Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Muda mwingine kutumia hekima kwenye changamoto hizi za kifamilia ni kujimaliza mwenyewe, unaonesha upendo kwa watu ambao wao hawana upendo na wewe. Wanakuchekea kinafiki ukiwapa msaada, wakitoka wanapanga mipango ya kukudhuru na kukuombea uharibikiwe.

Binadamu wana Roho mbaya sana, hata Yesu hakuwa na kosa lakini walimsulubu msalabani japo aliwapa chakula wakiwa hoi na njaa walivokula na kushiba wakaanza kumtesa. Wanaonesha kukupenda lakini mioyo yao imejawa chuki. Naandika haya nikiwa na Jazba siku kadhaa zilizopita ningekuwa niko karibu na viumbe hawa waliofanya niandike hapa basi leo maiti kadhaa zingekuwa mochwari au zishazikwa na mimi ningekuwa nyuma ya nondo.

Ndugu zangu kwa sasa ni ndugu wa damu tu wadogo zangu na mama zangu. Hawa wanaojiita ndugu za baba huu ushenzi wanaoniletea kwenye familia yangu na mimi binafsi pamoja na kujishusha sana kwao Imefika mahali imetosha, naona ni kama nakumbatia kundi la wachawi huku nikijifanya nawapenda. Huku wao wakiwa na mipango yao binafsi.

Nimesaidia sana kifedha na kila aina ya msaada lakini hawa watu nia yao sio njema Lakini majibu niliyowapa nadhani washanifahamu kwamba mimi sasa ni mtu wa namna gani, siwezi kukumbatia nyoka tena.

Nilipofikia ukinipiga kofi, nakurushia bomu huu upuuzi wa kumuachia Mungu aamue sina tena. Tutajibu dhambi zetu tukiwa kwenye kiti cha enzi.
Zegota Msaada una hatarisha uhuru wa mtu, mimi ningekuwa ndugu yako ningekuroga hasa ufilie kwa mbali, ndugu zako wako sahihi kukuumiza, kukuombea mabaya!

kwa nini unawasaidia? kwani wao vilema? hawana mikono? akili, na utashi? au Mazezeta pa kutoa misaada hupajui? Ndugu zake Matonya, Mayatima! shule ya viziwi Buguruni Malapa, hupajui? peleka misaada huko!

Misaada hatari kwa uhuru, kwa nini ulihatarisha uhuru wao kwa misaada yako? na ulijuaje ulicho wapa kinakidhi mahitaji yao? wewe ndiyo una roho mbaya! unachuki ambayo huijui, unawaroga kisaikolojia kwa kile unachoona binafsi ni Misaada! umtatulie ndugu yako matatizo usiyo yajua?

Ndugu zangu wa Damu, popote mlipo Diasporas na kwingineko ole wenu mnisaidie mimi Nyarusare, naanza nanyi kuwamaliza! wengine wanajipendekeza kupenyeza vijimisaada maksudi sababu Baba ya mtu ni tajiri, ili wamsimange baadaye! na ku gain popularity! kupitia mgongo wangu!

Ndugu Mpe njia yatosha, usimuonyeshe njia, bali Mpe njia ya mafanikio halafu mtupe nje ya Mawanda yako, Mtukane on the spot! atajiju hiyo safi sana, atarudi kukushukuru! na mtakuwa kitu kimoja!

Na ndugu mpenda vya kupewa toka hapo kwa bro! wako, anza hivo ulivo! kalale chini sokoni kariakoo! kashinde stendi, kula kwa ma ntilie, osha vyombo/suuza, atakulipa, Malori ya Mkoa yakija usiku jichanganye na Matingo piga kazi upate msingi. Msaidie wewe huyo anaye penda kukupa misaada wewe.

Weye ndiyo uwe tegemeo la misaada kwao, siyo wewe ndiyo upewe kataa vya kupewa hata ukilala njaa! ikibidi watie Bakora seriously wale watoa misaada kwako wote! then watupie hela zao usoni, japo huna kitu! hii itawachanganya, soon watakuiga mwenendo wako wa maisha!

