Zama za Kilimanjaro Express zimeisha

Zama za Kilimanjaro Express zimeisha

Juzi kati nikawa na kijisafari cha kuelekea mikoa ya huko kaskazini mwa Tanzania.
Nikasema ngoja nipande Kilimanjaro express, duh kwa kweli nilijuta sana kupanda lile basi.
Cha kwanza tulidanganywa kuwa basi ni luxury hivyo tukakatishwa nauli kubwa ila kiuhalisia hakuna luxury bus pale, bus siti zake zimechakaa,ndani linatoa harufu kama ya uvundo flani hivi,hakuna cha AC wala TV ndani ya basi. Basi lilikua limejaza kiasi kwamba abiria wengine wakawa wamekaa pale mbele kwa dereva na tulikua tukifika karibu na mizani wanawashusha baadhi ya abiria wanawachukulia bodaboda then tunawakuta mbele ya safari tukishavuka mizani.
Wahudumu wa basi ni kama wamekata tamaa yani hawana mwamko na kazi yao wanaongea lugha mbaya kwa abiria,badala yake muda wote wa safari walikua wamekaa tu kule mbele wanapiga story pasipokusikiliza abiria
pia bus lilikua linavuja.
Kwa kweli Kilimanjaro express niliyoipanda miaka mitano huko nyuma ina tofauti kubwa sana na hii ya leo.wakati narudi Dar nikasema ngoja nijaribu kupanda BM coach,kwa kweli nimeinjoy sana kusafiri na BM,huduma nzuri sana na wahudumu wao wakarimu mno.
Kilimanjaro express msipobadilika na kufanyia kazi hizi kero za wateja wenu basi naweza kusema huu ndiyo mwisho wa zama zenu.
Mkuu badala ya kupiga picha basi na siti zake mbovu umepiga tiketi!!!
 
Wapo hovyo sio uongo...
Hayo luxury nilipanda siku moja walisema iko na choo ndani kumbe ni haja ndogo tu...sasa kuna mwanamke mmoja akafanya kubwa badala ya ndogo Aisee gari zima ilinuka safari ilikuwa chungu sana na watu walikuwa wanalalamika mno
Kwani wanawake wanakunyer?
 
mkuu majinjah, ni mashine zile. ziache tu,
we uliza tu safari zao ni za wapi, dar-sumbawanga, dar kibondo,
ukitaka kujua, wewe siku ukipanda ukishuka toka nje kaisikilize ikiwa inanguruma.
Majinjah ni scania au volvo. ,

YEREMIAH 23
Hizi hizi CDE, BUL??
Zinazojazwa maji Kila baada ya km 100 ili kupooza radiator, come on
Ilitufikisha Dodoma saa 11 jioni kutoka Moro saa nne, halafu tukafika mpanda saa 10:30 alfajiri
 
Mkuu hakuna Luxury buses Tanzania kama wanavyozitaja.

Ni ile BM moja tu yenye seat nne mwanzoni za kuweza kuadjust na kulala comfortably na ina space ya kuweka food stuffs

Mengine yote ni matangazo tu...Mara Luxury, Mara semi luxury....hamna kitu.
Na pia ma-bus yote yanayoletwa bongo hua Ni kwa ajili ya watu wafupi tu.
 
Arusha panda
1. BM
2. Tilhisho
3. Marangu

Ukikosa hayo panda
4. Extra luxury
5. Esther
Ukikosa haya hairisha safari ndugu hao wakina Kilimanjaro sijui Dar express wamejichokea ni safari za kubahatisha.
Nilipata extra luxury, niliridhishwa na huduma.
 
