Zambia kufunga mpaka wake na Tanzania kwa hofu ya kuenea kwa COVID-19

Zambia kufunga mpaka wake na Tanzania kwa hofu ya kuenea kwa COVID-19

unarudi kule kule kwa magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tutaathirika kwa namna moja au nyingine, moja ya sababu ya nchi yetu kugoma kufunga mipaka yake katika kipindi hiki ni kukwepa athari ya kiuchumi. Sasa wale tunaoona ni wateja wetu nje ya mipaka ya nchi yetu wameanza kugomea huduma zetu! Mteja akisusa, utamhudumia nani? Diplomasia zaidi inahitajika juu ya suala hili la Covid-19.
Hakuna mwenye ubavu wa kugomea huduma mkuu. Amini hilo.

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Wenzetu wakimaliza corona? Duuh! Hivi mkuu hukuwahi kujiuliza kwa nini nchi kubwa za dunia ya kwanza zilishindwa kuzuia ugonjwa huu usingie kwao then wakasubiri uingie ndio wafungie watu ndani?

Amini amini nakuambia kama corona itaisha Zambia, Kenya, Burundi, Rwanda nk na Tanzania pia itaisha. Kama ambavyo ilivyoanza China hakuna aliyeweza kuizuia isiingie nchini kwake vivyo hivyo hakuna atayeweza kuzuia corona ishishe Tanzania wakati dunia nzima imeisha.

Ni Mungu pekee ndio mwenye kujua corona itaisha lini duniani. Hata sasa njia tunazotumia kuudhibiti huu ugonjwa kisayansi tunaita trial and error, hakuna mwenye huwakika na njia yake, ndio maana kuna wengine hufanya total lockdown wengine partial lockdown, wengine wameanza kufuta lockdown na wengine hawakufanya lockdown kabisa. Wote hawa wanaweza kuwa sahihi kwa namna moja ama nyingine maana hakuna mwenye huwakika na njia yake.
unaweza kutofautisha maambukizi ya Taiwan na china ?hawa ni majirani
 
unaweza kutofautisha maambukizi ya Taiwan na china ?hawa ni majirani
Sasa kama Taiwan na China hawafanani kwa maambukizi japo ni majirani, kwanini unataka Tanzania ifanane kwa maambukizi na majirani zake?
 
Lungu kaamua kuondoa katazo la watu kukutana kwenye nyumba za ibada baada ya kuwekwa lockdown mwezi mzima. Viongozi wa dini wamepinga. Wanatala Lockdown iendelee. Wa Tz mnafeli sana. Mtu mmoja akisema wote mnafata kama kondoo. Baadae raisi akaamua ajirudi.
FB_IMG_1587892771903.jpg
View attachment 1430966
FB_IMG_1587892593647.jpg
InShot_20200426_111710573.jpg


Sent From Galaxy S9
 
Ni heri kuweka wazi hali ya maambukizi ili watu wajue ukubwa wa tatizo na kuchukua tahadhari. Huwezi kujificha corona, itakufata popote ulipo. Mombasa Billionaire Who Escaped Quarantine Dies From Covid-19 in Tanzania

Rais mmoja wa huko nchi za nje aliamuru kila anaepata corona ale shaba, lakini Mungu ni mwema,hali aliyonayo hiyo Rais kwa sasa, anaijua yeye na mwili wake.

Malipo ni hapahapa duniani, ukishangilia mwenzio kufa unaanza wewe.

Screenshot_20200427-162030.png


Screenshot_20200427-162114.png

Screenshot_20200427-162135.png
 
Bora nitukanwe!!
Raha sana!!

IF:X=WanaUFIPA+wanamaendeleo,Y=WanaLUMUMBA.
THUS:X=MABADILIKO
Y=WACHUMIA TUMBO!!
 
Mbona hicho kinachotaka kufanywa na Zambia kinaelekeana na moja ya options anazozifikiria Museveni? Museveni amesema kuwa option mojawapo anayoifikiria ni madereva wa malori toka Tanzania waishie pale mpakani. Toka mpakani malori yaendeshwe na Waganda kuingia ndani ya Uganda. Hivyo wasafirishaji watatakiwa kuwa na madereva wawili, mmoja wa kuwepo Tanzania, na mwingine ndani ya Uganda.

Option ya pili wapimwe mpakani halafu waruhusiwe kuendelea ndani ya Uganda lakini wasichangamane na yeyote, waende mpka kituo kitakachokuwa kimepangwa, wasubirie majibu. Ukiwa positive, unaishia hapo hapo. Ukiwa negative, unaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app

..biashara ya usafirishaji / transit cargo ni kubwa na tegemeo kwa uchumi wetu.

..tulitakiwa tujiandae mapema kwa kuwa na test kits za kutosha na maabara za kuwapima wafanyakazi wa sekta hii, kama madereva etc.

..kama wanazungumzia madereva kuwekwa karantini maana yake ni moja tu, kuwa wahusika hawako serious ktk kazi zao.
 
Zambia kufunga mpaka wake na Tanzania wa Nakonde kuanzia kesho Jumatatu, kwa mujibu wa taarifa hii chini hapa.

Nahisi muda si mrefu hatua hii ya kufunga mipaka itaanza kuwa maarufu, na kuchukuliwa na nchi nyingi zaidi!
Nchi zitaanza kufunga mipaka yake dhidi ya majirani zao inayowaona hawachukui hatua kali vya kutosha dhidi ya Corona.

Cc: Sammy awamy
Screenshot_20200510-151240.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam. Kiburi cha kujifanya kuwa una bandari. Wenzio wamejibana wee kwa ajili ya afya za watu wao, wewe unaweka pesa mbele na kufanya juhudi za majirani zako kuwa machozi ya samaki. Sasa atakoma. Wakiondoka, kuwarejesha tena hata baada ya ugonjwa itakuwa siyo rahisi.
 
Back
Top Bottom