezaji bora wa nchi, na kumuita kwenye timu ya taifa.

Mwaka huo Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chama cha soka cha Tanganyika, TFA, kikabadilika na kuwa chama cha soka cha Tanzania, FAT.

FIFA ikakisajili rasmi chama hicho kama chama cha soka cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini kwa ndani, FAT ilisimamia soka la Bara, na Zanzibar ikaundwa idara maalumu ya kusimamia soka, iliyoitwa IFOZA, yaani Idara ya Football Zanzibar.

Baada ya michakato yote hiyo, Kocha Milan Celebic akaishauri FAT kuanzisha ligi ya kitaifa itakayomsaidia kupata wachezaji wa timu ya taifa.

Rais wa FAT, Balozi Majjid, akakubaki na ndipo mwaka 1965 ikaanzishwa ligi ambayo iliitwa Mashindano ya kutafuta Klabu Bingwa ya Taifa.

Ligi hiyo ilichezwa bila madaraja, na iliendeshwa kwa mtoano kama ilivyo ASFC, na ilisajiliwa kama ligi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini kwa miaka yote ya 1960, timu za Zanzibar hazikushiriki kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo za kiuchumi na kushindwa kujipanga vizuri kwa IFOZA.

Zilianza kushiriki mwaka 1972 pale timu za Ujamaa na Navy zilipovuka na kuja, na zikaendelea kuongezeka kila mwaka

Miaka ya 1970, mashindano haya yalianzia ngazi ya wilaya, mikoa hadi taifa.

Ngazi ya taifa ilikuwa kwenye kituo kimoja, kama ilivyokuwa 1974 kwenye kituo cha Nyamagana Mwanza.

Itaendelea
 
Kwa hiyo kuna uwezekano katika hizo 29 za Yanga, zimehesabiwa za Bara na za Muungano wakati katika 22 za Simba, za Muungano hazijahesabiwa?

Je hii inamaanisha tukijumuisha makombe yote mawili, tofauti ya Ubingwa wa ndani kati ya Simba na Yanga ni 29-27?

Haya maswali nayauliza kwa nia ya kujua siyo kuleta mabishano.
Hapana hesabu ya Yanga ipo upo upande wa ligi ya bara peke yake, narudia tena unielewe. Yanga wakati anachukua kombe la muungano alikuwa pia anachukua na kombe la ligi kuu bara isipokuwa ni msimu mmoja tu ambao wa mwaka 2000 Yanga aliishia kubeba kombe moja tu la muungano huku ligi kuu bara akibeba Mtibwa Sugar. Hivyo kama kuhesabika ya muungano ni msimu mmoja tu wa mwaka 2000 ila misimu yote Yanga kanyanyua kwapa kote kote ( bara & muungano)
 
Sehemu ya nne
zakazakazi-20230615-0001.jpg (1)~2.jpg


ILIKOTOKA LIGI YETU

Mwaka 1974 Tanzania ililetelewa na FIFA mtaalamu wa kusaidia maendeleo ya mpira.

Mtaalamu huyo raia wa Ujerumani aliitwa Bert Trauttman, kipa wa zamani wa Manchester City ya England na mmoja wa mashujaa wa muda wote wa klabu hiyo.

Huyu ndiye aliyeanzisha chama cha makocha wa mpira nchini, TAFCA.

Alipokuta ligi inachezwa bila madaraja, akaona ni tatizo ndipo akashauri ligi yetu ichezwe kwa madaraja.

Mijadala ikaanza, hayo madaraja yaundwe vipi.

Baada ya kuumiza vichwa sana, mfumo wa mashindano kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa ukafutwa rasmi mwaka 1981.

Kuanzia 1982 ukaanza mfumo mpya. Ile ligi ya bila madaraja iliyoitwa mashindano ya kutafuta Klabu Bingwa ya Taifa, ikaitwa Ligi Muungano.

Halafu zikaanzishwa ligi zingine mbili, kama mashindano ya awali ya ligi ya Muungano..

Ligi hizo ni ya Tanzania Bara na Zanzibar. Huo ndiyo mwanzo wa ligi ya Bara...kabla ya hapo haikuwahi kuwepo!

Ligi hizi mbili ndiyo zikawa na madaraja, kuanzia la kwanza hadi la nne.

Mfumo huu ulikuwa sawa na Marekani wanavyofanya kwa Eastern Conference na Western Conference kwenye mashindano yao.

Bingwa wa Ligi hizi hakuwa na hadhi yoyote zaidi ya kushiriki Kombe la Kagame ambalo wakati huo liliitwa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.

Bingwa wa ligi ya Muungano ndiyo alikuwa na hadhi sawa na yule bingwa wa mashindano ya kutafuta Klabu Bingwa ya Taifa, na alishiriki Klabu Bingwa Afrika.

Ligi hizi mbili zilidumu kuanzia 1982 hadi 2003.

Mabingwa wa Bara 1982-2003

Yanga (11)
Simba (6)
Mtibwa Sugar (2)
Pan African (1)
Tukuyu Stars (1)
Coastal Union (1)

Kama mtihani, tungesema ligi ya hizi mbili, ya Bara na Zanzibar, zilikuwa Moko, halafu logo ya Muungano ndiyo mtihani wa taifa.

Hata uwe Tanzania One kwenye Moko, kama umefeli mtihani wa taifa, wewe ni ANDAZI.

Kwa hiyo mabingwa hawa wote hawakuwa na hadhi yoyote kwenye rekodi za CAF wala FIFA.

Mabingwa wenye hadhi walikuwa wale wa Ligi ya Muungano.

Itaendelea....
 
changaule
Tate Mkuu
Bila bila

Someni hapo

Kumbe ligi ya muungano ambayo leo hii mnaiona inferior ndio iliyokuwa yenye hadhi kuliko ligi zetu na mmetulia tu
lengo la ligi ya muungano ilikuwa ni kudumisha Muungano wetu na kutoa usawa wa kiuwakilishi katika michuano ya kimataifa ya vilabu, hii ni kutokana na Tanzania bara kuwa na ligi yake na Zanzibar kuwa na ligi yake huku upande wa pili (Zanzibar) ukiwa sio mwanachama wa shirikisho la soka barani Africa caf, hivyo kukosa sifa ya timu zake kushiriki michuano ya vilabu bingwa africa na kombe la washindi (ilijulikana hivyo miaka hiyo). Kwa kuwepo kwa ligi ya Muungano ambayo ilikuwa inajumlisha timu 3 zilizomaliza nafasi juu kwenye ligi husika basi timu kutoka Zanzibar nazo zilipata nafasi ya kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano kwenye michuano ya CAF.
 
ila utopolooo.janja janja nyingi.ndo maana nabi kawakimbia.nabi alipokuwa anafungwa fungwa mlitaka afukuzwe leo mnamuita profesa.mzee kashtukia MTEGO
 
Kwenye Website ya Yanga hadi mwaka 2016, ukihesabu miaka waliyoiandika inaonesha wamechukua ubingwa mata 22.
Ila juu wameandika wamechukua ubingwa mara 27.

Nimeshindwa kuwaelewa
Ukiachana na source ya website ya yanga je kwenye vyanzo vingine vinaonesha mara ngapi?
 
Back
Top Bottom