Una uhakika hawa walitokea familia masikini ? Zamani drs lilikuwa mwisho la 4 kisha wanapelekwa middle school kwa mchujo mkali.
Ni kama leo ukiulizwa kwa nini hujaenda kusoma havard au oxford wakati wenzio wanaenda kusoma huko kila mwaka ?
Hivi ukiulizwa kwa nini hujaunda kitu chochote cha maana wakati kuna wenzio kama wewe huko India china wanaunda vifaa mbali mbali utajibuje ? Kwa nini wewe sio tajiri na haufahamiki wakati kuna mitandao ya kijamii inampa mtu umaarufu sekunde ?
Maswali ni mengi sana yanayokuhusu wewe na wakati wa sasa na uneshindwa kutimiza, ni hivyo hivyo wazee wako walishindwa.
Watu wa dini wanasema Myngu ndio muweza wa yote. Wengine wanasema utajiri au mafanikio ni bahati.
Mada ni kumiliki ardhi na kumudu uchumi binafsi, yaani kutokuwa mzigo kwa uzao wako.
Hivi unajua kuna zamani kulikuwa na wigo mpana wa ajira tofauti na sasa na wazee wengi walikuwa wanachagua kazi kwa kujazana ujinga?
Kwa mtu aliyezaliwa 1950 unajua wengi wao walipata umri wa kuajiriwa nchi tayari ikiwa imepata uhuru tofauti na hizo simulizi unazoleta sijui za middle school et al.
Hivi una habari kuna watu waliajiriwa kuwa watendaji kwa sifa ya kujua kusoma na kuandika tu ila wengi walikataa kuwa hawataki kufanya kazi vijijini?
Unafahamu kuna watu waliajiriwa kwenye Majeshi kwa sifa za kadi ya umoja wa vijana tu, yaani unakuta mtu hajui kusoma wala kuandika anatia sahihi kwa dole gumba na bado alikula ajira?
Una habari mashirika ya umma chini ya Serikali ya Tanganyika kama vile NMC, TRC na Tanganyika packers yalimwaga ajira kwa sifa ya kuwa raia tu unalamba ajira bila hata usaili yaani kama vile unaandikishwa shule?
Wapo waliokubali ajira za wakati huo na wakatumia vibaya vipato vyao mwisho wa siku wakawa na majuto, wapo waliokataa hizo ajira wengine ndiyo wakaanza michezo ya kuzamia kwenda ulaya wapo waliotoboa na wapo walioishia jela.
Wengi wanaoyumba kwasasa aidha ubishoo, uvivu, matumizi mabaya ya vipato vyao na kuchagua ajira ndiyo kumewafanya kuishi kilofa hii leo na hakuna cha kuilaumu Serikali maana hakuna kipindi nchi ilikuwa haina changamoto ya ajira kama kipindi hiko, labda kwa kizazi hiki ndiyo kweli changamoto ya ajira imeanza kushamiri tena mostly kuanzia awamu ya 5 tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa ukimaliza kusoma ualimu au udaktari ni mwendo wa kushinda kwenye tv tu ukisubiria post.
Majeshi ndiyo usiseme ilikuwa sifa damu na nguvu hata darasa la 7 anakula C/no.
Usiwatetee hao wazembe Mkuu waliouchezea ujana