Zamani nilivyokuwa Mjinga!

Zamani nilivyokuwa Mjinga!

Mimi nilikuwa najua padre hanyi maana anavaa kanzu na anandisha mambo ya MUNGU.
 
Mimi nlikuwa naogopa ntakapokufa ntakuwa napumuaje ntakapofunikwa kaburini.
 
Mimi nilikua naogopa kumtaja Nyerere eti nitakamatwa
 
Niliwahi kuulizwa unakaa wapi nikajibu kwenye kiti
 
Mara ya kwanza kumuona mlevi, alikuwa anatafuna karanga, hivyo nikajua karanga ndio pombe.
 
mimi nilijua na kuamini kuwa maendeleo ya watanzania yataletwa chini ya CCM......lazima nilikuwa punguwani kichizi!
 
Kuna dogo class kwenye hili swali la kinyume alijaza kama hivi:-

1. Njaa = anja
2. Kulia = aliku
3. ...

Nimekumbuka enzi izo nipo class tatu shule ya msingi BARAA huko Ar tuliambiwa kinyume cha neno SIMAMA si nkasema MAMASI?
 
Back
Top Bottom