Zamani Wazazi waliuza Binti zào Kwa Kile kiitwacho Mahari. Kwa Sasa ni Mila Potofu na biashara haramu

Zamani Wazazi waliuza Binti zào Kwa Kile kiitwacho Mahari. Kwa Sasa ni Mila Potofu na biashara haramu

Niwie radhi Mkuu

Umebahatika kuwa na Wazazi wote wawili (Me na Ke)? Kama hautajali unaweza kumuuliza Bi Mkubwa(Kama yu angali hai) kama aliolewa Kwa kutolewa mahari ama alichukuliwa bure kwenda kuishi na Mzee?

Tunaweza kujadili mambo ya Ndoa na mahari na kumbe mwenzetu Mtibeli hajaoa wala hana mpango wa Kuoa 🙌
 
Zamani huku ulichoandika hakikuwepo.

Mwanamke huweza KUTOLEWA mahari yàani kununuliwa na Mtu àmbaye hata hakuwa akimjua.

Zamani Ndoa za kulazimishwa zilikuwa NI nyingi Mno, tenà karibia zote zilikuwa Ndoa za kulazimisha. Kilichoangaliwa NI Mnunuzi atatoa shillingi ngapi, yàani mwenye mahari kûbwa ndiye atakayeoa Binti.

Hiyo ya Mwanamke kujua anaenda na kuamua pakuolewa haina hata Karne Moja toka ianze
Hii ndo ulipaswa uipinge kulazimishwa ila kama anaenda Kwa hiari yake sio.

Kingine Cha kupingwa ni Ile kutofautiana mahari na kusababisha uchumba kufa hii haipo sawa kikubwa kama wamekubaliana wao iwe hivo Kwa mahali yoyote Ile.

Andiko lako lipo sawa ukiamua umtoe Bure sio kosa Wala ukiamua upokee mahari sio kosa. Ni wewe mwenyew utakavyo jisikia
 
Mahari sio bei ya kununua mtu hizo elimu mnazosoma kijinga jinga za kukariri ndizo zinekufikisha hapo ukasoma kakingereza bride price unakuja wangu wangu na mada ya kijinga

Mahari elewa sio pesa pekee watu wanalipa mahari ng'ombe hadi 50

Mahari ni kionyeshi cha kama mume mtarajiwa ana uwezo wa kutunza mke

Lakini kwa wewe kwa kuwa huna mpango wa kuoa na huwezi kuoa wewe hilo linaeleweka waachie wenyewe waoaji sababu kwenye hilo kundi la wanaume waoaji humo pamoja na kuwa na jina la kiume

Ndîo maana nikasema hiyo ni Mila na dhana potofu.
Kwaakili yako hela ya kununua Mwanamke àmbayo utaitoa Siku Moja inathibitishaje kuwa utaweza Kumtunza mwanamke Kwa Miaka yote?

Kwa hîyo wewe ukibet ukapata Milioni tano ukaenda Kutoa mahari ya Milioni nne Wazazi WA Binti wataona unauwezo WA Kumtunza Binti Yao?😃

Kwa hîyo aliyetoa mahari nyingi ndiye mwenye uwezo wa Kumtunza kuliko Yule aliyetoa ndogo?

Wewe ukipewa na ndugu zako Pesa ukatoe mahari Wazazi WA Binti watachukulia NI kipimo cha wewe kuweza Kumtunza huyo Binti?

Unazungumzia vipi mamilioni ya Watu waliotoa mahari àmbao wanashindwa kutunza Wake zào kimwili, kiroho, kihisia na kiakili?
 
Kwa hîyo mtazamo wenu huo ndio unawafanya mnunue Wanawake?
Hakuna manunuzi hapo, wewe ndio umejenga mawazo mabaya na huu utaratibu.
Je umefanya utafiti wanawake wenyewe wanasemaje kuhusu mahari?
Na je athari za ndoa ya mahari na ambayo haitakuwa na mahari zikoje?
 
