Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Nilichojifunza kwa Tanzania hii ukijifanya mwema unatoa misaada inajiingiza kwenye matatizo na chuki maana wengine unawasaidia kiroho Safi kumbe wanachukia, wengine wanaenda hata kukuloga ili uangamie, maana kutoa msaada wanaona unaringa,ni Bora wakukomeshe ili mkose wote wakucheke. Dunia hii Bora kuwa na roho mbaya, kwanza watu watakuogopa sana
Binadamu ni social being

Kuishi kibandidu kunasababisha stress na vifo vya mapema.
 
Kitu kigumu sana kwenye haya maisha ya kijamaa, ni wewe ndo uwe mtu wa kwanza kufanikiwa kwenye familia au ukoo wenu.

Aisee, acha niishie hapa!
Hii hoja naiunga mkono 100% by experience kabisa. Ninapitia changamoto kubwa sana japo hata mafanikio yenyewe sina! Ukiwa na ukoo masikini sana ukawa wa kwanza kupata kiugali kiduchu cha serikali ndugu wanakuvagaa hawataki kusikia majibu ya 'sina hela' wala 'subiri wiki ijayo', ngoma ni on the spot! Kuna wakati natamani kuacha kazi hii ya kimasikini inayonijazia chuki na lawama tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwajua aina ya ndugu wanaonizunguka nilitengeneza namna ya wao kubaki mbali nami na mimi kuwa mbali nao na imenisaidia sana,siwalaumu na wao hawanilaumu japo hawaishi vitimbi vya fitna
Na namshukuru mola kwa kunipa kizazi kwani nawafundisha na kuwaaminisha watoto kuwa kwa idadi yao wanaweza kutengeneza na kuendesha clan lao bila kuomba kuwajua ndugu wengine
Nimebakisha watoto na mke kwa mbaali kuwa ndo watu wangu wa karibu
You creating a self isolated family
 
Binadamu sijui kwanini ni wepesi wakusahau.
Tukumbuke hata aliye na pesa leo mwanzo alikua masikini kwani hakuna anayekuja na pesa hapa duniani.
Hivyo kama masikini wanatabia mbovu hata wewe ulishawahi kuzipitia kabla hujawa na vijisenti.
Tukumbuke pia hakuna mwenye uhakika wa kuendelea kuwa tajiri,ewe mtoa mada inawezekana kabisa ndani ya wiki tu nawe ukawa masiki kama wao.
Binafsi huwa naona wenye vijisenti(sio matajiri kama wao wanavyodhani)wengi wao wanamatatizo yakisaikolojia wanafikiri kila anayegombana naye ni kwasababu wanaonewa wivu.
Nawakumbusha tu hata wasio nacho pia hugombana wao kwa wao hivyo acheni dhana za hovyohovyo.
Hii misaada yenu isigeuke manyanyaso kwa ndugu zenu sio lazima kusaidia bakini na pesa zenu.
Nawakumbusha misaada ipo ya aina nyingi sio lazima iwe pesa,masikini huwasaidia sana matajiri kwa mengi sema huwa hawana fadhila.
Mnapougua na kujiharishia vitandani hawahawa mnao wananga ndio huacha shuguli zao kuhangaika na nyinyi hata kama mkae mwezi vitandani
 
Back
Top Bottom