Muda mwingine kutumia hekima kwenye changamoto hizi za kifamilia ni kujimaliza mwenyewe, unaonesha upendo kwa watu ambao wao hawana upendo na wewe. Wanakuchekea kinafiki ukiwapa msaada, wakitoka wanapanga mipango ya kukudhuru na kukuombea uharibikiwe.
Binadamu wana Roho mbaya sana, hata Yesu hakuwa na kosa lakini walimsulubu msalabani japo aliwapa chakula wakiwa hoi na njaa walivokula na kushiba wakaanza kumtesa. Wanaonesha kukupenda lakini mioyo yao imejawa chuki. Naandika haya nikiwa na Jazba siku kadhaa zilizopita ningekuwa niko karibu na viumbe hawa waliofanya niandike hapa basi leo maiti kadhaa zingekuwa mochwari au zishazikwa na mimi ningekuwa nyuma ya nondo.
Ndugu zangu kwa sasa ni ndugu wa damu tu wadogo zangu na mama zangu. Hawa wanaojiita ndugu za baba huu ushenzi wanaoniletea kwenye familia yangu na mimi binafsi pamoja na kujishusha sana kwao Imefika mahali imetosha, naona ni kama nakumbatia kundi la wachawi huku nikijifanya nawapenda. Huku wao wakiwa na mipango yao binafsi.
Nimesaidia sana kifedha na kila aina ya msaada lakini hawa watu nia yao sio njema Lakini majibu niliyowapa nadhani washanifahamu kwamba mimi sasa ni mtu wa namna gani, siwezi kukumbatia nyoka tena.
Nilipofikia ukinipiga kofi, nakurushia bomu huu upuuzi wa kumuachia Mungu aamue sina tena. Tutajibu dhambi zetu tukiwa kwenye kiti cha enzi.
Zegota Msaada una hatarisha uhuru wa mtu, mimi ningekuwa ndugu yako ningekuroga hasa ufilie kwa mbali, ndugu zako wako sahihi kukuumiza, kukuombea mabaya!
kwa nini unawasaidia? kwani wao vilema? hawana mikono? akili, na utashi? au Mazezeta pa kutoa misaada hupajui? Ndugu zake Matonya, Mayatima! shule ya viziwi Buguruni Malapa, hupajui? peleka misaada huko!
Misaada hatari kwa uhuru, kwa nini ulihatarisha uhuru wao kwa misaada yako? na ulijuaje ulicho wapa kinakidhi mahitaji yao? wewe ndiyo una roho mbaya! unachuki ambayo huijui, unawaroga kisaikolojia kwa kile unachoona binafsi ni Misaada! umtatulie ndugu yako matatizo usiyo yajua?
Ndugu zangu wa Damu, popote mlipo Diasporas na kwingineko ole wenu mnisaidie mimi Nyarusare, naanza nanyi kuwamaliza! wengine wanajipendekeza kupenyeza vijimisaada maksudi sababu Baba ya mtu ni tajiri, ili wamsimange baadaye! na ku gain popularity! kupitia mgongo wangu!
Ndugu Mpe njia yatosha, usimuonyeshe njia, bali Mpe njia ya mafanikio halafu mtupe nje ya Mawanda yako, Mtukane on the spot! atajiju hiyo safi sana, atarudi kukushukuru! na mtakuwa kitu kimoja!
Na ndugu mpenda vya kupewa toka hapo kwa bro! wako, anza hivo ulivo! kalale chini sokoni kariakoo! kashinde stendi, kula kwa ma ntilie, osha vyombo/suuza, atakulipa, Malori ya Mkoa yakija usiku jichanganye na Matingo piga kazi upate msingi. Msaidie wewe huyo anaye penda kukupa misaada wewe.
Weye ndiyo uwe tegemeo la misaada kwao, siyo wewe ndiyo upewe kataa vya kupewa hata ukilala njaa! ikibidi watie Bakora seriously wale watoa misaada kwako wote! then watupie hela zao usoni, japo huna kitu! hii itawachanganya, soon watakuiga mwenendo wako wa maisha!
Mleta Mada wewe ni Hatari sana! kuliko siraha za maangamizi au Bomu la Nuclear! Msaada haujawahi kuiletea jamii yeyote Maendeleo Duniani! Leo miaka zaidi ya hamsini bado Tanzania mnatega Bakuri chanzo humuhumu yaani ni watu km wewe!