Mleta Mada wewe ni Hatari sana! kuliko siraha za maangamizi au Bomu la Nuclear! Msaada haujawahi kuiletea jamii yeyote Maendeleo Duniani! Leo miaka zaidi ya hamsini bado Tanzania mnatega Bakuri chanzo humuhumu yaani ni watu km wewe!
 
Hii hoja naiunga mkono 100% by experience kabisa. Ninapitia changamoto kubwa sana japo hata mafanikio yenyewe sina! Ukiwa na ukoo masikini sana ukawa wa kwanza kupata kiugali kiduchu cha serikali ndugu wanakuvagaa hawataki kusikia majibu ya 'sina hela' wala 'subiri wiki ijayo', ngoma ni on the spot! Kuna wakati natamani kuacha kazi hii ya kimasikini inayonijazia chuki na lawama tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uache kazi kisa ndugu? Acha umama, achana nao
 
Wewe ni ndugu yake!!? Au mnapenda zogo tu.

Haya kasaidika nini sasa!?
kwani ameomba msaada? au ametoa mawazo yake tu. hata hivyo wewe huoni msaada wa mawazo ya wengine humu,huoni maoni kinzani humu?au ulitegemea msaada wa chakula
 
Hii hoja naiunga mkono 100% by experience kabisa. Ninapitia changamoto kubwa sana japo hata mafanikio yenyewe sina! Ukiwa na ukoo masikini sana ukawa wa kwanza kupata kiugali kiduchu cha serikali ndugu wanakuvagaa hawataki kusikia majibu ya 'sina hela' wala 'subiri wiki ijayo', ngoma ni on the spot! Kuna wakati natamani kuacha kazi hii ya kimasikini inayonijazia chuki na lawama tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi Bora nihonge hela kwa Demu angalau najua naweza kupata "return to investment" kuliko nisaidie ndugu
 
Kama unaniongelea mimi vileeee.........



Dah
Ni hatari sana
Nanukuu..."mpaka sasa kwa umri huo hana hata nyumba, hana maendeleo yoyote yupo yupo tuu anazurura mjini"

Wakasahau kwamba Mwamba kila akikusanya akiba inaishia kusomesha na kuwatibia hao hao ndugu wanaosema hafanyi maenedeleo...
Asipo wasaidia wanamuita moaka kwenye vikao vya ukoo, akiwasaidia wanamcheka kisa hafanyi maendeleo...

Ndugu tuna maudhi mengi sana..
 
Nilichojifunza kwa Tanzania hii ukijifanya mwema unatoa misaada inajiingiza kwenye matatizo na chuki maana wengine unawasaidia kiroho Safi kumbe wanachukia, wengine wanaenda hata kukuloga ili uangamie, maana kutoa msaada wanaona unaringa,ni Bora wakukomeshe ili mkose wote wakucheke. Dunia hii Bora kuwa na roho mbaya, kwanza watu watakuogopa sana
Kwani huwezi kumsaidia mtu wakati huo huo ukaweka mipaka ya mazoea ya kijinga jinga?? Kitu tunachokosea wabongo ni kuleta mazoea yasiyo na msingi na ile dhana ya polygamy family, unakuta mtoto wa shangazi sijui mama mdogo, mtoto wa dada wote wanakaa kwako.. Hapa lazima kuna lawama..

Mzee Mkapa alikuwa na ndugu wengi tu na alikuwa akiwasaidia sana sana pasipo kuwa na mazoea yaliyovuka mipaka na ki ukweli hao ambao aliweka nao mipaka waliupokea msaada na wakautumia vizuri. Sasa cha kushangaza Kuna binti mtoto wa dada yake aliyemchukua na kuishi nae, huyo ndiye akaja kuwa sifuri na wa ajabu kabisa.

Tujifunze kusaidia wengine na kuweka mipaka ya mazoea, ndugu wana lawama lakini kuacha kuwasaidia eti kuogopa hizo lawama hiyo nayo ni roho mbaya iliyovuka mipaka.
 
Back
Top Bottom