Hii ndo ulipaswa uipinge kulazimishwa ila kama anaenda Kwa hiari yake sio.
Chanzo cha kulazimisha ni mahari Kwa hîyo ninapinga chanzo.
Mzazi wamekuja wanaotaka kumwoa Binti Yao watano,
Wakwanza amesema mahari atatoa Milioni 7
Wapili, Milioni 5
Watatu, Milioni 4
Wanne Milioni 2
Watano Milioni 1

Binti anampenda wa mwisho, lakini Mzazi anataka Milioni tatu kwenda juu.

Kingine Cha kupingwa ni Ile kutofautiana mahari na kusababisha uchumba kufa hii haipo sawa kikubwa kama wamekubaliana wao iwe hivo Kwa mahali yoyote Ile.

Mahari ni biashara Mkûu.
Hiyo kukubaliana imekuja kipindi Hiki. Zamani Mchumba unachaguliwa na wàpo waliopinga hii desturi wakaonekana waajabu kama hivi ninavyopinga Mahari.

Ingawaje wàpo walioona Sawa pia kuchaguliwa Wenza kama ninyi mnavyoona mahari ni sawa
Andiko lako lipo sawa ukiamua umtoe Bure sio kosa Wala ukiamua upokee mahari sio kosa. Ni wewe mwenyew utakavyo jisikia

Siô kupokea, Hapa mwenye mamlaka ya Mahari ni Wazazi
 
Wazazi wenye akili timamu hawawez kuchukua mahali
MahaRi anapewa mchumba au mke na sio mzazi
Na huko sio kumnunua bali atanunua mahitaji yake au hata dhahabu wengine tunatoa kama mahari
Mzazi anapewa hela ya mboga tu
Na mtoto ana uhuru wa kuondoka kana ndoa inamshinda na hadaiwi na mtoa mahari
Hapo kanunuliwa vipi
Labda wenzetu wanao katazwa kabisa kutoa Talaka
 
Hakuna manunuzi hapo, wewe ndio umejenga mawazo mabaya na huu utaratibu.
Je umefanya utafiti wanawake wenyewe wanasemaje kuhusu mahari?
Na je athari za ndoa ya mahari na ambayo haitakuwa na mahari zikoje?

Kwa uelewa wako biashara ni nini?

Unaposema tafsiri yàngu kuhusu mahari ni potofu unazingatia Jambo gàni?

Mimi nimezingatia Kanuni za biashara àmbapo mahari imezitimiza zote.

Muuzaji,
Mnunuzi
Bidhaa
Kuthaminisha ubora wa bidhaa
 
MahaRi anapewa mchumba au mke na sio mzazi
Na huko sio kumnunua bali atanunua mahitaji yake au hata dhahabu wengine tunatoa kama mahari
Mzazi anapewa hela ya mboga tu
Na mtoto ana uhuru wa kuondoka kana ndoa inamshinda na hadaiwi na mtoa mahari
Hapo kanunuliwa vipi
Labda wenzetu wanao katazwa kabisa kutoa Talaka

Mahari ya Wapi hiyo Mkuu?

Labda Kwa Waislam lakini hiyo Sheria ya kiislam haitumiki kwèñye jamii za kibantu.

Watu watafunga Ndoa ya kiislam lakini mahari itatamkwa kijadi
 
Mahari ya Wapi hiyo Mkuu?

Labda Kwa Waislam lakini hiyo Sheria ya kiislam haitumiki kwèñye jamii za kibantu.

Watu watafunga Ndoa ya kiislam lakini mahari itatamkwa kijadi
Kwa Waislam boss, tunatoa mahari kwa kuafiki mahari anayotaja mwali
Na utailipa tu na kumkabidhi yeye na sio mzazi
Mzazi hahusiki
Kuhusu mila na jadi hayo ni mengine na sijawahi toa wala kujua
 
Niwie radhi Mkuu

Umebahatika kuwa na Wazazi wote wawili (Me na Ke)? Kama hautajali unaweza kumuuliza Bi Mkubwa(Kama yu angali hai) kama aliolewa Kwa kutolewa mahari ama alichukuliwa bure kwenda kuishi na Mzee?

Tunaweza kujadili mambo ya Ndoa na mahari na kumbe mwenzetu Mtibeli hajaoa wala hana mpango wa Kuoa 🙌

Wazazi Kutoa au kutotoa mahari haiondoi ukweli wa hoja kuwa Mahari ni biashara ya kumuuza Mwanamke Kwa Mwanaume.

