Zamani nilivyokuwa Mjinga!

NILISHINDWA KUANDIKA NNE KWENYE MTIHANI WA DARASA LA KWANZA NIKAANDIKA INE...Big kosa never 4get 96 marks nna pepa mpaka leo toka 1987.
 
Mm darasa la pili niliulizwa MTAKA CHA UVUNGUNI SHARTI nikajibu PANYA
 
Nilivyokuwa mdogo nilisimuliwa kuwa gari aina ya range rover ikikimbia sana inapaa kama ndege
 
sitakaa nisahau enzi hizo utoto akili yote ilijaa mapicha/movie, kwenye pepa moja kulikua na maswali ya kuandika kinyume mf, nene-nyembamba, kuna swali tukaambiwa kinyume cha adui nikajibu stelingi.

wewe ni kiboko
 
kuna jamaa alitudanganya 2kipanda pesa utaota mti mkubwa sana wa pesa nasi tutatajirika! Tukafukia mia tano chini ya udongo na kukojolea et tunamwagilia mbegu* tuliporud shule tukakuta shimo 2 na hakuna pesa....jamaa alishafukua na kuchukua pesa

ha'ha'ha'ha'ha'ha naweza zimia
 
Nikiwa darasa la tatu(Njombe huko) masikini hatujui hata kubalehe ni nini basi classmate wetu mvulana alikuwa mchokozi akagombana na rafiki yangu msichana akamwambia ndio maana una "mavu zi" bila kujua "mavu zi" ni nini nikamwambia "mavu zi" mwenyewe ghafla na mwalimu akawa anaingia akatoa kisago maana alilisikia lile neno akatuchukua mimi, rafiki yangu, na yule mvulana akatupeleka ofisini...... kufika ofisini akawaambia walimu nimewakuta wanagombana tena wanatukanana wanambiana mavu zi sasa nataka waniambile mbele ya walimu wenzangu eti mavu zi ni nini?

Mwalimu mmoja akadakia akasema mwalimu kwani wewe hujui"Mavu zi" ni nini, si ni matunda ya Uwemba hahaha walimu wote waliangua kicheko ila tulikula mboko tatu tatu kila mmoja kisha tukarudi darasani na nilikuwa sijui mavu zi ni nini mpaka nilipokua muda wote nilikuwa na lile jibu kuwa ni matunda ya Uwemba.
 
mimi nilikuwa nadhani zile picha za ukutani sebuleni wazazi walikuwa wakiniona hivyo nilikuwa naogopa kudokoa chochote kilichopo sebuleni:becky:

haaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
sitakaa nisahau enzi hizo utoto akili yote ilijaa mapicha/movie, kwenye pepa moja kulikua na maswali ya kuandika kinyume mf, nene-nyembamba, kuna swali tukaambiwa kinyume cha adui nikajibu stelingi.

haaaaaaaaaaaa, kweli ilikuwa ujinga. Tena stelingi ni rambo.
 
1.nilimwambia mama nataka kuwa konda baada ya kumwona anahela xaaaaaanaaa.
2. nkitoka kwenye gar nkaingia nyumban nakuta hamna umeme nashangaa heee!!!mbna kwenye gar upo?
3. wakat nipo darasa la pili nliambiwa ndugu yako kapata one form four ujitahid upate na ww one nkasema mi ntampita ntapata zero kwakua mwl kasema inaanza kabla ya moja.
 
Nakumbuka nikiwa darasa la pili ckwenda shule nkaenda porini na mama kumsaidia kulima, kesho yake mwalimu akaniulza kwanini ckwenda shule jana yake nkamjibu "mama kaniambia nkae nyumbani nkore soko" ikiwa na maana mama kaniambia nikae nyumbani nipike kunde, basi darasa zima na mwalimu wakanicheka nkaona aibu nkatoka nje mbio.
 
Nilipokua mdogo,Ilikua kombe la dunia nikasikia jamaa amefunga goli la kuotea,Hivyo limekataliwa! Niliwaza kweli,REFA alijuaje kama jamaa ameota kuwa leo atafunga goal???
 
nikiwa mdogo nilipenda sana mipanz mpaka nikiulizwa nichague mipanz na nyumba nachagua mipanz! ha' ha' ha' ha'
 
370H-SSV-0773H.



turn this code upsidedown and decode.
 
hahahaha.......uwiiii....nimecheka kweli na hizi comments zenu. duh
 
AMAVUBI umeniacha hoi bin taabani eti soko kuuuubwaaaa......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…