Attachments

  • 20220710_165259.jpg
    20220710_165259.jpg
    533.3 KB · Views: 8
Juzi kati nikawa na kijisafari cha kuelekea mikoa ya huko kaskazini mwa Tanzania.
Nikasema ngoja nipande Kilimanjaro express, duh kwa kweli nilijuta sana kupanda lile basi.
Cha kwanza tulidanganywa kuwa basi ni luxury hivyo tukakatishwa nauli kubwa ila kiuhalisia hakuna luxury bus pale, bus siti zake zimechakaa,ndani linatoa harufu kama ya uvundo flani hivi,hakuna cha AC wala TV ndani ya basi. Basi lilikua limejaza kiasi kwamba abiria wengine wakawa wamekaa pale mbele kwa dereva na tulikua tukifika karibu na mizani wanawashusha baadhi ya abiria wanawachukulia bodaboda then tunawakuta mbele ya safari tukishavuka mizani.
Wahudumu wa basi ni kama wamekata tamaa yani hawana mwamko na kazi yao wanaongea lugha mbaya kwa abiria,badala yake muda wote wa safari walikua wamekaa tu kule mbele wanapiga story pasipokusikiliza abiria
pia bus lilikua linavuja.
Kwa kweli Kilimanjaro express niliyoipanda miaka mitano huko nyuma ina tofauti kubwa sana na hii ya leo.wakati narudi Dar nikasema ngoja nijaribu kupanda BM coach,kwa kweli nimeinjoy sana kusafiri na BM,huduma nzuri sana na wahudumu wao wakarimu mno.
Kilimanjaro express msipobadilika na kufanyia kazi hizi kero za wateja wenu basi naweza kusema huu ndiyo mwisho wa zama zenu.
Kila chenye mwanzo kina mwisho wake
 
Hiyo kampuni hata kama hapo katikati ilikuwa inatoa huduma nzuri, niseme tu kwa sasa hiyo huduma wanayotoa sasa hivi ndio level zao. Kwa sie wahenga tuliosafiri mwanzoni mwa miaka ya 2000 tulikuwa tunaikwepa maana mnaweza kuishiwa mafuta njiani....enzi hizo kampuni ilikuwa inajulikana kama Kilimanjaro trucks au Sawaya

N.B. kama taarifa ya kweli lakini maana kwa gari za Arusha kwa Kilimanjaro Express sio mbaya sana
Yule anazidi kudorora daily. Subiri afundishwe kazi na akina BM. Atanyooka tu.
 
Juzi kati nikawa na kijisafari cha kuelekea mikoa ya huko kaskazini mwa Tanzania.
Nikasema ngoja nipande Kilimanjaro express, duh kwa kweli nilijuta sana kupanda lile basi.
Cha kwanza tulidanganywa kuwa basi ni luxury hivyo tukakatishwa nauli kubwa ila kiuhalisia hakuna luxury bus pale, bus siti zake zimechakaa,ndani linatoa harufu kama ya uvundo flani hivi,hakuna cha AC wala TV ndani ya basi. Basi lilikua limejaza kiasi kwamba abiria wengine wakawa wamekaa pale mbele kwa dereva na tulikua tukifika karibu na mizani wanawashusha baadhi ya abiria wanawachukulia bodaboda then tunawakuta mbele ya safari tukishavuka mizani.
Wahudumu wa basi ni kama wamekata tamaa yani hawana mwamko na kazi yao wanaongea lugha mbaya kwa abiria,badala yake muda wote wa safari walikua wamekaa tu kule mbele wanapiga story pasipokusikiliza abiria
pia bus lilikua linavuja.
Kwa kweli Kilimanjaro express niliyoipanda miaka mitano huko nyuma ina tofauti kubwa sana na hii ya leo.wakati narudi Dar nikasema ngoja nijaribu kupanda BM coach,kwa kweli nimeinjoy sana kusafiri na BM,huduma nzuri sana na wahudumu wao wakarimu mno.
Kilimanjaro express msipobadilika na kufanyia kazi hizi kero za wateja wenu basi naweza kusema huu ndiyo mwisho wa zama zenu.
Mkuu inaelekea wewe siyo mpandaji sana wa mabasi, hao BM wana huduma mbovu sana sijawah ona ofisini kwao. Nilishaenda kukata ticket ofisini kwao nikaona isiwe shida wakati hela ni ya kwangu nikasepa. Through experience na Kilimanjaro, Luxury huwa huwa zinakuwa chache sana na mara nyingi zinaondokaga saa 3 asubuhi- na kama hazipo huwa wanakuwa fair sana kusema ukweli.
- Hii habari ya kwamba KLM wanajaza sana mpaka abiria wanakosa pa kukaa nadhani ni uongo uliotukuka 🤣 🤣 🤣 . KVC au MBAZI tu na nauli zao za 20'000 hawawezi kujaza msimu huu wa ukosefu wa abiria ndo sembuse KLM 🤣🤣
 
Back
Top Bottom