Zambia: Hakainde Hichilema atangazwa mshindi wa Urais

Zambia: Hakainde Hichilema atangazwa mshindi wa Urais

Ok, hapo bado hajala kiapo na kuchukua madaraka rasmi!

Tusubiri miaka kama miwili au mitatu ijayo halafu tuone kama uhalisia utaendana na hayo maneno.

I’m not that naive…
 
RAIS MTEULE WA ZAMBIA

  • Nataka tuonyeshe tofauti kati Yetu na wao
  • Nilikamatwa mara 15 na kuwekwa ndani.
  • nilipigwa mabomu
  • Habari za mikutano Yangu hazikutangazwa na TV YA TAIFA

Ili kuonyesha kuwa sisi ni Tofauti na wao

- Nawasamehe wote
-Rais Mstaafu uwe na Amani
  • hakuna Bomu la machozi litakupata
  • Endesha mambo Yako kwa mujibu wa Sheria na hakuna atakayekugusa
  • TV ya Taifa onyesheni mambo Ya wapinzani pia. Msipoyaonyesha watazamaji watapungua. Watazamaji wakipungua hamtapata Matangazo. Mkikosa matangazo Mtakufa na mtafunga
  • wafuasi wangu msilipize Kisasi.
  • kama kuna mtu alikutendea vibaya usilipe kisasi.
  • ukienda ukavamia super makert na kuiba unakua unaharibu KAZI maana kuna watu watakosa kazi na sisi tumeahidi kuongeza ajira

  • wafuasi wangu mkiharibu mali za wapinzani wetu mnaharibu UCHUMI wa Taifa. Mali zao ni mali za Taifa pia. Ukiziharibu unaharibu uchumi
  • wafuasi wangu pelekeni Amani kwa waliowanyanyasa hapo nyuma. Waambieni huu ni wakati wa kuunganisha nchi

  • Taifa lilogawanyika halitashinda VITA ya uchumi
  • Nataka zambia iwe ya Wazambia WOTE bila kujali umezaliwa wapi na umezaliwa na nani mradi wewe ni Mzambia
- Amani ikiwepo Biashara mpya zitaanzishwa. Wawekezaji Watakuja
Ni mapema sana! Tumpe muda
 
Sasa Katiba unaihusisha kwa vipi?
Katiba ndio imempa madaraka makubwa rais aliyopo madarakani kuteua time ya uchaguzi, msajili wa vyama, mkuu wa polisi, mkurugenzi wa Tiss, na wengine wote. Hivyo Basi kwenye mazingira hayo kamwe hawawezi kutenda haki. Ni lazima watampendelea aliyewapa ugali
 
Wakuu karibuni tushirikishane.
  • Nataka tuonyeshe tofauti kati Yetu na wao
  • Nilikamatwa mara 15 na kuwekwa ndani.
  • nilipigwa mabomu
  • Habari za mikutano Yangu hazikutangazwa na TV YA TAIFA

Ili kuonyesha kuwa sisi ni Tofauti na wao

- Nawasamehe wote
-Rais Mstaafu uwe na Amani
  • hakuna Bomu la machozi litakupata
  • Endesha mambo Yako kwa mujibu wa Sheria na hakuna atakayekugusa
  • TV ya Taifa onyesheni mambo Ya wapinzani pia. Msipoyaonyesha watazamaji watapungua. Watazamaji wakipungua hamtapata Matangazo. Mkikosa matangazo Mtakufa na mtafunga
  • wafuasi wangu msilipize Kisasi.
  • kama kuna mtu alikutendea vibaya usilipe kisasi.
  • ukienda ukavamia super makert na kuiba unakua unaharibu KAZI maana kuna watu watakosa kazi na sisi tumeahidi kuongeza ajira
  • wafuasi wangu mkiharibu mali za wapinzani wetu mnaharibu UCHUMI wa Taifa. Mali zao ni mali za Taifa pia. Ukiziharibu unaharibu uchumi
  • wafuasi wangu pelekeni Amani kwa waliowanyanyasa hapo nyuma. Waambieni huu ni wakati wa kuunganisha nchi
  • Taifa lilogawanyika halitashinda VITA ya uchumi
  • Nataka zambia iwe ya Wazambia WOTE bila kujali umezaliwa wapi na umezaliwa na nani mradi wewe ni Mzambia
 
Ujumbe huu uwafikie CCM, chama cha mapinduzi tafadhali kuwa Tanzania ni yetu sote. Na umoja wa taifa hili ni zaidi ya maslahi ya chama na ni zaidi ya madaraka.
 
Kuna watu wimbo wao kwa wananchi kila wakati ilikuwa ni kumtanguliza Mungu mbele lakini cha ajabu kwenye uchaguzi huyo Mungu walimwacha nyuma,abarikiwe sana mheshimiwa Lungu kwa kuheshimu maamuzi ya wananchi wa Zambia.
 
IMG_20210528_133707.jpg
 
Pmj na mapungufu ya chama chetu cha ccm hawa chadema hawawezi kupata madaraka ni wakora sana
 
Lungu mjanja alijua akipora ushindi anaweza kutangulizwa mawinguni kabla hata hajafaidika na wizi wa uchaguzi.
 
Katiba ndio imempa madaraka makubwa rais aliyopo madarakani kuteua time ya uchaguzi, msajili wa vyama, mkuu wa polisi, mkurugenzi wa Tiss, na wengine wote. Hivyo Basi kwenye mazingira hayo kamwe hawawezi kutenda haki. Ni lazima watampendelea aliyewapa ugali
Hoja yako ina mantiki. Je, unapendekeza hao wateule na nani? Kwa vyovyote vile atakayekuwa na mamlaka ya uteuzi ni binadamu. Kama binadamu ana hisia, matakwa na tabia binafsi
 
Hoja yako ina mantiki. Je, unapendekeza hao wateule na nani? Kwa vyovyote vile atakayekuwa na mamlaka ya uteuzi ni binadamu. Kama binadamu ana hisia, matakwa na tabia binafsi
Kuna mamlaka zikiwezeshwa, zitafanya kazi vizuri. Rais akiwa mgombea, awe sawa na wagombea wengine. Magufuli akiwa mgombea uraisi alikuwa na kauli za ajabu Sana, mfano, nireteeni Gwajima, like lilikuwa ni agizo kwa tume ya uchaguzi
 
Leta namba kamili kuhusu nchi nzima siyo cherry picking vipande vinavokufurahisha na kuacha sehemu kubwa isyokufurahisha. Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa 2014,
We mzee kweli unazeeka vibaya nmekwambia ni 40% ukitoa mapingamizi bila mapingamizi ni hyo 34%

Screenshot_2021-08-17-08-56-30-1.png
Hapo kuna vijiji upinzani haukusimamisha na mapingamizi zaidi ya elfu 1 yaliengua wagombea wa upinzani meaning kma walipata 34% licha ya kushiriki chaguzi kwenye less than 80% vijiji na mitaa basi kwa kila mtaa/kijiji waliokuwa head to head na CCM the percentage obviously higher than 40%.

Sasa 2019 Upinzani uliweka wagombea Tanzamia Bara zaidi ya 95% ya vijiji, mitaa, na vitongoji so kama sio zaidi ya wagombea elfu 64 kuenguliwa tungekua na picha kamili ya nani anakubalika kwa grassroots.
 
Back
Top Bottom