NI Mila Potofu kama zilivyo Mila zingine.

Mzazi kufanya Jambo Fulani àmbalo Kwa Wakati wake huenda lilikuwa Zuri haimaanishi Mtoto Afanye Jambo Hilo Kwa nyakati hizi Ambazo Mtoto anaona siô Sahihi.

Mila kama Ndoa za mitala, ukeketaji, Ndoa za Makaburi, Kurithi mjane n.k.
Unàtaka kusema Kwa vile Wazazi wetu walikuwa wakifanya hayo ndîo na Sisi tufanye?
 
Kwa Waislam boss, tunatoa mahari kwa kuafiki mahari anayotaja mwali
Na utailipa tu na kumkabidhi yeye na sio mzazi
Mzazi hahusiki
Kuhusu mila na jadi hayo ni mengine na sijawahi toa wala kujua

Nenda mkoani kaoe muislam wsa kichaga au kisukuma uone kama utaratibu WA mahari utakaozingatiwa ni WA jadi au kiislam.

Juzi hapa nilimsikia sheikhe mmoja akikemea Watu kuchanganya Mila za kijadi na Uislam akazungumzia Hilo la mahari
 
Huna unachokijua kuhusu mahari ndo maana kila mara unakuja na hii mada iki mradi uonekane umeandika.Inaonekana kuna mwanamke ulimtaka mahari ikakushinda.
 
Huna unachokijua kuhusu mahari ndo maana kila mara unakuja na hii mada iki mradi uonekane umeandika.Inaonekana kuna mwanamke ulimtaka mahari ikakushinda.

Mwanamke ukimtaka unaweza ukampata Bila hata mahari.

Hata huyo Mkeo kûna Watu wanaweza kumchukua bure Kabisa.
Hakuna uhûsiano wowote WA kumpata Mwanamke na mahari
 
Nenda mkoani kaoe muislam wsa kichaga au kisukuma uone kama utaratibu WA mahari utakaozingatiwa ni WA jadi au kiislam.

Juzi hapa nilimsikia sheikhe mmoja akikemea Watu kuchanganya Mila za kijadi na Uislam akazungumzia Hilo la mahari
Ni kuchagua moja aidha wafuate Dini au Mila lakini huwezi changanya
Wengi hawajui dini kwa undani na hawaulizi
Ndio maana unaona watu wanagombania mpaka mirathi wakati ukifuata misingi ya dini au ubinadamu tu huwezi kutamani mirathi

Nyumba ya mzee mpaka leo ni ya familia na wajukuu wapo haina mtu bali ni ya familia na haiuzwi wala ndugu kutamani akodishe
Kupanga ni kuchagua
Kama unavyosema hao wanaochanganya mambo huwa wanaingiza mpaka ushirikini
 
Watumwa walikuwa wanauzwa Mpaka Laki Moja wewe Unazungumzia Milioni zote hizô.

MTU hauzwi anayeuzwa na binadamu asiye na Ûtu

Niende Wapi Wakati kîla Siku Naona Watu wanauza na kununua Watu.
Nishakuambia biashara ya kumuuza Mwanamke huitwa Mahari.

NI Sawa usemè mnyama anazaa alafu Mtu anajifungua lakini tukio ni lilelile.
Au mnyama anakunya Mavi alafu Mtu anajisaidia Kinyesi, Jambo ni lilelile lakini lugha Moja imewekwa Kwa staha ili Kulinda heshima ya Mtu.
Ndîo hicho, mahari ni lugha ya staha inayobeba maana ya kumuuza au kumnunua Mwanamke

Nimeshafanya chunguzi ndîo maana nimeandika Jambo hili.
Ninachoandika NI uhalisia

Kwa hîyo wewe mzazi wako kama aliwahi kufanya Kosa Fulani utashindwa kusema Kwa sababu Mzazi wako alifanya?

Au wewe unaweza Fanya Jambo Fulani àmbalo NI Kosa Kisa mababu zako walikuwa wakilifanya?
Tuishie Hapa
 
Back
Top Bottom